FT: Simba SC 2 - 0 Singida Fountain Gate | Mapinduzi Cup| Aman Complex | 03.01.2024

Match Day
Simba Vs Singida FT FC.
Time: 20:15.

View attachment 2860453

All the Best Mnyama
#nguvumoja#

Hii Match ni muhimu kwa Simba ila haina Pressure kabisa.

Simba wanahitaji point 3 ili kuingia robo fainali.

Nimejaribu kutengeneza Standing Table ya Kundi B.

Singida FG yeye ameshaingia Robo fainali, anakuja kukamilisha ratiba tu.

Tizama Msimamo wa Kundi B
View attachment 2860651

Simba anapaswa kushinda hii game ili game ya Mwisho na APR iwe rahisi zaidi.
Simba 2
Singida 1
 
😅😅😅 hapa ndio tunaanza kuona ubovu wa kocha wa 2 kwa ubora Afrika ya msimbazi!. Kwa kikosi lonyalonya hiki Cha simba, tutegemeee mnara wa 3 au 4G kabisa.
 
Simba anakazwa leo, alafu anashika nafasi ya pili anadondokea mikononi mwa Azam 🤭🤭🤭 Ila nyiee
 
hakuna ulazima wowote wa Singida fg kushinda hii game.

kwanini utumie risasi kuua kitu kisichokuwa na manufaa? nawashauri washughulike na hatua ya robo fainali sasa. mpira ni mbinu
Ulazima upo kwenye kutengeneza jina..!!
 
Singida Fg hapa itabidi waingize kikosi B.
Hawana cha kupoteza na nitawashangaa sana endapo watakamia
Hata kama hatuna cha kupoteza, sisi Singida tunaweka full mkoko. Kama kukamia na nyinyi mtukamie tu halafu tukutane baada ya dk90
 
Kocha aanze na kikosi kile kile ili tuone improvement na baadhi ya makosa kama yamefanyiwa kazi. Wachezaji 3 ambao wamelaumiwa sana - Jimmyson, Chilunda na Duchu mi naona hawa wanahitaji dakika zaidi uwanjani ili waonyeshe walichonacho kumbukeni wamekaa benchi sana na kama mnavyojua mchezaji asipocheza week in week out ni anakwisha. Miquisoone pia bado hajawa kwenye ubora wake ingawa alihusika kwenye magoli 2 kati ya yale 3. Generali vilevile bado kurudi kwenye ubora wake ingawa anatia moyo.

Otherwise naona Simba akimwadhibu vikali Singida.
kwamba mechi ya singida mnataka iwe ya majaribio? Benchikha ni mtu mwenye tamaa ya makombe na mapicha picha hawezi kufanya huo ujinga hao akina duchu wataozea benchi kama lilivyo jina la kocha wenu
 
kwamba mechi ya singida mnataka iwe ya majaribio? Benchikha ni mtu mwenye tamaa ya makombe na mapicha picha hawezi kufanya huo ujinga hao akina duchu wataozea benchi kama lilivyo jina la kocha wenu
Duchu akikaa benchi nani ataanza kwa mtazamo wako?
 
Match Day
Simba Vs Singida FT FC.
Time: 20:15.

View attachment 2861011

All the Best Mnyama
#nguvumoja#

Hii Match ni muhimu kwa Simba ila haina Pressure kabisa.

Simba wanahitaji point 3 ili kuingia robo fainali.

Nimejaribu kutengeneza Standing Table ya Kundi B.

Singida FG yeye ameshaingia Robo fainali, anakuja kukamilisha ratiba tu.

Tizama Msimamo wa Kundi B
View attachment 2860651

Simba anapaswa kushinda hii game ili game ya Mwisho na APR iwe rahisi zaidi.
Naiona Yanga ikichukua ubingwa wa ligi ikiwa bado mechi 15 mkononi
 
Back
Top Bottom