Maajabu: NHIF yashika namba 1 kwa mashirika ya umma yanayotengeneza hasara

Aramun

JF-Expert Member
Nov 8, 2023
232
1,008
Maajabu hayatakaa yaishe Tanzania. Dhirika linalokusanya mabilioni kwa mwezi ndilo linaongoza kutengeneza pia hasara kwenye nchi.

Kwa hali hii bima kwa wote ni ndoto za mchana. Sheria imeshatungwa lakini kwa kufosi sana. Tetesi ni kwamba feasibility study ya wataalamu ya bima kwa wote ilionesha HAIWEZEKANI.

Ndicho kilichomtoa katibu mkuu wa wizara ya afya mwaka juzi kwa sababu alisimamia uhalisia.

Ila kwa sababu hili jambo linapelekwa kisiasa, basi wakalipush mpaka ikawa sheria.

Namba zinaongea. Zikiongea namba hata mjinga anaelewa. Shirika lilikshindwa kuwahudumia wateja laki 8 litaweza kuhudumia watu milioni 70? HAIWEZEKANI.

Mahospitali makubwa hasa MNH, BMH, JKCI, MOI, KCMC, BUGANDO, MBEYA ZONAL nasikia yana hali mbaya sana kwa sababu NHIF hawajapeleka michango ya wanachama kwa miezi karibu 6 sasa.

Na hizi hospitali kubwa za umma zinajiendesha kwa 90% kwa kutumia pesa za NHIF. Kwa sasa wakuu wa hizi hospitali wanahaha kutokana na package mpya ya NHIF.

Hiyo package mpya inaenda kuzifanya hizi hospitali kubwa za umma zisiweze kujiendesha. Kwa hiyo ni either wizara ndiyo ibebe hilo gap litakalotokea, au warudishe package ya zamani kama ilivyokuwa..

TOP LOSS MAKING PUBLIC INSTITUTION IN TANZANIA

(Losses in Tanzanian shillings)

1. National Health Insurance Fund (NHIF), 𝐓𝐙𝐒 πŸπŸ“πŸ”.πŸ• 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

2. Tanzania Railways Corporation (TRC), 𝐓𝐙𝐒 𝟏𝟎𝟎.πŸ• 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

3. TANOIL Investment Limited, 𝐓𝐙𝐒 πŸ•πŸ”.πŸ“ 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

4. Air Tanzania Company Limited (ATCL), 𝐓𝐙𝐒 πŸ“πŸ”.πŸ” 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

5. Kariakoo Market Corporation, 𝐓𝐙𝐒 πŸ’πŸ.πŸ“ 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

6. University of Dar es Salaam (UDSM), 𝐓𝐙𝐒 𝟏𝟐.πŸ“ 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

7. Tanzania Biotech Products Limited, 𝐓𝐙𝐒 πŸ”.𝟏 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

8. Kilimanjaro International Leather Industries, 𝐓𝐙𝐒 πŸ’.𝟐 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

9. Mbeya Water Supply and Sanitation Authority, 𝐓𝐙𝐒 πŸ‘.πŸπŸ— 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

10. Petroleum Upstream Regulatory Authority (PURA), 𝐓𝐙𝐒 𝟐.𝟐 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧

β–ͺ️ CAG report, fiscal year 2022/23.
 
6. University of Dar es Salaam (UDSM), 𝐓𝐙𝐒 𝟏𝟐.πŸ“ 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧
Tuliambiwa wanazalisha majizi yaliyoko serikalini, itakuwaje wapate faida?
 
Sub company ya TPDC, wanashughulika na Mafuta, wanavyo vituo vyao siku hizi, filling stations.

Hasara sijui inatokea wapi!
Watakuwa wananywesha mafuta magari yao binafsi bila kulipa hao
 
Jana nimecheka sana kusikia eti kuna timu maalumu ya kwenda kuwaombea msamaha hawa waliotia hasara kwa Mh Rais. Nikazidi kucheka zaidi sana niliposikia eti wahusika wanachotakiwa kufanya ni kujutia makosa yao na kuahidi kutokurudia tena basi wanasamehewa..🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Sasa Kariakoo market inaptaje hasara?
Hakika hii nchi ni shamba la bibi, uwajibikaji hakuna kabisa.
 
Hali ni mbaya tunahitaji mabadiliko makubwa ya fukra na sera, tukiendelea hivi kuna siku wananchi nao watapigwa tu mnada.
 
7. Tanzania Biotech Products Limited, 𝐓𝐙𝐒 πŸ”.𝟏 𝐛𝐒π₯π₯𝐒𝐨𝐧
Hii imenisikitisha sana, sasaa kama hasara ni 6B, ina maana mtaji ni kiasi gani?

Halafu kama serikali, isiyolipa mi kodi na yenye access na wataalamu wote wa nchi na yenye soko nchi nzima kwa biotech products inakula hasara. Je mtu binafsi mwenye ndoto ya kumiliki biotech industry ataweza kweli?

Anyway, mnazo bidaa nyingine zipi hata tuzijue na sie tuwaungishe ukiachana na dawa ya mbu, I mean sumu ya mbu. Maana inaitwa biotech products. PRODUCTS zenu ni zipi?
Screenshot_20240421-123902_Chrome.jpg
 
nhif wanaibiwa sana kama hawataweka system kwenye mahospital yote yanayotumia nhif ili mteja aone huduma pamoja na kiasi alichotibiwa kuliko kujazishana maform yale. mm nilienda hospital moja kutubiwa garama ni elfu 40000 sasa nikauliza naweza kuona wap kiasi nilichotumia nisignwakaniambia system mbovu nikaondoka kuja kuchek badae eti sms nimetumia 70000 kwann wasipate hasara.
 
Back
Top Bottom