SoC02 Madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na matibabu yake kwa ustawi wa jamii

Stories of Change - 2022 Competition

damiro

New Member
Aug 16, 2022
4
3
Andiko langu linahusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na matibabu yake jinsi gani mtumiaji au muathilika wa dawa za kulevya anaweza kupata matibabu na akaludi katika hali ya usawa,

Aina ya dawa za kulevya,
1. Heroin
2. Bangi
3. Cocaine
4. Dawa za tiba zenye asili ya kulevya
5. Milungi


HEROINI
Hii ni aina ya dawa za kulevya inayotokana na mmea wa afyuni (opium poppy) unaulimwa zaidi kwenye nchi za Afghanistan, Pakistani na India na kusafilishwa kwote duniani

Heroini inashika nafasi ya pili kwa matumizi baada ya bangi kwa mujibu wa repoti ya Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya nchini ya mwaka 2021.

Heroini ni dawa inayoongoza duniani kwa kusababisha uraibu au utegemezi sugu, vifo kutokana na kuzidisha matumizi, maradhi mbalimbali pia inawatumiaji wengi wanaohitaji tiba. Dawa hii hujulikana kwa majina mengi mtaani kama unga, ngada, teli, cocktail, msharafu, white, kijiwe, brown nk.

Njia ya matumizi.
1. Kwa njia ya kuvuta kaa sigala vile
2. Kwa njia ya kujidunga
3. kwa njia ya pua wanaita kuseneezi.

BANGI
Hii ni aina ya dawa za kulevya inayotokana na mmea ambao hulimwa, ni aina ya dawa ambayo inashika nafasi ya kwanza kwa kua na watumiaji wengi kwote duniani,
Hutumika kwa njia ya kuvuta na hata kwa kula kwa baazi ya watu.

DAWA TIBA ZENYE ASILI YA KULEVYA
Hii inahusika zaidi kwenye dawa zinazotumika hospitalini kwa matibabu kwa baadhi ya maradhi zinaweza kupelekea mtumiaji kupata hali ya kulevya kama hazitotumiwa sahihi na kutokufata muungozo mzuli wa utoaji wa dawa hizo, moja ya dawa hizo ni kama; Pethidine, Morphine, Tramadol, Fentanyl, ketamine, Benzodiazepam na codeine.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya tarifa ya mwaka 2021 inaonyesha siku za hivi kalibuni kumekua na watu wengi kua wategemezi wa dawa hizi hasa dawa aina ya Tramadol hali hii inatokana na utoaji wa dawa bila usahihi au matumizi mabaya ya mtumiaji au mgonjwa na badae anakua tegemezi wa dawa husika na hata inapelekea wengine kujichoma wenyewe.

MADHARA YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
Matumizi ya dawa za kulevya yana madhala mengi sana kijamii, kiafya,

Kiafya
1.
Hupunguza au kuzohofisha mfumo wa utendaji kazi wa faham.
2. kifo kwa kiwango kikubwa cha matumizi
3. Kukosa hamu ya kula na kudhoofu afya
4. Kupelekea kupata maambukizi ya UKIMWI kwa kuchangia sindano hasa wakati wa kujidunga.
5. Husababisha magonjwa mbalimbali kama ya moyo, ini,mapafu figo, TB na salatani
6. Hupelekea kupata magonjwa ya akili.
7. Kubadilisha mfumo wa hedhi kwa wanawake.

Kijamii.
1.
Dawa za kulevya husababisha kushamili kwa vitendo vya kiarifu katika jamii wizi, ukabaji utapeli uporaji.
2. kunyanyapaliwa na jamii kwa watumiaji wa dawa za kulevya.

MATIBABU KWA WARAIBU AU WATEGEMEZI WA DAWA ZA KULEVYA.

Matibabu ya madhara ya dawa za kulevya hutolewa kulingana na aina ya dawa husika, kiasi cha dawa kilichotumika, Mda wa uraibu, Matatizo mengine ya kiafya na kijamii na mtu binafsi, kwa hapa nchini matibabu haya yanatolewa katika makundi makuu mawili;

1. Huduma za tiba saidizi kwa waraibu kwa kutumia dawa.
Hii hufanya mraibu au muasilika wa dawa za kulevya kupata huduma za tiba saidizi, Medically Assisted Therapy, (MAT)nyingi katika eneo moja kama waraibu wanaotumia dawa za kulevya aina ya afyuni kama vile heroin na baadhi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya hii inahusisha tiba kwa magonjwa yaambatanayo na matumizi ya dawa za kulevya kama vile magonjwa ya akili, UKIMWI, TB, magonjwa ya ngono na homa ya ini.
Kwa hapa nchini hii ni moja ya njia kuu inayotumika kwa matibabu ya waraibu wa madawa ya kulevya kwani zipo kliniki zinazohusika kutoa matibabu haya kwa waraibu wa dawa za kulevya, hizi ni baadhi ya clinic zinazopatikana katika jiji la Dar es salaam, Mhimbili hospital, Mwananyamala hospitali na Temeke hospital.

2. Huduma katika nyumba za upataji nafuu.
Hii hufanya mraibu wa dawa za kulevya kupelekwa kupata huduma za tiba katika nyumba za kupatia nafuu na kuishi huko akiendelea kupata huduma kwa mda flani kwa nchini

NJIA ZA KUJIUNGA NA HUDUMA KATIKA KLINIKI KUPATA MATIBABU YA URAIBU WA DAWA ZA KULEVYA

1. Mraibu anapaswa kuja na kalatasi ya rufaa kutoka asasi za kijamii zinazowaibua, kuwapa mafunzo na kuwaleta kliniki.
2. Atapokelewa na kupimwa uelewa wake kwa yale aliyofundishwa na utayali wake wa kuacha matumizi ya dawa za kulevya na kupata tiba.
3. Atapewa maelezo ya awali kuhusiana na huduma ya methadone
4. Ataonana na Muuguzi, Mshauri wa tiba, Daktali na badae ataanza dawa siku hiyo hiyo.
5. Utapewa utalatibu ni lini atanda tena kuonana na Daktali, Muuguzi na Mshauli wa tiba kujua maendeleo yake na badae ataluhusiwa kuondoka na kuludi kesho yake.

Ujumbe.
Uraibu ni ugonjwa unaotibika hospitalini tuwape ushirikiano wale wote wenye changamoto hii mapate matibabu.

Tukomeshe unyanyapaa kwa watumiaji wa dawa za kulevya.
 
Back
Top Bottom