Kamari yatafuna Taifa kimya kimya, Serikali ilizazame hili Kwa makini.

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,858
23,754
Salaam,Shalom!!

Nimesoma tafiti iliyofanywa na Taasisi inayotambulika Kwa Jina la SAUTI KUBWA: Isemayo. " Kamari yatafuna Taifa kimya kimya" iliyoandikwa na mwandishi aitwaye, Arodia Peter , makala hiyo imeandikwa 24 April 2024.

Kwa uchache nasummarize;

Ripoti ya Taasisi ya Utafiti na kupunguza Umaskini Tanzania ( REPOA) ya mwaka 2019, inasema, VYUO vyetu Kwa ujumla wake, vinatoa wahitimu Milioni Moja 1,000,000 Kila mwaka ukilinganisha na nafasi 250,000 zitolewazo na Serikali Kila mwaka.

Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) katika Ripoti yake ya mwaka 2017/2018, inaonyesha kuwa ajira katika sekta binafsi ilishuka Kutoka nafasi 239,017 kutoka 2016/2017 Hadi ajira 137,054 mwaka 2017/2018.

Madhara ya Michezo ya kubahatisha nchini imethibitika inapunguza GDP ya Taifa sababu inatengeneza uraibu hivyo kupunguza nguvu ya kufanya KAZI na kuwaaminisha vijana kuwa betting ni mojawapo ya ajira inayoweza Kutoa kipato.

.............Mwisho wa kunukuu.......

Huu ni mwaka 2024, tatizo limeongezeka zaidi, vijana Kila mwaka wanaingia mtaani, Serikali haijishughulishi kunasaidia kupata ajira Rasmi na zisizo rasmi, wanaruhusu betting utamalaki Ili iwapunbaze wasidai Ajira.

-CHADEMA na CCM wote Kwa asilimia kubwa, wameunganishwa katika mfumo huu hadaa wa betting na hawastuki kupaza sauti.

- Simba na Yanga, asilimia kubwa wanachama wao wanabet, Kila siku wanapeleka pesa huko.

- Boda Boda na vijana wengi sasa ni kubeti Kwa kwenda mbele, wapo wanaobet Hadi 5,000 Kila siku.

- Wanafunzi kuanzia ngazi ya msingi, sekondari, na VYUO wanabet. Wanatumia boom kubeti, wa msingi na sekondari, wanatumia pocket money kubeti, nani wa kuokoa kizazi hiki?

- Wavuvi, bankers, sekta ya biashara, vauza vioski kina mangi wanabet,wakulima wanabet, kiufupi hakuna sekta iliyobaguliwa na kampuni za kubeti.


USHAURI: Ikiwa Serikali imeona Betting ni chanzo kimojawapo Cha ajira nchini na Kodi, itoke na kuwapa TUZO na kuwapongeza Kwa KAZI nzuri ya kuimarisha Uchumi wa Taifa Kwa kutengeneza ajira Rasmi na zisizo rasmi.

KARIBUNI 🙏, Kwa maoni na ushauri kuhusiana na sekta hii muhimu inayoibukia na kuongoza Kutoa fursa za Uchumi wa Hasa vijana ijulikanayo kama "UCHUMI WA KUBAHATISHA".

Karibuni 🙏.
 
Serikali Ipo Ila Ina Usingizi Mzito Na Inatoa Ute Na Kukoroma
Viongozi Wa Serikali Na Wabunge Ndiyo Wenye Biashara Ya Betting
SportPesa Ya Nani?
Wakati Wa Mzilankende Baadhi Ya Viongozi Wa Dini Walipiga Kelele Ikulu Kuwa Betting Ni Haram Sasa Iweje Matangazo Kila Kona
 
DHAMBI IKISHAKOMAA HUZAA MAUTI

🔹 Mtu anaanza betting

🔹Ana advance kuja kwenye li bonanza la mchina

🔹 Anahamia kwenye ndude kipya liitwalo "KINDEGE" hili ndani hata ya siku unaweza kupoteza m.10
 
Back
Top Bottom