Mnaobeza na kukosoa milo yetu, basi tuambieni tule vyakula gani?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,958
28,073
Muungano OYEEE!!

Wakuu!
Kumekuwa na wimbi la wanaoitwa wataalamu wa afya na lishe kukosoa karibia kila aina za vyakula tunavyotumia kila siku.

Utasikia ugali ni chakula hatari sana kwa afya zetu. Wengine wanaenda mbali zaidi na kusema ugali ni chakula cha mifugo!

Profesa Janabi naye hayupo nyuma, kila kitu anapondea tu.

Lakini sasa hawasemi tunapaswa kula nini kwa matumizi ya kila siku.

Hebu tusaidieni ili na sisi tujiepushe na vyakula vya mifugo na kuboresha afya zetu.

Wasalaam....!!
 
Hao kina Janabi ndo wale unasikia wamekufa kwa sukari,pressure

Kifo kipo tu,huwezi kufa mapema sababu ya kula ugali
 
Kuna mzee mmoja Magomeni alikuaga anasema wasomi wanatudanganya kwamba lazima watoto wasomeshwe sana ili wawe wasomi watoboe kwenye maisha
Watoto wake wote hawajasoma ni wajanja wajanja wa mjini tu na maisha yako poa tu

Kuna watu wanasema baba yangu alikua anakula tungi mtu na sigara kwa fujo lakini kafa na miaka 90 kwa covid, hakuwa na sukari wala nini?

Kuna malaya wanauza K wanaamini zana ni miyeyusho tu swala la kutumia zana ni maamuzi ya mteja tu na kila wakipima hawana HIV wala nini

Siku moja nilikwenda Kijitonyama nilipokulia ule mtaa enzi hizo kulikua na madingi fulani hivi miaka kuanzia 40 walikua wanakula sana pombe na nyama choma kitimoto nk
Nilipokwenda nikusalimia nilikuta nusu yao baada ya kustaafu wamekufa na waliobaki kama wanne wana stroke wengine visukari vimepiga vibaya
Sisemi kama kuna namna ukiishi hauta umwa uzeeni ila kuna namna ukifanya uzee wako most likely utakua wa shida sana

TUSIDHARAU SAYANSI
 
Mara ya mwisho kuangalia list ya vitu haramu nilikuta kuna cocaine, heroin, lean, codeine nk.

Huwezi amini nilimaliza list yote hakukuwa na neno kitimoto.
Inategemea na rejea za orodha yako.
 
Mi nachoamini ni kula kulingana na shughuli unazofanya na kuepuka kula hovyo, kunywa hovyo na ulevi kupindukia.

Hizi mambo za kula muhogo mmoja, sijui ugali au wali kwa ukubwa wa ngumi yako na mamboga tele, kuna wengine utawaua njaa.

Nadhani huo ushauri mwingi wa vyakula ni kwa wale wafanyakazi nyepesi nyepesi za kutumia akili na sio nguvu sana, wafanyakazi wa kazi za nguvu sana wale misosi heavy, matunda kwa sana bila kusahau maji na kutotumia pombe hasa wakati wa kazi.

Hawa wa maofisini, kiti cha kuzunguka, wakaa dukani masaa yote nk ndo wanachangamoto ya kunenepa kama nguruwe mla mashudu kwasababu ya kula hovyo na kunywa hovyo, pia ukumbuke unene sio afya njema.
 
Cha mhimu punguza Kula Kula hovyo ....

Asubuhi unakula supu ya ng'ombe na chapatti tatu ,+peps ya baridi .........unaenda ofsin unakaa tu inazunguka kwenye kiti

Mchana unapiga ugali na samaki mkubwa ,unashushia Tena na pepsi ya baridi .....unarudi ofsin unakaa tu ....

Unatoka ofsin hata kutembea Kwa mguu mwili ufanye digestion Hakuna ...unaingia kwenye gari huyoo bar kumwagilia moyo ,bia 3 na nyama Choma nusu kilo ......unakaa tu na tumbo lako ....

Unafika nyumbani unapiga wali na nyama ,....unakaa tu kwenye sofa ,unaenda kulala....tumbo limejaa unapumulia juu juu kama nguruwe

Mazoezi hufanyi ...


Hicho chakula Hakiendani na Kazi unayofanya kiufupi kinaenda kuwa sumu mwilini ,Hakuna digestion system ....unaanza kufumuka na kuwa na tumbo kubwa ,ini ,Figo zote zinashindwa kufanya Kazi kutokana na mlundikano WA vyakula vya hovyo tu ...sumu unajitengenezea ...hauwezi fikisha miaka 50 Kwa life style hio nakuapia Kwa mwenyezi Mungu .....
 
Muungano OYEEE!!

Wakuu!
Kumekuwa na wimbi la wanaoitwa wataalamu wa afya na lishe kukosoa karibia kila aina za vyakula tunavyotumia kila siku.

Utasikia ugali ni chakula hatari sana kwa afya zetu. Wengine wanaenda mbali zaidi na kusema ugali ni chakula cha mifugo!

Profesa Janabi naye hayupo nyuma, kila kitu anapondea tu.

Lakini sasa hawasemi tunapaswa kula nini kwa matumizi ya kila siku.

Hebu tusaidieni ili na sisi tujiepushe na vyakula vya mifugo na kuboresha afya zetu.

Wasalaam....!!
Naunga mkono hoja-Wanao beza na kukosoa miilo yetu-Wakome kufanywa hivyo. Food is part of our culture. Ni utambulisho wetu kama nchi.

Kukosoa karibia kila aina ya vyakula tunavtotumia nankula kila siku, is an a affront to our nation and our Identity. Kwq bahati mbaya mbaya siwezi kuwapatia hawa watu kuwa na sifa za kuitwa
" wataalamu wa afya na lishe" , kwa maoni yangu, mbali na Daktari Janabi, hawa ni magaidi tu ya mtandaoni-strong assertion indeed, but warranted-they seek vitriol.


Hwapaswi kupewa nafasi ya kutupangia, kututajia tunachpaswa kula, itoshe afya zetu, historically, and statistically zinazoroteshwa na vyakula vya hovyo wanavyo recommend.

Nimekula mihogo yakuchemsha kachumbari na maharage!

Bon Appetit
 
hivi ni mimi alieona sikuhizi wanawake wanavyokula sana kuliko sisi wanaume hlf cha ajabu unakuta wengi wao wanafanya kazi soft soft tu no wonder wanaishia kushuka vitambi
 
Kaka we usihangaike nao, sie tulege tu kujaza matumbo yetu, tule tupate nguvu ya kufanyia kazi tusake ugali mwingine, hali duni ya maisha kwa watz inachangia, familia watu 7, baba kibarua wa ujenzi posho yake kwa siku ni 15k, unategemea huyu mlo wake uwe na maharage, nyama, matunda, mboga za majani.. ngumu sana, hapo ni kilo 2 na maharage kilo, kisha maji kwa wingiii, kila mmoja ashibe
 
Back
Top Bottom