Inadaiwa kuna utakatishaji Fedha kwa Mgongo wa Dini: Ongezeko la Makanisa na Wachungaji

Sep 10, 2023
24
68
Nimekutana na hii discussion hapa ikidai kwamba Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la makanisa na wachungaji. Hali hii imeibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa matumizi mabaya ya makanisa kwa ajili ya utakatishaji fedha.

Hapa wadau walikua wanasema hizi ni baadhi ya njia ambazo makanisa yanatumia kutakatisha fedha ,na kwavile taasisi za dini hazina ufatiliaji mkubwa kutoka serikalini mambo yanakua rahisi sana upande huo:

1. Michango ya Fedha:
Michango ya Waumini: Makanisa yanaweza kupokea michango ya fedha kwa wingi kutoka kwa waumini, ambayo inaweza kutumika kama njia ya kuficha chanzo halisi cha fedha hizo. Fedha hizi zinaweza kuwekwa kwenye akaunti za benki za kanisa bila kuulizwa maswali mengi.

• Sadaka za Kila Jumapili: Sadaka zinazokusanywa kila Jumapili zinaweza kuwa njia rahisi ya kuchanganya fedha safi na chafu, na hivyo kuzifanya fedha hizo zionekane halali.

2. Miradi ya Ujenzi:
• Ujenzi wa Makanisa na Majengo: Makanisa yanaweza kuanzisha miradi mikubwa ya ujenzi ambayo inaweza kutumika kutakatisha fedha. Fedha nyingi zinaweza kuingizwa kwenye mradi huo, na kisha kudaiwa kuwa zimetumika kwenye ujenzi, wakati ukweli ni kwamba zimekuwa zikisafishwa kupitia mradi huo.

• Matengenezo na Upanuzi: Miradi ya matengenezo na upanuzi wa makanisa inaweza kutumiwa kwa njia ile ile, ambapo gharama halisi zinaweza kupandishwa ili kuficha kiasi kikubwa cha fedha chafu.

3. Akaunti za Benki za Kanisa:
• Akaunti Nyingi za Benki: Makanisa yanaweza kuwa na akaunti nyingi za benki ambazo zinaweza kutumika kupitisha fedha kwa kiwango kikubwa na kisha kuzitoa fedha hizo kwa kiasi kidogo kidogo ili kuzifanya zionekane halali.
• Malipo ya Wachungaji na Watumishi: Malipo yanayofanywa kwa wachungaji na watumishi wa kanisa yanaweza kufanywa kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida, na kiasi cha ziada kinaweza kurudishwa na hivyo kufanywa kuwa fedha safi.

4. Huduma za Kijamii:
• Misaada kwa Jamii: Makanisa yanaweza kudai kuwa yanatoa misaada kwa jamii kama chakula, mavazi, na elimu. Hata hivyo, kiasi kikubwa cha fedha kinaweza kupita kwenye huduma hizi na hivyo kuficha chanzo halisi cha fedha hizo.
 
Hiyo shughuli inaweza kufanywa na makanisa makubwa na si haya machanga yanayoibuka. Kanisa dogo linawezaje kufanya uchafu huo wakati kumlisha mchungaji wao ni shughuli pevu? Kuna makanisa wanasali kwenye mazingira duni hizo fedha chafu watazipata wapi?
 
Nimekutana na hii discussion hapa ikidai kwamba Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la makanisa na wachungaji. Hali hii imeibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa matumizi mabaya ya makanisa kwa ajili ya utakatishaji fedha.

Hapa wadau walikua wanasema hizi ni baadhi ya njia ambazo makanisa yanatumia kutakatisha fedha ,na kwavile taasisi za dini hazina ufatiliaji mkubwa kutoka serikalini mambo yanakua rahisi sana upande huo:

1. Michango ya Fedha:
Michango ya Waumini: Makanisa yanaweza kupokea michango ya fedha kwa wingi kutoka kwa waumini, ambayo inaweza kutumika kama njia ya kuficha chanzo halisi cha fedha hizo. Fedha hizi zinaweza kuwekwa kwenye akaunti za benki za kanisa bila kuulizwa maswali mengi.

• Sadaka za Kila Jumapili: Sadaka zinazokusanywa kila Jumapili zinaweza kuwa njia rahisi ya kuchanganya fedha safi na chafu, na hivyo kuzifanya fedha hizo zionekane halali.

2. Miradi ya Ujenzi:
• Ujenzi wa Makanisa na Majengo: Makanisa yanaweza kuanzisha miradi mikubwa ya ujenzi ambayo inaweza kutumika kutakatisha fedha. Fedha nyingi zinaweza kuingizwa kwenye mradi huo, na kisha kudaiwa kuwa zimetumika kwenye ujenzi, wakati ukweli ni kwamba zimekuwa zikisafishwa kupitia mradi huo.

• Matengenezo na Upanuzi: Miradi ya matengenezo na upanuzi wa makanisa inaweza kutumiwa kwa njia ile ile, ambapo gharama halisi zinaweza kupandishwa ili kuficha kiasi kikubwa cha fedha chafu.

3. Akaunti za Benki za Kanisa:
• Akaunti Nyingi za Benki: Makanisa yanaweza kuwa na akaunti nyingi za benki ambazo zinaweza kutumika kupitisha fedha kwa kiwango kikubwa na kisha kuzitoa fedha hizo kwa kiasi kidogo kidogo ili kuzifanya zionekane halali.
• Malipo ya Wachungaji na Watumishi: Malipo yanayofanywa kwa wachungaji na watumishi wa kanisa yanaweza kufanywa kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida, na kiasi cha ziada kinaweza kurudishwa na hivyo kufanywa kuwa fedha safi.

4. Huduma za Kijamii:
• Misaada kwa Jamii: Makanisa yanaweza kudai kuwa yanatoa misaada kwa jamii kama chakula, mavazi, na elimu. Hata hivyo, kiasi kikubwa cha fedha kinaweza kupita kwenye huduma hizi na hivyo kuficha chanzo halisi cha fedha hizo.
Kwanini makanisa tu!? Misikiti haina miradi? haina sadaka? Haina waumini wanaoweza kushirikiana na viongozi wao kutakatisha fedha!? Wajukuu wa madevu mbona chuki zenu zimepita kiasi!?
 
Sijui lini wa Africa tutakua tunafikiria nje ya boksi juu ya hizi dini za ajabuajabu hamka ndugu yangu jamaa ajaiponda dini yako Bali ametuhabarisha Mambo yanavyoenda.
 
Kwanini makanisa tu!? Misikiti haina miradi? haina sadaka? Haina waumini wanaoweza kushirikiana na viongozi wao kutakatisha fedha!? Wajukuu wa madevu mbona chuki zenu zimepita kiasi!?
Ile misikiti iliyokuwa inajengwa mingi na kwa kasi kuanzia miaka ya mwanzo 2000 naona wanajisahaulisha.Hadi leo kuna viashiria hatarishi.Safari za nje kama Uganda na Uarabuni haziishi.
 
Kwa hiyo hata wale wawili waliokufa inawezekana ni u mafia ndani ya dini hizi kumalizana kwa ajili ya fedha
Labda alishinikizwa kuandika barua
Dunia ya leo usiamini chochote maana hali imekuwa ngumu kila kona na mbinu zinaongezeka
Kama wale viongozi wa Vatican walipiga mamilioni ya hela wakiwa na waweka hazina itakuwa sisi
Money laundering imejaa kila mahali
 
Ukivutia bangi chooni lazima utakua na mawazo ya kipumbavu kama haya
 
Back
Top Bottom