Esther Bulaya: Serikali iwekeze katika kutibu waathirika wa dawa za kulevya

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
327
419
Ester Bulaya ameshauri Serikali kuwekeza katika kutibu waathirika wa dawa za kulevya, aliongelea kuwa multi clinic Nchini zipo 11 na wanaohitaji matibabu ni maelfu, asilimia ya dawa za kulevya kuzalishwa duniani imeongezeka na siyo dawa zote huwa zinakamatwa Nchini.

Sober House zipo 40 nchini, na tatizo la waathirika wa dawa za kulevya ni wengi sana, ila huwa wanakamatwa tu bila kutibiwa. Hivyo serikali inabidi ifanye mipango mizuri wa kuwekeza katika hizi sober house zilikuwepo na hata kuanzisha zingine ili kuweza kutibu waathirika wa dawa hizo za kulevya Nchini na sio tu kuwakamata.

Kwa mtazamo wangu nahisi jambo hili ni muhimu sana kuwekeza katika rehabilition centers itasaidia sana watu wengi walioathirika, kwa sababu inaweza saidia kuwapa waarithika hawa matumaini na purpose katika maisha yao tena, hizi center hazitibu tu kwa tiba bali kushirikishwa katika elimu mbalimbali na kuoneshwa namna kwa wao kutumia madawa inaathiri vipi watu wengine pia.
 
Hii iende mpaka kwa jamii pia na hao lords wa madawa nao wajitolee japo kinafiki.

Jamii inawajibika kujitengenezea mazingira ya ustawi bora wa kizazi chake na sio jukumu la serikali pekee.

Jamii zetu nyingi tunawajua wasababishi wa uathirika wa vijana na wana jamii wenzetu lakini tumegeuka “Chawa wao kisa senti zao matokeo yake vizazi vyetu ndivyo vinaathirika.

Hao lords wa madawa wakijitolea kinafiki kuweka mazingira wezeshi ya kutibu na kusaidia waathirika, itawasaidia wao pia katika “maslahi yao kijamii.

Maana hata tukipiga kelele kwamba Dawa za kulevya ni mbaya na zinaua kizazi na kufilisi jamii, kamwe unga na mengineyo havitaacha kuletwa na kupitishwa nchini. Ndio dunia tuliyopo.
 
Back
Top Bottom