Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 320
- 1,203
Hapa nchini kama tukiacha majungu na unafiki kiungo Kevin Nashon hafanani na kiungo yoyote yule mkabaji, kwa wale walioangala semi final leo baina ya Yanga na Ihefu watakubaliana na mimi kuwa dogo huyu ni fundi hasa lakini haheshimiki, hana bahati.
Mzamiru Yasin ambaye ni kiungo punda hakabi kama dogo huyu, huyu dogo na Yussuf Kagoma ni wakabaji hasa sio masihara, cjui kwanini Mecky Mexime alimtoa kipindi cha kwanza, alihakikisha Aziz Ki hazunguki katika maeneo yake, sio ajabu Aziz Ki amefunga goli na amefurahi sana Kevin Nashon alipotolewa, Nashon aliharibu mipango yote ya Yanga leo.
Nimewahi kuwashauri sana Simba kuhusu huyu dogo, huwezi kumsajili Sawadogo au Babacar Sarr halafu una fundi hapa nchini kama huyu tena ana umri mdogo anaachwa halafu wanasajiliwa wachezaji wa hovyo kabisa.
Kevin Nashon, soma ujumbe huu tunaokufuatilia na kukupenda ni wengi sana, unajua boli, leo umethibitisha kuwa wewe ni zaidi ya Kiiungo Punda, unakaba kuliko hata Yahya Zayd, makocha wetu hapa nchini hawana uwezo wa kubaini kipaji chako lakini wewe ni hatari sana.
Unanikumbusha enzi za Method Mogella Fundi au Iddi Seleman Nyigu (Wote marehem), ukitaka kucheza soka la kistaarabu kama akina Mao Mkami au Nico Bambaga unaweza ukitaka kukichafua kama akina Kibode au Nyigu unaweza.
Natafuta mawasiliano yako nikupe vocha kaka, umenikuna sana kwenye gemu ya leo, ulipotolewa tu sikuhangaika kuangalia tena maana nilishajua mipango imeanza.