CAG Ripoti 22/23: TEMESA inailipa Kampuni ya AZAM Tsh. Milioni 5 kila siku kuendesha Vivuko

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,441
8,261
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amependekeza TEMESA itathmini mikakati mbadala ya kupunguza utegemezi wa vivuko vya mwendokasi kwakuwa kuendelea kukodisha vivuko hivyo kutoka Kampuni ya Azam Marine kunaathiri uendelevu wa huduma ambapo TEMESA inailipa Azam ada ya huduma kila siku Tsh. milioni 5 pamoja na kodi ya zuio ya 5%.

Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema “June 14, 2022, Wakala wa Huduma za Umeme Tanzania (TEMESA) uliingia mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya AZAM Marine Ltd ya kukodi na kuendesha vivuko viwili vya baharini ‘Sea Taxi 1’, na ‘Sea Taxi 2’ kati ya Magogoni na Kigamboni, mpango huu ulilenga kuongeza uwezo wa TEMESA kuhudumia Wateja kufuatia ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Magogoni”

“Kila kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 250 kwa kila safari, kwa mujibu wa Kifungu Na. 5 cha Mkataba wa Makubaliano, mkodishwaji (TEMESA ), analazimika kuilipa Kampuni ya AZAM Marine Ltd ada ya huduma kila siku ya Sh. milioni 5 (pamoja na kodi ya ongezeko la thamani) pamoja na kodi ya zuio ya 5%, Mkodishaji, Kampuni ya AZAM Marine itatoa ankara ya malipo kila mwezi inayoeleza idadi ya siku ambazo huduma ilitolewa kwa mkodishwaji katika mwezi husika”

“Nilibaini kuwa kuanzia July 1, 2022 hadi June 30, 2023, TEMESA ilikusanya jumla ya Sh. bilioni 5.76 za tozo za vivuko katika Kituo cha Magogoni - Kigamboni, kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 1.83 (sawa na 31% ya makusanyo yote) zililipwa kwa Kampuni ya AZAM kwa ajili ya uendeshaji wa vivuko viwili”

“TEMESA ilibakiwa na Sh. bilioni 3.93 (69%) ili kulipia gharama za undeshaji kama vile mafuta ya vivuko, gharama za kazi, ukarabati na matengenezo, na gharama zinginezo, hata hivyo, kiasi kilichobaki cha Sh. bilioni 3.93 kilikuwa hakitoshi kulipa gharama hizo, hivyo kusababisha Wakala wa Huduma za Umeme Tanzania kutumia fedha za vyanzo vingine kugharamia undeshaji wa kituo cha Magogoni - Kigamboni, hali hii inasabisha Wakala kuendelea kutegemea ruzuku ya serikali kugharamia shughuli zake badala ya kujitegemea, napendekeza TEMESA iongeze idadi ya vivuko ili kukabiliana na ongezeko la Wateja.

Pia soma:

Ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2022/23

CAG Kichere: Licha ya kupewa Ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22
 
Wataalamu wa idara hii wanatakiwa wakae watafute suluhisho sio kuongea tu Kila siku na hakuna hatua inayochukuliwa
 
1713191279227.png

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amependekeza TEMESA itathmini mikakati mbadala ya kupunguza utegemezi wa vivuko vya mwendokasi kwakuwa kuendelea kukodisha vivuko hivyo kutoka Kampuni ya Azam Marine kunaathiri uendelevu wa huduma ambapo TEMESA inailipa Azam ada ya huduma kila siku Tsh. milioni 5 pamoja na kodi ya zuio ya 5%.

Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema “June 14, 2022, Wakala wa Huduma za Umeme Tanzania (TEMESA) uliingia mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya AZAM Marine Ltd ya kukodi na kuendesha vivuko viwili vya baharini ‘Sea Taxi 1’, na ‘Sea Taxi 2’ kati ya Magogoni na Kigamboni, mpango huu ulilenga kuongeza uwezo wa TEMESA kuhudumia Wateja kufuatia ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Magogoni”

“Kila kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 250 kwa kila safari, kwa mujibu wa Kifungu Na. 5 cha Mkataba wa Makubaliano, mkodishwaji (TEMESA ), analazimika kuilipa Kampuni ya AZAM Marine Ltd ada ya huduma kila siku ya Sh. milioni 5 (pamoja na kodi ya ongezeko la thamani) pamoja na kodi ya zuio ya 5%, Mkodishaji, Kampuni ya AZAM Marine itatoa ankara ya malipo kila mwezi inayoeleza idadi ya siku ambazo huduma ilitolewa kwa mkodishwaji katika mwezi husika”

“Nilibaini kuwa kuanzia July 1, 2022 hadi June 30, 2023, TEMESA ilikusanya jumla ya Sh. bilioni 5.76 za tozo za vivuko katika Kituo cha Magogoni - Kigamboni, kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 1.83 (sawa na 31% ya makusanyo yote) zililipwa kwa Kampuni ya AZAM kwa ajili ya uendeshaji wa vivuko viwili”

“TEMESA ilibakiwa na Sh. bilioni 3.93 (69%) ili kulipia gharama za undeshaji kama vile mafuta ya vivuko, gharama za kazi, ukarabati na matengenezo, na gharama zinginezo, hata hivyo, kiasi kilichobaki cha Sh. bilioni 3.93 kilikuwa hakitoshi kulipa gharama hizo, hivyo kusababisha Wakala wa Huduma za Umeme Tanzania kutumia fedha za vyanzo vingine kugharamia undeshaji wa kituo cha Magogoni - Kigamboni, hali hii inasabisha Wakala kuendelea kutegemea ruzuku ya serikali kugharamia shughuli zake badala ya kujitegemea, napendekeza TEMESA iongeze idadi ya vivuko ili kukabiliana na ongezeko la Wateja”
 
Hilo huwezi lisikia mama akilisema kuwa watu wanakwepa Kodi, ama wanakula Kodi , ama wanahujumu uchumi wa nchi Ila mwananchi akikwepa kadogo hata ka alfu kumi tu ndiko kanakoongelewa.
January akajilipa bilioni moja kuiandika strategic plan sijui ya Nini na akampatia mtu binafsi.
Hakuna asiyetaka kulipa Kodi Ila zinatumiwaje.
Kuna shule kibao hata mwanza mjini watoto wanakaa chini kabisa na hawana madawati.
Shuleni umeacha saivi walimu wanawachangisha wanafunzi hela eti.
Sijui ndio watafaulu
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amependekeza TEMESA itathmini mikakati mbadala ya kupunguza utegemezi wa vivuko vya mwendokasi kwakuwa kuendelea kukodisha vivuko hivyo kutoka Kampuni ya Azam Marine kunaathiri uendelevu wa huduma ambapo TEMESA inailipa Azam ada ya huduma kila siku Tsh. milioni 5 pamoja na kodi ya zuio ya 5%.

Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema “June 14, 2022, Wakala wa Huduma za Umeme Tanzania (TEMESA) uliingia mkataba wa makubaliano (MoU) na Kampuni ya AZAM Marine Ltd ya kukodi na kuendesha vivuko viwili vya baharini ‘Sea Taxi 1’, na ‘Sea Taxi 2’ kati ya Magogoni na Kigamboni, mpango huu ulilenga kuongeza uwezo wa TEMESA kuhudumia Wateja kufuatia ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Magogoni”

“Kila kivuko kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 250 kwa kila safari, kwa mujibu wa Kifungu Na. 5 cha Mkataba wa Makubaliano, mkodishwaji (TEMESA ), analazimika kuilipa Kampuni ya AZAM Marine Ltd ada ya huduma kila siku ya Sh. milioni 5 (pamoja na kodi ya ongezeko la thamani) pamoja na kodi ya zuio ya 5%, Mkodishaji, Kampuni ya AZAM Marine itatoa ankara ya malipo kila mwezi inayoeleza idadi ya siku ambazo huduma ilitolewa kwa mkodishwaji katika mwezi husika”

“Nilibaini kuwa kuanzia July 1, 2022 hadi June 30, 2023, TEMESA ilikusanya jumla ya Sh. bilioni 5.76 za tozo za vivuko katika Kituo cha Magogoni - Kigamboni, kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 1.83 (sawa na 31% ya makusanyo yote) zililipwa kwa Kampuni ya AZAM kwa ajili ya uendeshaji wa vivuko viwili”

“TEMESA ilibakiwa na Sh. bilioni 3.93 (69%) ili kulipia gharama za undeshaji kama vile mafuta ya vivuko, gharama za kazi, ukarabati na matengenezo, na gharama zinginezo, hata hivyo, kiasi kilichobaki cha Sh. bilioni 3.93 kilikuwa hakitoshi kulipa gharama hizo, hivyo kusababisha Wakala wa Huduma za Umeme Tanzania kutumia fedha za vyanzo vingine kugharamia undeshaji wa kituo cha Magogoni - Kigamboni, hali hii inasabisha Wakala kuendelea kutegemea ruzuku ya serikali kugharamia shughuli zake badala ya kujitegemea, napendekeza TEMESA iongeze idadi ya vivuko ili kukabiliana na ongezeko la Wateja”
CCM mbele kwa mbele.
 
Hapo angeachiwa Azam afanye hiyo biashara, angekuwa analipa kodi na concession kwa kila abiria anaebeba.
Sahihi wanachofabya Temesa ni uhuni.Wamwachie aendeshe wao wafunge virago wafanyakazi wote wa hapo wanafanya nini sasa? Wamwachie tu serikali ikusanye kodi basi
 
Back
Top Bottom