Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,472
- 11,455
Katika orodha ya masharti ya kusitisha vita ni kuruhusiwa kuingia Gaza kwa malori 200 ya misaada mbali mbali yakiwemo kwa uchache malori 4 ya mafuta kila siku.
Masharti hayo yatakayoanza kutekelezwa kesho Ijumaa saa moja asubuhi za Gaza itaanza kwa kutosikika risasi yoyote hewani halafu malori hayo yaanze kuingia kupitia kituo cha Rafah mpakani na Misri.
Wapalestina wakisha kula na kunywa na kushiba na kuchaji simu zao ifikapo jioni saa 10 mateka 13 tu wa mwanzo wataachiwa.
Zoezi hilo litaendelea kama hivyo kwa siku 4 na huenda likaendelea ili kuachiwa kwa mateka zaidi ambao Israel ilishindwa kuwapata kwa njia ya mapigano.
Katikati ya mjadala wa kutekelezwa kwa masharti hayo ya kusitisha vita Israel iliwahi kusema katika kipindi hicho cha siku nne wale wote waliolazimika kuhama kuelekea kusini hawataruhusiwa kurudi eneo la kaskazini.
Sharti jengine Hamas walilokuwa wakilishikilia mwanzoni mwa mazungumzo hayo ni kuwa misaada iingie Gaza nzima bila kubagua kusini na kaskazini.Pia haijajulikana iwapo sharti hilo nalo lilikubaliwa.
Hata hivyo leo wapalestina kadhaa walio kusini wamesikika wakisema kwa furaha kwamba watapata nafasi ya kurudi majumbani kwao huko kuchukua nguo za kuwabadilisha watoto wao,Wakasema japo majumba mengi yamebomolewa lakini itawapa furaha kuyaona kwa mara nyengine.
Kwa kauli hizo za wapalestina haijajulikana iwapo Israel ilibanwa na kukubali kuacha kikwazo cha watu walioko kusini kurudi kaskazini japo kwa muda mdogo.
Kwa hakika kesho itakuwa ni siku ya furaha sana kwa ulimwengu mzima kwa kuona picha za mateka na msururu mirefu ya malori yakiingia Gaza.