Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,472
- 11,455
Kumekuwepo na nukta ambazo zimekwamisha makubaliano ya kusitisha vita kwa muda mrefu kati ya Israel na Hamas.
Israel imeshikilia haitaki kuona Hamas ikiendelea kuitawala Gaza na la plli ni kupata mateka wote wanaoendelea kushikiliwa na Hamas.
Kulikuwa na baadha ya nukta pia viongozi wa Hamas na makundi mengine yanayopigana ndani ya Gaza hawakuweza kuyaweka sawa kwa wenzao walioko nje.
Ismail Haniye amekuwa akipendelea kusitishwa kwa vita kwa muda na kuachia baadhi ya mateka na baada ya hapo mazungumzo yaendelee.Hata hivyo viongozi wenzake waliopo Gaza walipendelea kuendelea na vita wakiona mipasuko ya ndani ya Israel inafanya ushindi uwe karibu yao.
Yawezekana kujitokeza kwa Yahya Sinwar na kupata muda wa mazungumzo na wenzake kumesawazisha mambo hayo.
Kwa sasa ni rasmi kwamba Hamas imekubali kufa na kuachia mateka wote inaowashikilia ili kukamilisha ajenda ya Israel.
Hata hivyo wapiganaji hao wametoa sharti la kuundwa kwa taifa la Palestina kwanza ambapo na wao watajiunga na mamlaka nyengine ya Palestina itakayotawala Gaza na ukingo wa magharibi kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967.