Kwenu Mashabiki wa Simba na Yanga wenye Viherehere

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,895
5,386
Tukiwa tunaelekea mwishoni kabisa kukamilisha duru ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania,almaarufu kama NBC PREMIER LEAGUE,naomba niwakumbushe mashabiki wa Simba na Yanga ili ikiwezekana waondoe tongo tongo za ujinga ndani ya bongo zao!

Klabu za Simba na Yanga ili zijiendeshe zinahitaji pesa,eidha ni pesa za wadhani,wafadhili,wanachama au kwa ajili ya mauzo ya vifaa vya klabu hizo!.Sasa tunafahamu fika ili klabu ilete wachezaji wazuri ni lazima fungu la uhakika litumike.

Kwa klabu ya Simba ambayo bila shaka kila mmoja wetu hapa anafahamu iko kwenye muundo wa Wanachama na Mmiliki,ambapo wanachama wanamiliki Asilimia 51 za hisa na Mmiliki au tajiri aliyeweka pesa yake yeye anabakiwa na asilimia 49.

Kwa kule Yanga nako itakuwa hivyo hivyo kwakuwa nao wako kwenye muendelezo wa Mabadiliko!

Leo sitawajadili wamiliki wa hizo shea asilimia 49 kutoka kwenye hivyo vilabu,leo naomba niwajadili mashabiki wenye viherehere na midomo mirefu kama chuchunge!.

Unakuta shabiki anakaa huko mitaani,Vijiweni au hata hapa JF akiiponda klabu yake kwamba inafeli kwakuwa inafanya usajili wa Low Budget na hivyo kupelekea kutokufanya vizuri!.

Huyo huyo shabiki mwenye kiherehere ukimuuliza maswali yafuatayo anakuwa hana majibu!

1.Je,Una kadi ya uanachama ya timu yako iliyo hai? - Jibu ni hapana

2.Je,unataka nani awe mwanachama badala yako na alipe Ada ya Mwaka ili wewe uendelee kikenua meno? - Jibu ni kucheka cheka kama Tahira!

3.Je,Msimu mzima ulipoanza umenunua Jezi orijino ya timu yako ili uiwezeshe kimapato? - Jibu ni hapana.

(Hapo unakuta kavaa Jezi ya Chelsea,Liverpool,Arsenal,Barca,Man utd,Man city au Madrid)

4.Je,Unavaa Jezi ya timu za Ulaya na hapo hapo bado unajiita shabiki kindakindaki wa Simba au Yanga huoni utakuwa na matatizo ya kiakili? - Jibu lake ni "Achana na mimi"!.

5.Je,Uwanjani huwa unaenda kila unapopata muda ili kuisapoti timu yako kwenye upande wa Molali ya uwanjani pamoja na Mapato? - Jibu ni Hapana!.


Sasa kama haya yote hufanyi unataka nani afanye badala yako wewe uendelee kukenua meno?,Jezi orijino ya klabu huna,Uwanjani huendi,Kadi ya Uanachama ya klabu huna halafu wakati huo huo unataka timu iendelee kusajili na kufanya vizuri kama unavyotaka wewe!,Hivi kichwani kweli utakuwa mzima?

Mkikaa huko Vijiweni mnaanza kuzitukana hizi timu kana kwamba kuna pesa yako umewekeza hapo na inakuuma kuliko inavyomuuma mwenye ile Asilimia 49!

Kama kweli unaipenda Simba kwanini usiwe mmoja wa wanachama wanaomiliki ile Asilimia 51?,Kazi yako wewe na wajinga wenzio ni kusema kila siku "Mangungu atuachie timu yetu",Mara oooh "MO atuachie timu yetu"

Wewe ukiachiwa timu na MO utaweza kuwanunulia hata maji ya kunywa wachezaji pale kambini?,Au unadhani kuendesha timu ni sawa na kukalia hiyo Boda hapo kijiweni na kung'aa ng'aa macho kutafuta abilia kama Zumbukuku?

Kama siyo Mwanachama unayelipa Ada yako kwa klabu yako nakuomba ukae kimya kiherehere wewe!,Acha wenye kadi zilizo hai wawe na uhalali wa kupaza sauti zao kwasababu hao ndiyo wenye timu,wewe mlala hoi kaa utulie!

Kama Uwanjani huwajawahi kukanyaga na huwa huendi nikuombe uache kiherehere!,Waache wanaoenda uwanjani kuisapoti timu yao waongee!

Kama huwa hununui Bidhaa za timu ikiwemo Jezi Orijino nakuomba uache Kiherehere,wewe endelea kuvaa Jezi za timu yako pendwa ya Liverpool,Man Utd au Arsenal,waache wenye kuichangia timu yao upande wa Jezi waichambue timu yao na siyo wewe Kiherehere!

Umeshaambiwa na timu yako kuwa,Habari za timu yako zote utazipata kwenye Application maalumu ya timu,lakini kutwa ni kuwasikiliza viherehere wenzio kina Jemedari na Wenzie ndio wakupe habari za Klabu yako,Hivi kweli utakuwa na utimamu wa akili?,Hao ni wachambuzi tu wa Mipira na wapiga umbeya,lakini taarifa mahsusi na mara zote hizi klabu zinapatikana kwenye App ya klabu au kwenye mitandao ya kijamii ya klabu husika!.

Unajua kabisa mbali ya taarifa za klabu kutoka kwenye App lakini pia App ni mojawapo ya Chanzo cha Mapato ya Klabu,lakini kila ukiambiwa upakue App ya klabu ili uwe wa kwanza kupata habari za klabu na kuchangia mapato,wewe unaona ni heri ukapukue App ya Umbeya ya Mange Kimambi uendelee kufaidi nyuchi za wanaume na wanawake wenzio wakiwa wanabanduana halafu mwisho wa siku matusi yote na Hasira zote za Maisha yako ukawabebeshe Mangungu na Viongozi wenzie!.

Kama Unajua kabisa wewe ni shabiki wa hizo timu nilizozitaja hapo na hakuna hata moja ulilofanya hapo,ni heri uwe unafunga bakuri (Domo) lako kwakuwa huna msaada wowote kwenye timu unayoiita "Timu yangu".


Nawasilisha
 
Chukua like....waambie hao wasikie...hakuna watu wananiboa kama wale wa Mo tuachie timu yetu....una mbadala? Kuna mtu amewaambia kuwa anaitaka Simba au ndo viherehere vyenyewe....
 
Chukua like....waambie hao wasikie...hakuna watu wananiboa kama wale wa Mo tuachie timu yetu....una mbadala? Kuna mtu amewaambia kuwa anaitaka Simba au ndo viherehere vyenyewe....
Hii dawa ni chungu Miss Kalpana Ni lazima wainywe hivyo hivyo ili wapone!
 
Back
Top Bottom