Mtu akifa anatakiwa azikwe wapi? Migogoro ya kuzika maiti

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,552
52,226
MTU AKIFA ANATAKIWA AZIKWE WAPI? MIGOGORO YA KUZIKA MAITI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Mwezi Aprili nilifiwa na Bibi yangu kipenzi ambaye ndiye aliyenilea, kwangu alikuwa kama Mama. Nilijifunza mengi kupitia yeye, madhaifu na ubora wake. Mazuri na mabaya yake.

Maziko ya Bibi yangu yalijaa mvutano mkubwa. Wapi Bibi azikwe. Ukoo alipoolewa anasema azikwe Kwao(Chome) wakati watoto wa Bibi(wenye mama yao) wanasema Mama yao(Bibi yangu) azikwe Makanya(kwake alipojenga na alipokuwa anaishi).

Tumempumzisha bibi yetu salama na kwa amani. Lakini mimi Kama Taikon na Mtibeli Halisi kwa makusudi na kwa kujua,na kwa mapenzi nikaona ni vyema niandike ili ku-share uzoefu na wengine wajifunze kwa sababu mambo haya huweza kukukuta au kumkuta yeyote. Hivyo kwa kuandika na kama mtu atasoma itamsaidia siku jambo hilo likitokea kwa mtoto, mzazi, mwenza au ndugu yake kujua nini afanye kwani haitakuwa mara ya kwanza.

Andiko hili kuhesabiwa kama sehemu ya manufaa na yenye kujenga kizazi kilichopo na kijacho katika misingi ya Haki, upendo, kweli na Akili kama tulivyo Watibeli.

Kugombea maiti kuna sababu zake, kila mtu huweza kujipa umuhimu na haki ya kumzika mtu(mpendwa wake) kadiri ya uhusiano uliopo baina ya mhusika na maiti.

Chanzo cha utata katika kugombea maiti na wapi la kuzika;
1. Ndoa.
Tumemuoa Mwanamke huyu hivyo sisi ndio wenye Mamlaka ya kuzika.
2. Malezi
Sisi ndio tumemlea mtoto au mtu huyu hivyo sisi ndio tunauhalali wa kumzika.
3. Vinasaba
Mimi ndiye mzazi wa mtu huyu hata kama sijamlea nina uhalali wa kumzika mahali ninapotaka mwanañgu.
Huyu ni Baba au mama yangu nina uhalali wa kuchagua pakumzikia.

Sasa ni nani mwenye mamlaka ya kuzika na kuchagua sehemu ya kumzika mtu anapokufa?

Wakati mtu anapokufa maneno mengi huzuka na kuzushwa. Mengine huwa ya kweli na mengine huwa ya kutunga tuu. Ilimradi maiti haiwezi kujieleza na kujitetea basi mtu huweza kusema lolote awezalo,

Sio ajabu ukasikia mtu akisema Mama au Baba au mtoto au mjomba au marehemu alisema azikwe sehemu fulani. Hata bila ya uthibitisho.

Kwa Case Study ya Bibi yangu.
Yeye aliolewa ni kweli. Akaanzisha familia na mumewe(Babu yangu). Kisha wakawa na watoto na wajukuu na vitukuu. Kisha Baba alifariki miaka kumi na sita iliyopita. Akazikwa Kwao Chome. Nako kulikuwa na utata kutokana na kile ambacho wengi huita migogoro ya kifamilia lakini hilo lilipita.

Bibi alipofariki, Wazee wa ukoo wa alipoolewa walihitaji Azikwe karibu na mumewe huko Chome. Hoja kubwa hapa ilikuwa ni Aliolewa hivyo wanamamlaka naye kwa sababu hata baada ya kifo cha Mzee(Babu,) hakupata ndoa nyingine(Bibi). Hivyo hiyo ingehesabika kuwa bado Bibi alikuwa chini ya ukoo wa marehemu mumewe.

Ukoo wa Bibi(alipotoka) makundi yalikuwa mawili, wapo waliosema Bibi azikwe alipoolewa yaani kwa Mamlaka ya ukoo wa mumewe. Lakini wapo waliosema kuwa familia yake ndio inamaamuzi ya wapi azikwe Mama yao. Yaani watoto wa Bibi waô ndio wataamua na kusikilizwa.

Mvutano na mgogoro huu ukifuatilia chanzo chake utagundua kuwa kulikuwa kuna mahusiano yasiyoridhisha ya kindoa au tuite migogoro kipindi cha uhai wa Babu na Bibi. Na hii imeenda na kupelekea mgogoro kukomaa mpaka kufika hatua ya juu kabisa na kuleta fedheha na matokeo mabaya katika hatua ya mwisho ya Babu na Bibi katika kuwapumzisha katika makazi yao ya milele.

Taikon kama Mtibeli halisi, naona kuwa migogoro ya kifamilia huweza kufanya Mtu asijivunie ukoo alioolewa au alipozaliwa na hii hupelekea matatizo mpaka wakati wa mazishi.

Mume anaweza asiwe na shida lakini ukoo wa mume unaweza ukasababisha Mke akawa hajivunii kuwa sehemu ya ukoo alioolewa. Halikadhalika mke anaweza asiwe na shida lakini ukoo wake ukawa na shida hali inayoathiri na kuleta matokeo mabaya wakati wa wapi mtu azikwe.

Mimi kama Mjukuu kipenzi niliyekuwa karibu zaidi na Bibi kuliko mtu yeyote, nilijua kabisa kuwa Bibi asingekubali kuzikwa upande wa mumewe, ukoo wa mumewe. Kwa sababu mbalimbali.

Sitamtetea Bibi wala sitampinga kwa sababu yeye alikuwa na sababu zake na sisi Watibeli tunaheshimu maamuzi na chaguzi za Watu wengine. Hata hivyo tuna la kujifunza na hiyo ndio sababu naandika hapa.

Mambo ambayo lazima Watu wayaelewe na ambayo yanatakiwa kujulikana ni kuwa;
1. Ukoo hauna nguvu za kuingilia maamuzi ya familia ya wapi mhusika katika familia azikwe wapi. Ila ukoo utasaidia na kushauri kama ikibidî.
Maamuzi ya ukoo yatakuja kama familia husika Baba na Mama wamekufa na kuacha watoto wadogo wasioweza kujitegemea basi ukoo ndio utaamua mhusika au wahusika wazikwe wapi.

2. Mtu kuolewa katika ukoo fulani haimaanishi kuwa ukoo huo unamamlaka ya kuamua Mwanamke huyo azikwe wapi. Mwenye mamlaka ni Mhusika mwenyewe kama aliomba, au mumewe au watoto wake kama ni wakubwa wanaojiweza kiuchumi.

Mhusika anahaki ya kuamua mahali pa kuzikwa kutokana na mahusiano na mapenzi yake na vile aonavyo.

3. Familia ndio yenye mamlaka ya kuamua mpendwa wao azikwe wapi na azikweje kwa kufuata maelekezo ya mhusika, marehemu kama alitoa hayo maelekezo.
Ikiwa maelekezo ya Màrehemu hayaendani na kipato cha familia husika basi familia inayohiyari ya kuamua vinginevyo.

4. Ndoa sio sehemu ya kugeuza nafsi za Watu kuwa vifungoni. Ndoa ni sehemu ya hiyari/mapenzi. Vile mtu unavyomtendea na mnavyoishi basi ataona haja ya kujivunia ikiwezekana kukupa Mamlaka ya kumzika popote na vyovyote utakavyo,
Hii inaenda sambamba na Mwanamke kuchukua majina ya mume au ukoo wa mume wake. Huo ni uamuzi binafsi wa Mwanamke kutokana na vile ambavyo anaishi na mumewe. Kama anajivunia mumewe ataamua kwa hiyari yake kubadili majina. Kama alivyo na hiyari ya kuyabadilisha vyovyote atakavyo.

5. Kwenye maziko na mazishi fanyeni mazishi kulingana na uwezo na kipato cha wanafamilia bila kutegemea misaada kutoka upande wowote ule. Hii itawasaidia kutokuwa under Pressure na itawafanya muwe katika nafasi nzuri ya kuamua msiba wa mpendwa wenu uweje.
Kwa sisi Watibeli, mazishi ni ibada na sherehe ya kuomboleza maisha ya mpendwa wetu. Tunafanya kwa uwezo wetu na sio sehemu ya kuonyesha ufahari na majivuno kwa Watu.
Fanyeni mazishi yaliyo ndani ya uwezo wenu.

6. Msikubali mtu yeyote aingilie maamuzi ya Familia yenu. Baba na mama na watoto kuhusu wapi pa kumlaza mpendwa wenu. Maamuzi yenu yaendane na kile alichopendekeza marehemu au kile ambacho mnajua marehemu angekipendekeza.

7. Usiwaze msiba wako utakuwaje. Au ushiriki wa Watu utakuwaje. Watibeli hawawezi hivyo. Ila jaribu kuishi kwa Haki, upendo, kweli na akili.
Kujaribu kufikiri msiba wako utakuwaje itakufanya uwe mtumwa na mnafiki ili kutaka msaada ambao kwa wanadamu hautaupata. Mwanadamu wa leo sio wa kesho. Hujui nani atakuzika na hujui kifo chako atashuhudia nani na nani atakuwa kwa kwanza kushika mwili wako. Îshi kwa upendo na haki.

8. Kwa habari za mtoto aliyechini ya utegemezi na ambaye hajitegemei au anayejitafuta ikatokea akafariki basi yeye atazikwa upande aliokulia na kulelewa. Yaani familia au ukoo uliomkuza na kumlea ndio wenye Mamlaka ya kuamua marehemu azikwe wapi na azikweje.

Ikiwa mtoto amelelewa na Baba wa kambo na wakati huohuo Baba yake mzazi yupo na hakutoa malezi au alimtelekeza mtoto, na ikatokea mtoto huyo akafariki, basi mwenye uhalali na mamlaka ya kumzika huyo mtoto ni Baba wa kambo.
Ikiwa mtoto amekua na kujitegemea basi mtoto atazikwa kadiri ya yeye alivyooona, na ikiwa mtoto huyo alijitegemea lakini akawa kama wale Watu wasiofikiri kuhusu kifo(hakupanga wala kuwa na wazo wapi azikwe) basi mtoto huyo hata kama alijitegemea atazikwa kulingana na mahali alipolelewa.

Ikiwa mtoto amelelewa kwa muda wote mpaka anajitegemea kisha akaamua mwenyewe kwa utashi wake azikwe upande wa Baba yake mzazi basi atasikilizwa.

Îkiwa mtoto kalelewa na Mama yake pekee basi mama yake ndio atakuwa na Mamlaka ya kuamua wapi mwanaye azikwe. Lakini kama mtoto amekua mkubwa mtoto ataamua mwenyewe. Lakini mtoto kama amekufa na hakutoa maelekezo yoyote basi mama yake ataamua. Na ikiwa mamaye hayupo na mtoto amekufa basi upande wa mamaye ndio utakaotoa maamuzi,

Acha nipumzike sasa.
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon WA Fasihi
Kwa sasa Kahama
 
Kw

Kwa ukweli kabisa,alitakiwa kuzikwa kwa mumewe.
 
Wachomwe ili kupunguza watu kutambika makaburi na kuombea maiti.
 
Ni upumbavu tu mkuu

Ujinga ujinga

Nimeona baadhi ya koo wanagombania hadi misiba iwe kwa fulani
Msiba unachangia sana nani achukue mirathi.
Akizikwa kiislamu mara nyingi mwanamke anakosa mali, akizikwa ki-kristu mwanamke anapata mali nyingi maana Yesu na dini yake haina ubaguzi wa mwanamke wala mwanaume ila kwenue nuislamu mwanamke anapata 1/8 tu ukisoma Surat al nisa 4:10.
 
Naomba umeamua kutunga Sheria [zako] za maziko.
Kaandika kweli.

Babu yangu alichora mpaka ramani ya wapi azikwe. Bibi nae akasema azikwe pembeni ya mumewe.
Watoto nao wakasema yeyote atakaefariki basi azikwe pembeni ya wazazi wao.
Nasi wajukuu tutazikwa hapohapo bila utata wala ubishi.

Hizi mambo huleta migogoro mno, hapo ndipo watu mliokua na chuki nao hurefusha makucha na kuonesha zile chuki za wazi, visa na meneno ya kebehi na matusi.
 
Ni upumbavu tu mkuu

Ujinga ujinga

Nimeona baadhi ya koo wanagombania hadi misiba iwe kwa fulani
Jambo hili huwa linanishangaza sana. Unakuta miongoni mwa ndugu wanalumbana ,kisa maiti atazikwa na nani, au wapi........mzozo unakuwa mkubwa wakati mwingine hadi uongozi wa Serikali hulazimika kuingilia kati.

La kustaajabisha zaidi wakishazika hata kaburi linasahaulika wakati mwingine hata usafi halifanyiwi
 
Kaandika kweli.

Babu yangu alichora mpaka ramani ya wapi azikwe. Bibi nae akasema azikwe pembeni ya mumewe.
Watoto nao wakasema yeyote atakaefariki basi azikwe pembeni ya wazazi wao.
Nasi wajukuu tutazikwa hapohapo bila utata wala ubishi.

Hizi mambo huleta migogoro mno, hapo ndipo watu mliokua na chuki nao hurefusha makucha na kuonesha zile chuki za wazi, visa na meneno ya kebehi na matusi.
Kama mtu alishasema azikwe wapi ni sawa japo napo sio sheria kwamba lazima iwe hivyo ikitegemea na hali zilivyo wakati huo

Ila hawa wa kugombania misiba na wapi azikwe ni wapumbavu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom