SoC03 Elimu yenye manufaa

Stories of Change - 2023 Competition

Hizb Tahrir Tanzania

JF-Expert Member
Feb 18, 2020
258
235

ELIMU YENYE MANUFAA

1.0 UTANGULIZI
Mfumo wa elimu nchini Tanzania anakabiliwa na chngamoto nyingi kama vile matumizi ya muda mrefu katika kutafuta elimu, mrundikano wa masomo na mada zisizo akisi uhalisia wa maisha ya sasa, kushindwa kumuwezesha mwanafunzi kujitegemea na kujiajiri na kadhalika. Andiko hili linalenga kuangazia kwa ufupi changamoto ya kupoteza muda mwingi kwa mwanafunzi katika kutafuta elimu na wingi wa masomo yasiyo na manufaa hitajika.

2.0 TATIZO LA WANAFUNZI KUPOTEZA MUDA MWINGI KATIKA KUTAFUTA ELIMU
Mfumo wa elimu wa sasa nchini unamfanya mwanafunzi kutumia muda mwingi katika kusoma kwani kuanzia elimu ya msingi mpaka shahada ya kwanza hulazimika kutumia jumla ya miaka 16 iwapo atasoma moja kwa moja bila kusitisha masomo yake. Katika shule ya msingi ni miaka saba, elimu ya sekondari ni miaka sita na elimu ya chuo kikuu kwa shahada nyingi ni miaka mitatu. Huu ni muda mrefu kwani vijana huhitajika katika jamii mapema ili waweze kunufaisha jamii kwa muda mrefu zaidi.

2.1 JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA WANAFUNZI KUPOTEZA MUDA MWINGI KATIKA KUTAFUTA ELIMU
2.1.1 KUPUNGUZA UMRI WA KUANZA SHULE YA MSINGI KUTOKA MIAKA 7 MPAKA MIAKA 5

Badala ya mwanafuzi kuanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka saba, ni vizuri mwanafunzi akaanza shule akiwa na miaka mitano kwani ni umri muafaka ambao mtoto anaweza kuanza kujifunza kusoma, kuandika, kusikiliza, kutamka na kuhesabu hesabu za awali. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni ,katika taarifa yake kuhusu umri wa kuanza shule ya msingi(UNESCO Institute for Startics, Primary school starting age,2021), umri huu unatumika na nchi nyingi duniani kama vile Uingereza, Burma,Mauritius, Nepal, Sri Lanka na kadhalika.

2.1.2 KUPUNGUZA MIAKA YA KUSOMA ELIMU YA MSINGI KUTOKA MIAKA 7 MPAKA 6
Kwa sasa wanafunzi hutumia miaka saba kusoma elimu ya msingi nchini, badala yake wasome miaka sita, ambayo inatosha kabisa kumaliza masomo ya elimu ya msingi. Kwahiyo kutakuwa na darasa la kwanza mpaka la sita na mwanafuzi aliyeanza akiwa na miaka mitano atamaliza elimu ya msingi akiwa na miaka kumi na moja.

2.1.3 KUPUNGUZA MIAKA YA KUSOMA ELIMU YA SEKONDARI KUTOKA MIAKA 6 MPAKA 4
Elimu ya sekondari inaweza kusomeshwa kwa muda wa miaka minne. Kwahiyo mwanafunzi aliyemaliza shule na miaka kumi na moja ataanza elimu ya sekondari akiwa na miaka kumi na mbili na atamaliza elimu ya sekondari akiwa na miaka kumi na sita. Kwa mfumo huu, mwanafunzi ataanza shahada yake ya kwanza (bachelor degree) akiwa na umri wa miaka kumi na saba na kumaliza akitimiza miaka ishirini kwa shahada nyingi ambazo zinatumia miaka mitatu. Kwa mfumo huu tutakuwa tumeokoa miaka mitano kutoka kuanza elimu ya msingi mpaka kumaliza shahada yake ya kwanza ambayo mwanafunzi anapoteza katika mfumo wa sasa kwani katika mfumo wa sasa.

3.0 MASOMO YA KUSOMA YATAKAYOMNUFAISHA MWANAFUNZI NA KUMFANYA AWE MTU MWEMA KATIKA JAMII, ANAYJITEGEMEA NA MWENYE UWEZO WA KUJIAJIRI BAADA YA MASOMO
3.1 MASOMO YA SHULE YA MSINGI
3.1.1 DARASA LA KWANZA MPAKA LA TATU (MIAKA 5-8)

Hii ni hatua ya mwanzo ya kusoma, hapa mwanafunzi atasoma masomo makuu ya msingi manne ambayo ni maadili, kiswahili,kiingereza, sayansi na hesabu. Mwalimu atawapa wanafunzi ujuzi na kuendeleza uwezo wao wa kufikiri na kufanya kazi,kutengeneza vitu, kuchora, kusoma, kuandika, kusikiliza, kutamka, kazi za bustani na michezo ya viungo(physical education)

3.1.2 DARASA LA NNE MPAKA LA SITA (MIAKA 9-11)
Hapa mwanafunzi huwa amekomaa na mwenye kuweza kudadavua mambo zaidi. Atasoma somo la maadili, kiswahili, kiingereza, sayansi, hesabu, kompyuta na historia. Katika sayansi mwanafunzi atajifunza utangulizi katika masomo ya kemia, fikizia, baiolojia na jiografia. Mwalimu atawapa ujuzi wanafunzi na kuendeleza uwezo wao kupitia kuchora, mashamba darasa, mafunzo stadi(vocational trainings), kujisomea(library) na elimu ya viungo(ukakamavu)

3.2 MASOMO YA SHULE YA SEKONDARI
3.2.1 KIDATO CHA KWANZA MPAKA CHA PILI (MIAKA 12-14)

Mwanafunzi atasoma masomo aliyosoma darasa la nne mpaka la sita kwa upana zaidi, kwahiyo atasoma maadili, kiswahili,kiingereza, sayansi, hesabu, kompyuta na historia. Mwanzafunzi atatumia muda mwingi katika kujisomea na utafiti mdogo wa kivitendo katika masomo yote.

3.2.2 KIDATO CHA TATU (MIAKA 15)
Hapa mwanafunzi atachagua mchepuo kutokana na mapenzi yake na ufaulu wake, na atasoma kwa muda wa mwaka mmoja. Badala ya mitatu ya sasa(sayansi, sanaa,biashara) kutakuwa na sita ambayo ni sanaa, biashara, sayansi, viwanda, kilimo na sayansi kimu.

3.3.1 MASOMO KATIKA MCHEPUO WA SANAA
Mwanafunzi atasoma maadili,kiswahili,kiingereza,historia, jiografia na kompyuta na mazoezi ya viungo

3.3.2 MASOMO KATIKA MCHEPUO WA SAYANSI
Mwanafunzi atasoma maadili,hesabu,kompyuta, kemia, fizikia na baiolojia. Maabara za kisayansi zitatumika na mazoezi ya viungo

3.3.3 MASOMO KATIKA MCHEPUO WA VIWANDA
Atasoma maadili, kompyuta, hesabu za viwanda,sayansi ya viwanda na mazoezi ya viungo. Masomo yatalenga ufundi standi na viwanda vidogo

3.3.4 MASOMO KATIKA MCHEPUO WA KILIMO
Maadili, kiswahili, kompyuta, jiografia, sayansi kilimo na mazoezi ya viungo. Mashamba darasa,maabara zitatumika

3.3.5 MASOMO KATIKA MCHEPUO WA BIASHARA
Maadili, kiswahili, kompyuta,hesabu za biashara, sayansi biashara na mazoezi ya viungo. Atajifunza mbinu za biashara na miradi midogo midogo

3.3.6 MASOMO KATIKA MCHEPUO WA SAYANSI KIMU
Yatawahusu zaidi wanawake, watasoma maadili, kiswahili, kompyuta, sayansi kimu na mazoezi ya viungo. Wanafunzi watajifunza kuhusu afya ya familia, kutunza nyumba,watoto na familia, kilimo bustani, ujasiriamali, kupika, kusuka nywele na maisha ya kijamii

3.4 MASOMO KATIKA SHULE YA SEKONDARI KIDATO CHA NNE (MWAKA 16)
Mwaka huu wa mwisho wa masomo ya sekondari,utatumika kivitendo katika ofisi, kiwanda, shambani, nk. Ataandika nadharia katika ripoti yake na vitendo vitakavyoshuhudiwa na msimamizi wake na mwalimu wake.Katika hatua hii hata kama hataendelea na elimu ya juu atakuwa kijana bora katika jamii anayeweza kujitegemea na kujiajiri

4.0 HITIMISHO

4.1 FAIDA ZA MFUMO MPYA WA MASOMO TUNAOPENDEKEZA

4.1.1 KUKUZA NA KULEA MAADILI KATIKA JAMII:
Kupitia somo la maadili lililopo kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu kama tulivyoonesha

4.1.2 KUJENGA JAMII MAIKINI YENYE UKAKAMAVU: Kupitia somo la michezo na mazoezi ya viungo(physical education) ambalo lipo hatua zote

4.1.3 KUOKOA MUDA WA KUSOMA:Tumeokoa miaka mitano ambayo mwanafunzi anaipoteza kwa ajili ya kusoma katika mfumo wa sasa

4.1.4 KUJENGA WELEDI NA UWEZO WA KUJIAJIRI KWA VIJANA: Elimu itakuwa ya vitendo na halisia, kama anasoma kilimo aweze kulima, msomi wa biashara aweze kufanya biashara, nk. Kiswahili ndiyo itakuwa lugha pekee ya kufundishia
 
Serikali ichukue maoni kama haya
 
Mkuu,umeandika kisomi mno
 
Asante sana mkuu
Inafuraisha ukikuta watu wanawaza/wanatamani kuona mabadiliko katika sehemu/jambo lilelile unaloliwazia

Elimu yetu ya sasa nikama tunaingizwa kifungoni tunawekwa kwenye mfumo wa kutawaliwa elimu ina nafasi ndogo sana yakutusaidia sisi wasomi tuweze kujitegemea
Nimependa mawazo/mapendekezo yako
Tuishi tukiwaza na kutamani na kuyatafuta mabadiliko ili tuendelee kuwepo
 
Hii ndiyo Tz, maandiko mengi lakini mwandishi akipewa nafasi asimamie utekelezaji, atapotelea hewani.

Waliandika akina Makweta, prof Ndalichako, prof Mkenda nk.

Walipopewa nafasi kutekeleza mawazo yao, wote wamepoteza mwelekeo.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Tatizo ni serikali kukubali kuyafanya hayo mabadiliko
 
Back
Top Bottom