Kumiliki gari ukiwa Tanzania sio jambo la mchezo... yataka moyo.

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
624
1,523
Wakuu nimetafakari sana nimegundua kumiliki gari ukiwa TZ sio jambo dogo tofauti na nchi jirani. Gari linachukua pesa zako nyingi sana kwa mara moja. Kwa mfano ukiagiza gari ulilolipia labda Tsh 10m itakulazimu uandae kiasi kama hicho ndani ya siku 45 ulipie kodi na gharama zingine za kuingiza gari nchini. Ni jambo zito. Nchi kama Zambia hilo gari la 10m unaweza lipia kiasi kisichozidi Tsh 4m kodi na gharama zingine zote ndo maana majamaa wananunua sana magari. Gari kama Passo wao hulipia Tsh 1.8m hadi 2.6m

Kimsingi ukiwa Tanzania bora ujiunge na kundi la baba wenye nyumba kisha gari ifuatie baadae. Nyumba ya kawaida ukiwa na 2m inafanya kazi kubwa. Vinginevyo unaweza kujiumiza sana kugharamia gari kwa mtu ambaye ndo umeanza biashara au ajira.

Huu uzi uzingatiwe sana na vijana wadogo.
 
Ee ndo ukiona mtu ana gari unatakiwa umuheshimu

Sio matako kila mwanamke anayatingisha
 
Kama vipi tafuta gari humu ndani, muhimu uwe na fundi ifanyie uchunguzi wa kutosha isiwe na matatizo mengi ikakutoboa mfuko.
 
Kumbe ni nyumba vs gari?
Ameongea maneno ya msingi wewe unafanya utani,hebu jaribu kufikiri tu kidodo Zambia hawana bandari na ushuru ni mdogo mno kuliko sisi kwanini tz imekaa kukomoana sana? na kufanya maisha yawe magumu kwa watu wake?? Hii leo ukiwa na Account crdb na kwengine kuangalia salio kwenye Internet banking unakatwa na mijitu ipo kimya hii ni nini??
 
Mi ni mwendo wa tvs pikipiki popote naenda ndani ya mji na gharama ni nafuu
Ulichosema kuhusu gari ni kweli kabisa ukiona ndinga inatamba town aisee jua mwenye nayo hela si shida sana
 
Ameongea maneno ya msingi wewe unafanya utani,hebu jaribu kufikiri tu kidodo Zambia hawana bandari na ushuru ni mdogo mno kuliko sisi kwanini tz imekaa kukomoana sana? na kufanya maisha yawe magumu kwa watu wake?? Hii leo ukiwa na Account crdb na kwengine kuangalia salio kwenye Internet banking unakatwa na mijitu ipo kimya hii ni nini??
Hili suala la kukatwa salio kwa ajiri ya kuangalia salio huwa siliewagi kabisa
 
Nchi ya hovyo,watu wa hovyo na hatujielewi ww watu watengeze gari kwa bei rahisi ili watu waweze kupata huduma ya usafiri.Unakuja kukutana na kodi kubwa kuliko bei ya gari unajiuliza hupati jibu na wala watu hatujali wala kulalamika
 
Viongozi hawataki wtz tununue magari.kodi ni nyingi sana.mafuta nayo Kila siku yanapanda.mfano Kwa Sasa petroli ni 3350 haijawahi kutoka Toka uhuru.ukienda Nchi jirani kama Rwanda na congo ambao wanapitisha gari zao hapa shamba la bibi,gari zao ni bei rahisi sana na ni mpya na za kisasa tofauti na mikweche ya hapa
 
Wakuu nimetafakari sana nimegundua kumiliki gari ukiwa TZ sio jambo dogo tofauti na nchi jirani. Gari linachukua pesa zako nyingi sana kwa mara moja. Kwa mfano ukiagiza gari ulilolipia labda Tsh 10m itakulazimu uandae kiasi kama hicho ndani ya siku 45 ulipie kodi na gharama zingine za kuingiza gari nchini. Ni jambo zito. Nchi kama Zambia hilo gari la 10m unaweza lipia kiasi kisichozidi Tsh 4m kodi na gharama zingine zote ndo maana majamaa wananunua sana magari. Gari kama Passo wao hulipia Tsh 1.8m hadi 2.6m

Kimsingi ukiwa Tanzania bora ujiunge na kundi la baba wenye nyumba kisha gari ifuatie baadae. Nyumba ya kawaida ukiwa na 2m inafanya kazi kubwa. Vinginevyo unaweza kujiumiza sana kugharamia gari kwa mtu ambaye ndo umeanza biashara au ajira.

Huu uzi uzingatiwe sana na vijana wadogo.
Mimi kijana mdogo nipo hapa kujifunza
 
Nchi ya hovyo,watu wa hovyo na hatujielewi ww watu watengeze gari kwa bei rahisi ili watu waweze kupata huduma ya usafiri.Unakuja kukutana na kodi kubwa kuliko bei ya gari unajiuliza hupati jibu na wala watu hatujali wala kulalamika
Jana nimechagua Toyota Vanguard Befoward ya USD 5500, TRA Calculator ikasoma Tax na wadogo zake TSHs 16+ Million! Nimekaa kwanza chini ya Mti!
 
Kikubwa ni kukaza tu,waliopewa dhamana uwezo wa kufikiri ni mdogo.

Magari yangekuwa mengi yangechangia ukuaji wa sekta zingine pia,ajira etc na mwisho wa siku kodi ingepatikana pengine kubwa kuliko kukaba kwenye uagizaji kwa kodi inayozidi bei ya bidhaa.
 
Nyumba ni muhimu japo kwenye safari za hapa na pale gari linasaidia sana
 
Back
Top Bottom