Tetesi: Ilikuaje Makontena 329 yakapotea bandari kavu ya Azam na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Bilioni 12.6? Je, Nani alicheza huu mchezo?.

Jan 28, 2024
96
133
UFISADI WA MAKONTENA 329 BANDARI KAVU YA AZAMU ICD (2015)
To make a long story short,
Kama umekua mfatiliaji wa mambo, utakumbuka mnamo December, 2015, Waziri Mkuu Majaliwa alifanya ziara TPA na kumuhoji Meneja wa TPA, (Abel Muhanga kwakipindi hiko), kuhusiana na tuhuma za ufisadi wa kupitisha makontena 2431 bila kulipa ushuru kwa TRA
View: https://youtu.be/4o6lt6KZKaw?si=EzVDTurOLGLJzot9).

Hii ilifuatiwa na kukamatwa kwa watu 8 siku moja baadaye

View: https://youtu.be/nwsMxK_UHnk?si=P2AG_gD8jmDofiay),
na hatimaye, December 12 zaidi ya watu 40 walishikiliwa na jeshi la polisi chini ya Kamanda Kova kwa tuhuma za upotevu wa makontena 329 kati ya hayo 2431

View: https://youtu.be/kGs7KWU4cDw?si=hqAxiIIxqNw_2Uuo).
(Nitarudi kwenye hii story baadae).

Ikumbukwe, Mwezi huohuo, Dr. Mpango, akiwa kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, alitangaza ugunduzi wa makampuni

43


yaliyohusika na ukwepaji kodi na utoroshaji wa makontena 329 kutokaka TPA na kuwa Makampuni 15 kati yao yalikubali kulipa madeni yao, hivyo kubaki na makampuni 28 yenye madeni, na hii ikapelekea watumishi 35 wa ngazi mbalimbali TRA kusimamishwa kazi.

View: https://youtu.be/_ROlG1a8SJ0?si=mYJbrkLK89L_0nor.

images (36).jpeg


Mnamo Novemba 10, 2016, kampuni ya udalali ya YONO ilithibitisha kupewa tenda na TRA ya kufilisi wateja 24 kati ya 28 waliokuwa wanadaiwa kodi ya Tsh. 18.95 bilioni kwa utoroshaji wa makontena 329 katika bandari kavu ya Azam ICD(taarifa kamili go to hii 👉 Thread "Bandari kwalipuka. Wateja 24 kufilisiwa kwa kutorosha makontena' Bandari kwalipuka. Wateja 24 kufilisiwa kwa kutorosha makontena".
IMG_20240402_155414.jpg

Lakini maswali yalibaki pale pale, ni kena nani wapo nyuma ya huu mchezo wote?🤔, ama kwa lugha nyingine. Ni kena nani wahusika wa Issue hii🤔?

Ku connect dots, sasa hapa nitarudi kwenye ile story ya wale watu 40 waliokua wameshikiliwa na jeshi la polisi chini ya mzee wetu Kova. Baada ya uchunguzi kufanyika ni watu 7 pekee kati ya wale 40 ndio waliofunguliwa mashtaka na ni watano pekee ndio walikutwa na kesi ya kujibu. Ambapo mnamo tarehe 25 Machi 2019 Jaji Korosso aliwaachia huru wawili kati ya hao watao ambao ni Haruni Lyson Mpande na Khamis Ally Omar. Hata hivyo, Raymond Adolf Louis na Khalid Yusuph Hassan, wafanyakazi wa Bandari Kavu ya Azam ICD, pamoja na Benson Vitalis Malembo, mfanyakazi wa kampuni ya Region Cargo Service, walihukumiwa vifungo na faini ya pamoja.
Screenshot_20240402-063416~2.jpg

Raymond na Khalid walipewa kifungo cha miaka mitatu kwa makosa 105 ya kughushi nyaraka, kinyume na vifungu namba 333, 335(a)(d)(i), na 337 vya Sheria za Kanuni ya Adhabu (Penal Code). Lakini wote kwapamoja na Bw. Benson walihukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kuisababishia serikali hasara ya Tsh. 12,618,970,229.00, kinyume na fungu la 10(1)&(4) la jedwali la kwanza pamoja na kifungu cha 57 (1) na 60(2) vya Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa (EOCCA).

Pia, mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi almaalufu kama Mahakama ya Mafisadi iliwahamuru watuhumiwa kulipa Tsh. 2.15 bilioni kila mmoja, jumla ya Tsh. 6.35 bilioni kwa wote, kwa Mamlaka ya Mapato (TRA), ikiwa ni nusu ya hasara iliyosababishwa na watuhumiwa hao. Hata hivyo, Bw. Raymond na Khamis walikata Rufaa kwenda mahaka ya rufani, ambapo kufikia January 27, 2022 Mahakama ya rufani chini ya majaji watatu ikiongozwa na Jaji Ndika ilitupilia mbali rufaa hiyo kwakukosa mashiko. Full Judgment 🔗👉 Raymond Adolf Louis & 2 Others vs Republic (Criminal Appeal 120 of 2019) [2022] TZCA 3 (27 January 2022).

Natamani kuelezea hii story yote ya namna hili game lilivyochezwa na hivi vichwa (Kena Raymond) lakini kwa leo wacha niishie hapa tu. Nitashare PDF ya case zao kwa faida ya anayetaka kwa undani kuhusu game lililochezwa na kena Raymond.


 

Attachments

  • Screenshot_20240402-063416~2.jpg
    Screenshot_20240402-063416~2.jpg
    106 KB · Views: 3
  • images (37).jpeg
    images (37).jpeg
    41.7 KB · Views: 3
  • images (37).jpeg
    images (37).jpeg
    41.7 KB · Views: 3
  • Republic vs Raymond Adolf Louis Others (Economic Case 1 of 2017) 2019 TZHC 2116 (27 March 20...pdf
    4 MB · Views: 4
  • Raymond Adolf Louis 2 Others vs Republic (Criminal Appeal 120 of 2019) 2022 TZCA 3 (27 Januar...pdf
    701.6 KB · Views: 4
Nchi Inachezewa Sana Halafu Eti Viongozi Wapo Mbele Kimya Kama Hawaoni Lolote
Kama Ni Uzushi Leteni Ufafanuzi Sasa
 
Sasa pata picha enzi za Msoga ilikuwaje, kuhusu kauli ya Mwendazake ya kuwa nchi inachezewa unaweza kuona uhalisia ndani yake

Hakika alimaanisha kutoka moyoni
 
Back
Top Bottom