Mfumo wa Kidigitali - Jinsi ya Kuanza

Apr 5, 2024
13
13
Wanajamvi,
Natumaini tunaendelea vyema. Kama mnavyojua, dunia ina kasi ya kidigitali.

Na huenda hutaki kuachwa nyuma.

Juzi kuna lecturer mmoja aliniomba kumsaidia wazo na kudadavua jambo:

  • Ana biashara ya guest house kule dar. Eneo fulani hiv ndani ndani. Sio nyumba moja, zipo kadhaa ndani ya eneo moja.
  • Ana wahudumu wa kusaidia kazi
  • Ana mfumo wa kawaida wa ukusanyaji. Mhudumu anachukua pesa, anahudumia, anapeleka risiti benki.
Aliniita kumsaidia katika haya
  • alitaka kuunda mfumo wa kujua mapato yote. Ili aweze kujua kilichoingia na kilichotoka
  • alitaka kujua utendakazi wa wafanyakazi wake. Wanakuwaga na mkataba wa mwaka mmoja mmoja
  • alitaka kuwa na mfumo "smart" wa kujua anachopaswq kulipia kodi. Si unajua tena...

Nikamshauri
  • awe na mfumo wa point of sale (kama wanayotumia wanaosajili line) kwa ajili ya matzo
  • awe na mfumo wa accounting (uhasibu, kwa ajili ya kufanya mapato na matumizi)
  • awe na mfumo wa HR (rasilmali watu) kwa ajili ya performance appraisal (kupima utendakazi).
  • awe na mfumo wa digital marketing (kuteka masoko kidigitali). Aweze kuchukua details za wateja wakija (namba ya simu, kazi, anakotoka, amekaa muda gani). Aweze kuingiza taarifa hizi kwenye mfumo ili kupiga simu na kujua nature ya huduma.

Je, nilimshauri vizuri? Kuna nlichokisahau,?

Wenye gesti mtupe uzoefu pia. Na wenye kusuka mifumo, karibuni.
 
Hiyo guest inaingiza sh ngapi? Tuone tusije mshauri atumie gharama kuliko uzalishaji
 
Back
Top Bottom