Kassim Majaliwa: Watu 155 wamepoteza maisha na wengine 236 wamejeruhiwa kutokana na Mvua za El nino

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,851
12,088

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza Bungeli, leo Aprili 25, 2024 ametoa taarifa ya kuhusu mwendendo wa Matuko ya hali ya hewa, athari zake na hatua zilizochukuliwa na Serikali.

Amesema mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kuongezeka kwa mvua katika maeno mbalimbali Duniani ikiwemo Tanzania. Taarifa za tahmini kutoka TMA zimeendelea kuonesha mwelekeo wa kuongezeka kwa kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwemo matukio ya mvua kubwa na upepo Mkali.

Tathmini ya mvua kwa misimu yote inaonesha maeneo mengi yamepata mvua za juu ya wastani ikiambatana na matukio ya hali mbaya ya hewa hususan mvua kubwa na mafuriko.

Ongezeko la joto duniani limesababisha uwepo wa El Nino ambayo imesababisha mvua kubwa zilizosababisha mafuriko nchini kuanzia Mwezi Oktoba-Desemba 2023. Ongezeko hilo la mvua limeshuhudiwa pia kuanzia mwezi Januari-Aprili 2024 na utabili wa TMA unaonesha mvua za masika zitaendelea hadi Mei 2024.

Mvua kubwa za El nino zinazoendelea zikiambatana na upepo mkali, mafuriko na maporomoko ya udongo maeneo mbalimbali nchini zimesababisha athari kubwa ikiwemo vifo, uharinifu wa makazi na mazao mali za wananchi, miundombinu na kutokana na athari hizo zaidi ya kaya 51,000 za watu 200,000 waliathirika ambapo watu 155 walipoteza maisha, 236 walijeruhiwa na nyumba zaidi ya 10,000 ziliathiriwa kwa kiwango tofauti.
 
Attachments

  • TAMKO_LA_SERIKALI_KUHUSU_MATUKIO_YA_HALI_YA_HEWA_NCHINI_25_04_2024.doc
    87 KB · Views: 2
Hawa ndio wahujumu uchumi wakuu wa hili taifa wote ambao wapo Kwenye hilo likikao wanatakiwa kupandishwa mahakamani Kwa kuhujumu uchumi wà hili taifa. THE PIGS
 
Si juzi juzi tu Hapa nilisikia Shehe wa bakwata anaandaa dua ya kumuomba mungu mvua itulie??! au mungu alikua misele?
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza Bungeli, leo Aprili 25, 2024 ametoa taarifa ya kuhusu mwendendo wa Matuko ya hali ya hewa, athari zake na hatua zilizochukuliwa na Serikali.

Amesema mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kuongezeka kwa mvua katika maeno mbalimbali Duniani ikiwemo Tanzania. Taarifa za tahmini kutoka TMA zimeendelea kuonesha mwelekeo wa kuongezeka kwa kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwemo matukio ya mvua kubwa na upepo Mkali.

Tathmini ya mvua kwa misimu yote inaonesha maeneo mengi yamepata mvua za juu ya wastani ikiambatana na matukio ya hali mbaya ya hewa hususan mvua kubwa na mafuriko.

Ongezeko la joto duniani limesababisha uwepo wa El Nino ambayo imesababisha mvua kubwa zilizosababisha mafuriko nchini kuanzia Mwezi Oktoba-Desemba 2023. Ongezeko hilo la mvua limeshuhudiwa pia kuanzia mwezi Januari-Aprili 2024 na utabili wa TMA unaonesha mvua za masika zitaendelea hadi Mei 2024.

Mvua kubwa za El nino zinazoendelea zikiambatana na upepo mkali, mafuriko na maporomoko ya udongo maeneo mbalimbali nchini zimesababisha athari kubwa ikiwemo vifo, uharinifu wa makazi na mazao mali za wananchi, miundombinu na kutokana na athari hizo zaidi ya kaya 51,000 za watu 200,000 waliathirika ambapo watu 155 walipoteza maisha, 236 walijeruhiwa na nyumba zaidi ya 10,000 ziliathiriwa kwa kiwango tofauti.

Hivi ni kweli mhishimiwa huyu alisema magufuli ni mzima wa afya wakati magufuli akiwa ICU?.
 
Nimeona taarifa ya Habari, Al Jazeera,wameandika watu wamepoteza maisha nchini,takribani 155.

Sijasikia hizi taarifa Kwa vyombo vyetu vya ndani,hata hapa jukwani,sijaona tatizo Hilo kupewa uzito. Wenzetu wanaita el nino,sisi tunasema mvua za kawaida.

Hali si nzuri, Serikali ielekeze nguvu kusaidia wahanga na kurekesha miundombinu iliyoharibiwa na Elnino.
 
Mungu Mwema,kama lipo mezani Kwa mtendaji mkuu wa Serikali majibu mazuri tuyatarajie
 
Nimeona taarifa ya Habari, Al Jazeera,wameandika watu wamepoteza maisha nchini,takribani 155.
Sijasikia hizi taarifa Kwa vyombo vyetu vya ndani,hata hapa jukwani,sijaona tatizo Hilo kupewa uzito. Wenzetu wanaita el nino,sisi tunasema mvua za kawaida.

Hali si nzuri, Serikali ielekeze nguvu kusaidia wahanga na kurekesha miundombinu iliyoharibiwa na Elnino.
fatilia vizuri hivyo vyombo vya habari. PM alitangaza idadi ya vifo inayoshabihiana na hiyo uloiona huko kwenye hiyo foreign media 🐒

na kwa hali ilivyo mpka sasa, madhara zaidi na pengine maafa zaidi yanaweza kua yametokea 🐒
 
Mwenyewe nimeona Al Jazeera nimeshtuka kwakweli, vyombo vya ndani mbona havitoi hizi taarifa?
 
Nimeona taarifa ya Habari, Al Jazeera,wameandika watu wamepoteza maisha nchini,takribani 155.
Sijasikia hizi taarifa Kwa vyombo vyetu vya ndani,hata hapa jukwani,sijaona tatizo Hilo kupewa uzito. Wenzetu wanaita el nino,sisi tunasema mvua za kawaida.

Hali si nzuri, Serikali ielekeze nguvu kusaidia wahanga na kurekesha miundombinu iliyoharibiwa na Elnino.
PM alishalisemea, sema media za bongo utakuta zimejaza mic kwenye press za kina manara. Au mpaka mkubwa anayesimamia masuala ya habari awatumie ujumbe WhatsApp (awapangie cha kutangaza) kuwa habari hiyo irushwe kwenye vyombo vyote.
 
Back
Top Bottom