#COVID19 Askofu Gwajima Kaathiriwa na Filamu za Hollywood "Fiction movies" Pamoja na Mambo dhahania

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,552
52,226
GWAJIMA AMEATHIRIWA NA FILAMU ZA HOLLYWOOD "FICTION MOVIES" PAMOJA NA MAMBO DHAHANIA.

Na, Robert Heriel.

Gwajima anaonekana ni muumini mkubwa wa filamu za kimarekani "Hollywood", hasa zile fiction movies, adventure movies na Horror movies.
Ukimsikiliza Kwa umakini mkubwa Ndugu Gwajima utakuungana na Mimi kuwa, tayari anaathari mbaya ya Filamu hizo.
Mbali na athari za Filamu za Hollywood lakini pia AMEATHIRIWA na mambo DHAHANIA, mambo ya kusadikika, mambo ya kufikirika ambayo kimsingi hayawezekaniki.

Sio ajabu Gwajima, ukimsikia akijitapa kuwa yeye ananguvu mpaka za kufufua wafu, kurejesha misukule. Mtu yeyote wa namna hiyo AMEATHIRIWA kisaikolojia na Kiroho.

Ukikaa na watu Kama kina Gwajima sio ajabu kwenye Stori zao ukiwasikia wakisema wanaouwezo wa kupaa angani Kama Spiderman au Batman, wenyewe watakuambia wanaouwezo wa kuruka juu kupitia nguvu za Yule wamwitaye Yesu.

Gwajima Hana tofauti kubwa na wala unga "madawa ya kulevya", ambao mawazo Yao mengi ni Kama wapo ndotoni, sio ajabu wakajiona wapo Marekani ilhali kiuhalisia wapo Buza Kwa mpalange huko.

Gwajima na watu wote wa dizaini yake, sio ajabu akakupa kikombe cha chai ya Kahawa alafu akakuambia ukinywa utapona UKIMWI, au gonjwa lolote kubwa.

Kumuamini Gwajima au watu dizaini yake itakupasa uwe na akili na mtazamo Kama wake, aidha uwe imeathiriwa na Filamu za Hollywood au unapenda mambo dhahania ambayo ni fiksi tuu.

Gwajima ni Aina ya watu Kama kinjektile Ngwale, Mzee wa maji maji. Yaani Wazee wa fiksi fiksi tuu. Gwajima ni Aina Ile Ile ya watu Kama kina Kibwetere.

Kumsikiliza Gwajima labda iwe Kwa kujifurahisha, kujiburudisha, au Comedy tuu.

Ingawaje kuna wakati anaweza kuongea mambo ya msingi lakini mara nyingi akiongea mambo asiyo na utaalamu nayo hujikuta akipata athari za Filamu za Hollywood na mambo ya dhahania.

Juzi nilimsikiliza nikacheka Sana, yaani Gwajima anatafuta istilahi ya kitaalamu ngumu ngumu ambayo waumini wake hawaijui kisha huilezea kuipa nguvu hoja zake.

Jambo moja la hakika na ambalo Gwajima anaweza kujivunia ni uwezo wa kujieleza na kushawishi watu hasa WAVIVU WA KUFIKIRI,
Watu dizaini ya Gwajima wengi wao wamejaliwa Ushawishi na uwezo mkubwa wa kujieleza. Kwenye biashara Kama za Mtandaoni Kama Qnet,Aim Global, Rifaro na biashara za namna hiyo watu Kama Gwajima ni wamoto, yaani wakija kukushawishi ujue umekwisha.

Watu Kama Gwajima wanaposhikilia msimamo hasa kwenye ishu wasizo na utaalamu nazo, huwa na Agenda ZIFUATAZO

1. Kuvumisha jina lake.
Watu mashuhuri wa dizaini ya kina Gwajima, wakiona jina limepoa Kwa kitambo, hutafuta kitu cha kuinuka nacho.
Gwajima anajua baada ya kuwa opposite na Serikali na kuipinga basi lazima atakutwa na misuko suko ambayo itamuimarisha zaidi kuliko kumfifisha.
Gwajima hata akiwekwa ndani Leo hii, kwake ni faida. Maana lengo lake litakuwa limetimia.

2. Kurejesha Imani ya waumini wake.
Mbali na Gwajima kujitetea baada ya video ya ngono iliyovuja yenye Sura yake lakini bado waumini wengi Imani zao zilishuka. Baadhi yao waliacha hata kwenda kanisani kwake.
Hivyo Kitendo cha Gwajima kushikilia msimamo wake kuhusu Chanjo ya Corona kutarejesha Imani ya waliorudi nyuma na ikiwezekana kupata waumini wapya.

Zingatia, Watanzania wengi wameathiriwa na mambo dhahania zaidi kuliko halisia. Watu Kama Gwajima hupendwa zaidi kwenye jamii Kama ya kitanzania.

3. Kuitikisa SERIKALI.
Gwajima hakuwahi kwenda kinyume na serikali ya awamu ya tano licha ya kuwa na mapungufu mengi. Gwajima nilishawahi kumsikia wakati wa Kikwete akiishambulia serikali, lakini awamu ya tano hakuwahi kuthubutu kuleta vyokovyoko zake.

Kuingia Kwa Samia Suluhu, Gwajima kaanza tena kujifaraguza Kama mtu mwenye kusimamia ukweli(kile akionacho ni ukweli) Gwajima ningekuwa upande wake Kama angekuwa msema ukweli pasipo hofu wakati awamu ya tano, lakini ukimya wake kipindi kile na zaidi alikuwa akipongeza pekeake kunanipa mashaka.

Wapo Maaskofu Kama kina Mwingira, Kakobe, Mwamakula, Fredrick Shoo, na Yule wa Bukoba hawa walishajipambanua kuwa ni wasema ukweli ingawaje ukweli wao unaigusa tuu serikali ya CCM na mara nyingi hawakosoi Vyama pinzani. Hata hivyo nikitaka kuwatetea naweza sema kuwa, siku zote Mdogo anatetewa, na mkubwa ndiye anayelaumiwa.

Gwajima Hana tofauti na Wale wanaokupigia hesabu za kilimo cha Tikitiki wakati hawajawahi kulima tikiti, ni watu wa nadharia na mambo dhahania.

Gwajima hafai kwenye mambo Sirius kwani anaweza ingiza hadithi Kwa ishu halisi.

Gwajima ni Wale wanaokuambia hadithi za 666 sijui Freemason, vitu ambavyo Kwa lugha rahisi ni matokeo ya Utandawazi.

Vitu Kama Passport (Hati za kusafiria), Vitambulisho vya NIDA, Tin number, Kadi za Benk ni Teknolojia ya namna ya kupata Huduma tuu havina uhusiano wowote na mambo ya kiroho.
Hivyo sio ajabu miaka ijayo kadiri Teknolojia inavyokuwa hiyo 666 ikawa ni sehemu Teknolojia ya kumrahisishia kupata Huduma.

Kuliko kutembea na makarabrasha mengi kwenye mkoba, ni Bora upigwe chapa moja sehemu yoyote ya mwili kurahisisha upewaji wa Huduma mbalimbali.

Watu Kama kina Gwajima hupenda kutisha watu ili nafasi Yao nao iwepo.

Ndio maana wao kila kitu huweza kukitumia kutisha watu, sababu ni Ile ile, nayo ni ili nafasi Yao nayo ionekane, nao wazingatiwe.

Sio ajabu watu dizaini ya Gwajima, ukiwasikia wakizungumza ishu za kulogwa, sijui uchawi, sijui majini, yaani wao mambo Yao Kwa 90% huyachukulia kidhahania dhahania.

Wakati mambo dhahania kwenye maisha ya binadamu hayazidi hata Asilimia 10%.

Mwisho, Gwajima Hana makosa. Jamii bado ndiyo yenye makosa Kwa sababu IPO katika Giza la Ujinga.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro
 
Wakati anatapeli Watu kuwa ana uwezo wa kufufua Wafu serkali ilikaa kimya kwa kisingizio cha imani za Watu.

Sasa kanogewa kaamua kabisa kuingila kabisa kwenye maswala ya kitaifa.

Kuna mambo lazima serikali mgutuke kwa manufaa ya wengi sio kungoja Mtu afanye alivyofanya Kibwetere ndio mshtuke.
 
Sio Gwajima tuu, wahubiri wengi wa Kitanzania hawajui kutofautisha Hollywood fiction stories na vitu vyenye uhalisia. Saa nyingine unasikiliza mahubiri ya mtu anaongea utumbo tena kwa kujiamini, na watu watamuona kama anajua kweli kumbe anawapotisha tuu.
 
Ni chizi pekee anayeweza msikiliza na kuamini wasemacho dk Gwajima na dk Molleli ambao miezi kitatu tu waliuaminisha umma kwamba kuvaa barakoa na kupata chanjo ni hatari kwa maisha na ustawi wa watanzania.

Wakahamasisha watu wajifukize na kula maliamao na matango. Shubamiti!!!
 
Yaani watu 500 wanaema ndio
wanashindwa lakini mtu mmoja anasema hapana .... kuna rais
Kuna mawaziri
Kuna wakuu wa mikoa
Kuna wakurugenzi
Kuna manaibu wote
Askofu ngwajima yuko juuu
 
Sio Gwajima tuu, wahubiri wengi wa Kitanzania hawajui kutofautisha Hollywood fiction stories na vitu vyenye uhalisia. Saa nyingine unasikiliza mahubiri ya mtu anaongea utumbo tena kwa kujiamini, na watu watamuona kama anajua kweli kumbe anawapotisha tuu.
Sio wahubiri wa Kitanzania tu
 
Wakati anatapeli Watu kuwa ana uwezo wa kufufua Wafu serkali ilikaa kimya kwa kisingizio cha imani za Watu.

Sasa kanogewa kaamua kabisa kuingila kabisa kwenye maswala ya kitaifa.

Kuna mambo lazima serikali mgutuke kwa manufaa ya wengi sio kungoja Mtu afanye alivyofanya Kibwetere ndio mshtuke.

Huyu jamaa ananifurahishaga Sana
 
Wewe na wanasayansi wenzio hamjajibu maswali yake ya msingi. Jikiteni humo.

Hivi mtu utakaa ujibu ishu za Fiction movies kweli Mkuu??
Hivi mtu na akili zako ukae ujibu ishu za 666 kweli Mkuu?

Hizo ni hadithi Kama za Taikon tuu, hadithi za kubuni.

Sasa Kwa akili zako Mimi nikiandika fiction stori kuna haja ya kujibiwa??

Gwajima hawezi kujibiwa kisayansi Kwa maana Sayansi haijibu mambo ya DHAHANIA
 
Sio Gwajima tuu, wahubiri wengi wa Kitanzania hawajui kutofautisha Hollywood fiction stories na vitu vyenye uhalisia. Saa nyingine unasikiliza mahubiri ya mtu anaongea utumbo tena kwa kujiamini, na watu watamuona kama anajua kweli kumbe anawapotisha tuu.

Mara nyingi nawachukulia Kama wapiga Soga na visasili.
 
Ni chizi pekee anayeweza msikiliza na kuamini wasemacho dk Gwajima na dk Molleli ambao miezi kitatu tu waliuaminisha umma kwamba kuvaa barakoa na kupata chanjo ni hatari kwa maisha na ustawi wa watanzania.

Wakahamasisha watu wajifukize na kula maliamao na matango. Shubamiti!!!

Hao walikuwa wanalinda vitumbua vyao visiingie mchanga
 
Wakati anatapeli Watu kuwa ana uwezo wa kufufua Wafu serkali ilikaa kimya kwa kisingizio cha imani za Watu.

Sasa kanogewa kaamua kabisa kuingila kabisa kwenye maswala ya kitaifa.

Kuna mambo lazima serikali mgutuke kwa manufaa ya wengi sio kungoja Mtu afanye alivyofanya Kibwetere ndio mshtuke.
Hizi Imani bana unaweza kukuta wafuasi wa Kibwetere ukiwaambia habari ya wale wasabato masalia waliotaka kwenda Iraq bila passport wala nauli watawacheka. Wakati huo huo wasabato masalia wanawaona wafuasi wa Kibwetere walikuwa vilaza tu.
 
Hahaha!! Kwahiyo waweza kukuta wanaotaka chanjo nj mbumbumbu na wasioitaka chanjo ni mbumbumbu (huku wafuasi wa Kibwetere kule wasabato masalia).
 
Back
Top Bottom