Yusuph Manji: Hans Poppe alinipa wakati Mgumu sana enzi za uongozi wangu

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
51,989
23,500
“Unajua wakati nikiwa Yanga, mtu pekee aliyekuwa ananipa wakati mgumu ni Hans Poppe. Huyu jamaa alikuwa anafanya kazi yake kuonesha kabisa kuwa Dabi inatakiwa kuwa na mvuto, alikuwa akizungumza na watu wanamuelewa, alinipa wakati mgumu sana.

“Hata niliposikia amefariki, ukweli kibinadamu nilisikitika sana kwa kuwa alikuwa ni mtu muhimu kwenye soka, lakini nilijua kabisa kuwa Simba inakwenda kupata wakati mgumu na hiki ndiyo kinatokea leo, nafikiri mechi umeiona na msimamo unaonesha hali halisi ilipo Yanga na Simba kwa sasa,” alisema Manji ambaye alidumu kwenye timu ya Yanga kwa miaka 13 kama mfadhili na Mwenyekiti.

“Tulikuwa tunapambana sana uwanjani, lakini tulikuwa marafiki, alikuwa akizungumza lazima nijue amesema nini, huyu alikuwa ana nguvu kubwa sana kwenye soka la Tanzania na alikuwa anaweza kufanya jambo lolote na watu wakamuelewa.”

“Nafikiri unakumbuka wakati tulipoichapa Simba mabao matatu hadi mapumziko, baadaye wakaja kurudisha yote. Hapa Hans Poppe alihusika, siwezi kukuambia alifanyaje, lakini nguvu yake ilisababisha Simba wakapata sare kwenye huo mchezo, alikuwa na ushawishi wa hali ya juu sana kwa wachezaji.”

Yusuph Manji - Mfadhili na Mwenyekiti wa zamani Young Africans
 
BINAFSI NILIWAHII KUMWOGOPA SANA MPAKA IKAFIKA SIKU AMEKAA SEHEMU NKAJITAMBULISHA JIRANI YAKO HUKU.....

UNCLE M MSHABIKI WA YANGA ILAAA NAKUOGOPA NA KUKUHESHIMU SANAA KWANI MBINU GAN UNATYMIAGA KUPATA WACHEZAJI....


NKAANZA MTANIA NIYONZIMA...MORRISON...NK KHA AKACHEKA SANA AKASEMA SUBIRI DERBY IJAYO..TULICHOKUTANA NACHO TAIFA NAMWACHIA MUNGU NA N SIKU YA MWISHO KWENDA TAIFA MPAKA KESHO
CONT RIP LEGENDARY HANS HOPE
 
Hanspope ndio kafanya Babra aonekane Bora, kwenye usajili alikuwa hasubiri pesa za mo, alikuwa akitoa mfukoni na kuzikata pindi timu ikipata pesa.
Pamoja na kuifadhili Simba muda mrefu hakuwahi kufikiria kumiliki, Alikuwa kiongozi shabiki.
 
Back
Top Bottom