MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,014
16,750
Ni yule ambaye aliripotiwa hapa JamiiForums na Member mmoja nimemsahau jina kuwa alimjeruhi aliyemhusi mwizi wa mkewe (mama Zai ambaye sasa ni mjamzito) kwa kumkata kiukatili sikio na kidole kisha kupita navyo sokoni Kawe akiwa anatamba na kuvionyesha kwa watu huku akisema hakuna wa kumtisha kwani ana hela na uchawi anaujua.

Alikamatwa majuzi akiwa kwa mganga wa kienyeji Bagamoyo na sasa yuko Kituo cha Police Kawe akisubiri kupelekwa Mahakamani Kisutu siku ya Jumatatu kwa kesi yake ya kukusudia kuua.

Pongezi nyingi ziende kwa Jeshi la Police Tanzania na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kwa kuwezeshesha kupatikana huyu mfanyabiashara wa mihogo Kawe Bwana Charahani ambaye taarifa za uhakika zinasema laini (line) yake ya simu ndiyo imerahisisha kukamatwa kwake baada ya Police kwa kushirikiana na TCRA kumuwekea mtego ambao aliuingia.

Mkiambiwa Jamhuri (Serikali) hairogeki na haikimbiwi muwe mnaamini, kwani huyu Bwana Charahani ni bingwa wa uchawi na kuroga na tokea afanye hilo tukio amezunguka mno kwa waganga wa kienyeji ili alisahaulishe hili tukio lakini Mwenyezi Mungu kawalinda vyema Police na watu wa TCRA na hatimaye kakamatwa kama kuku kwa mganga wake wa kienyeji Bagamoyo.

Shikamoo Police Tanzania na TCRA.
 
Ni yule ambaye aliripotiwa hapa JamiiForums na Member Mmoja nimemsahau Jina kuwa alimjeruhi aliyemhusi Mwizi wa Mkewe ( Mama Zai ambaye sasa ni Mjamzito ) kwamkata Kiukatili Sikio na Kidole kisha kupita navyo Sokoni Kaww akiwa anatamba na Kuvionyesha kwa Watu huku akisema hakuna wa Kumtisha kwani ana Hela na Uchawi anaujua.

Alikamatwa Majuzi akiwa kwa Mganga wa Kienyeji Bagamoyo na sasa yuko Kituo cha Police Kawe akisubiri kupelekwa Mahakamani Kisutu Siku ya Jumatatu kwa Kesi yake ya Kukusudia Kuua.

Pongezi nyingi ziende kwa Jeshi la Police Tanzania na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kwa kuwezeshesha kupatikana huyu Mfanyabiashara wa Mihogo Kawe Bwana Charahani ambaye Taarifa za uhakika zinasema Laini ( Line ) yake ya Simu ndiyo imerahisisha Kukamatwa Kwake baada ya Police kwa Kushirikiana na TCRA kumuwekea Mtego ambao aliuingia.

Mkiambiwa Jamhuri ( Serikali ) hairogeki na haikimbiwi muwe mnaamini kwani huyu Bwana Charahani ni Bingwa wa Uchawi na Kuroga na tokea afanye hilo Tukio amezunguka mno kwa Waganga wa Kienyeji ili alisahaulishe hili Tukio lakini Mwenyezi Mungu kawalinda vyema Police na Watu wa TCRA na hatimaye Kakamatwa kama Kuku kwa Mganga wake wa Kienyeji Bagamoyo.

Shikamoo Police Tanzania na TCRA.
What's so special to this guy.
 
Back
Top Bottom