Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,851
- 12,088
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi, Faustine Maijo amesema miradi inayotekelezwa na Serikali kwa manufaa ya Wananchi inashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na baadhi ya Watumishi wa Serikali kushindwa kuisimamia ipasavyo.
Maijo amesema Watumishi wa Serikali wanapaswa kuzingatia taratibu za usimamizi wa miradi ili iweze kukamilika kwa wakati.
Amesema Mtumishi atakayeshindwa kusimamia miradi ya Serikali Sheria kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kuwapeleka katika vyombo vya Kisheria.
Aidha, amewaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ili kuzuia na kubaina uzembe au ubora katika miradi mbalimbali.