Bashe: Rais Samia ametupa Idhini kuyarejesha Serikalini Mashamba ya MO Dewji ikithibitika hana Nia ya kuyaendeleza kwa mujibu wa Mkataba!

Aisee huyu jamaa anahodhi Ardhi kubwa sana bila matumizi yeyote ya maana.

Ni mapori na mapori na mapori.

Hii haikubaliki mtu mmoja kujimilikisha Ardhi kubwa namna ile.
 
Waziri wa Kilimo mh Bashe ameliambia Bunge timu ya wizara yake itamwita Mwekezaji MO Dewji Ili kujua matazamio yake kwenye mashamba aliyouziwa na Serikali kwa Masharti maalumu huko Korogwe Tanga na Rungwe Mbeya

Bashe amesema Rais Samia ameshatoa Idhini kwa wizara yake kuyarejesha serikalini Mashamba hayo endapo MO Dewji hana Nia ya kuyaendeleza kama ilivyokuwa kwenye makubaliano ya Mauzo

Source: Mwanahalisi Digital
Hii ingetokea enzi za Magufuli, nchi nzima ingejaa makelele
 
Back
Top Bottom