Kavimbe
Member
- May 9, 2023
- 34
- 53
Fundi Cherehani (Tailor) na Fundi Mbao (Carpenter) ni mafundi wenye maajabu.
Wewe kama huamini haya maneno au hujawahi kuona maajabu yao basi mtafute ndungu yako au rafiki yako wa karibu amabaye ni fundi nguo au fundi mbao, halafu umuulize vipi bwana kazi zinakwendajee siku hizi. Moja kwa moja atakwambia.. siku hizi ni doro hakuna kabisa wateja wanaohitaji vitanda wala kabati. Watu wananunua fenicha cha China. Na fundi nguo na yeye atakujibu hivyo hivyo.. hakuna kazi kabisa siku hizi watu wananunua nguo special tu sisi hatuna kazi.
Baada ya majibu hayo.. kama ndugu yako au rafiki yako ni fundi mbao basi mwambie mimi ninahitaji kitanda, jee ni shilingi ngapi? Hapo hatakwambia bei yake moja kwa moja kwa vile ni jamaa yako wa karibu, ataanza na hesabu zake za kitaalamu. Atakwambia kitanda kinahitaji mbao 12 za ngapi kwa ngapi, pia kunatakiwa mbao ngapi za ngapi kwa ngapi. Halafu tuzipeleke mashine, halafu kuna msasa, misumari, vikomeo vya droo. Wewe utamwambia sawa piga tu hisabu ya vitu vyote. Basi atachorachora chini aridhini halafu ataibuka na kukupa jibu la thamani ya vitu vyote pamoja na ufundi wake. Atakwambia kama laki tatu na elfu sabini hivi. Kwa vile ni mtu wako wa karibu na hana kazi katika kazi zake basi utamwambia sio tatizo ninakupa pesa taslimu laki nne ili unifanyie kazi yangu.
Baada ya kumkabidhi pesa unamuuliza ni lini kitanda changu kitakuwa tayari. Hapo atakupa tena utaalamu wa kazi kazi yake. Kesho nitakwenda kununua mbao, halafu nitazipeleka mashine halafu zitakauka ndio nitaanza kazi ya kuzichonga. Jibu hapo atakwambia baada ya siku sita kitanda kitakuwa tayari. Wewe kwa vile ni rafiki yako unamwambia mimi ninakupa wiki mbili ili unifanuyie taratibu.
Sasa hapo ndio maajabu yao mafundi yanapoanza. Zile wiki mbili zitafika na utamuuliza vipi kitanda tayari. Atakwambia keshokutwa kitakuwa tayari. Na keshokutwa ikifika ukimuuliza vipi nije nichukuwe kitanda changu. Atakwambia nivumilie kidogo siku mbili tatu hivi. Kwa vile ni rafiki yako unampa tena wiki mbil. Baada ya wiki mbili ukienda atakwambia bado kidogo kwa sababu nilipata kazi ya kufunga milango kwa Mpemba Mbagala Chini.
Yaani hapo itapita miezi sita kama si miezi tisa bila kupata kitanda chako. Kumbuka mwanzoni alikwambia siku hizi hakuna kazi. Ni kwanini kama hakuna kazi kitanda tu kinachukua zaidi ya miezi sita kukitengeneza.
HAYO NDIO MAAJABU YA FUNDI MBAO NA FUNDI NGUO NI HIVYO HIVYO AMTAFUTE NA UMPE KAZI YAKO ILI UONE MAAJABU YAKE NA YEYE.
WASALAMU ni BabuAli Wa Baraka.. baba wawili.