Kutoka Vita Vya Maji Maji 1905 Hadi Kuasisiwa Kwa TANU Lindi 1955

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,071
30,419
KUTOKA VITA VYA MAJI MAJI 1905 HADI KUUNDWA KWA TANU SOUTHERN PROVINCE 1955

Vita Vya Maji (1905 - 1907) ndiyo kielelezo cha juu kabisa kuonyesha unyama wa Wajerumani kwa wananchi waliosimama kupambana kukomboa nchi yao.

Bahati mbaya sana historia ya vita hii haijaelezwa katika ukweli wake unaostahili.

Katika Makumbusho ya Vita Vya Maji Maji Songea kuna kaburi moja la halaiki wamezikwa wazalendo 76 walionyongwa na Wajerumani.

Hawa walikuwa ndiyo viongozi na majemadari walioongoza vita hii.

Wengi wa majemadari walionyongwa walikuwa Waislam.

Kwa nini iwe hivi?

Historia ya kuasisiwa kwa chama cha TANU baada ya nusu karne baada ya Vita Vya Vya Maji Maji Southern Province (Jimbo la Kusini) itakupa jibu.

Kabla ya Waislam hawa kunyongwa Wajerumani walimleta Fr. Yohannes Hafliger kutoka Misheni ya Peramiho kuwabatiza wazalendo hawa.

Wote walibatizwa na kupewa majina ya Kikristo.

Misheni ya Peramiho ilistawi vizuri baada ya vita hivi na Kusini yote ikawa shwari na tulivu kwa miaka 50.

Hofu ilirejea upya Kusini mwaka wa 1955 Southern Province pale Lindi mjini zilipoanza harakati kuunda chama cha TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hii ni historia ya Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Suleiman Masudi Mnonji, Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sharifa bint Mzee kwa kuwataja wachache.

Nimeweka video tano kueleza histroria hii.

Tafadhali tembelea:



View: https://youtu.be/f5izlAf0MSk?si=yhO6IsnUE-pZlzGv


View: https://youtu.be/eWGW9vONv5w?si=Ye0ROf610kr1DFf2


View: https://youtu.be/rMTxUyanQg0?si=-iWe6cWPM4lgwH8J


View: https://youtu.be/qtEp0VmHsG8?si=v5_aMMiQPXsJEJKi


View: https://youtu.be/DLFdvv-yzbI?si=Rm8cd4RddHT4OWVf
 
Walikuwa Waislam.Bila kuutia Uislam katika porojo zako story haikamiliki.
 
Back
Top Bottom