KWELI Watu 155 wafariki kwa Mafuriko Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Salaam,

Wakuu nimepata wenge baada ya kuona taarifa inaeleza watu 155 wamefafiki kwa Mafuriko Tanzania. Sijakutana na hii habari. Na hata Mtandao wa X (Twitter) wengine wanapata mashaka kama Mimi tu.

Screenshot_20240427-144900_1.jpg


Je, kuna ukweli kwenye jambo hili?

Tunaombeni ufafanuzi
 
Tunachokijua
Mnamo Januari 30, 2024 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ilitangaza kuwapo kwa mvua kali/ Mvua za El nino kuanzia mwezi Aprili mwaka huu (Soma hapa). Tangu kuingia kwa mwezi Aprili maeneo mbalimbali nchini yametawalia na mvua na mafuriko Soma hapa, hapa na hapa. Mafuriko hayo yanadaiwa kusababisha maafa mengi ikiwamo vifo, upotevu wa mali na makazi kwa watu soma soma hapa, hapa na hapa.

Tangu tarehe 25/04/2024 kumeibuka sintofahamu baada ya kusambaa taarifa inayoelezea watu 155 mpaka sasa wamefariki kutokana na mvua na mafuriko yanayoendelea maeneo mbalimbali nchini. Wadau wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakiona taarifa hii katika vyombo vya habari vya kimataifa na kupata mashaka kama taarifa hii ni ya kweli, na wanahoji chanzo cha taarifa hii.

Mathalani @Charllote100 Mtumiaji wa Mtandao wa X alihoji taarifa ya Aljazeera iliyoelezea vifo vya mafuriko na kupata mashaka juu ya taarifa hiyo. Mtumiaji huyo aliuliza

Al Jazeera hii habari wameipata wapi mbona sijaona news hapa Tz kwamba watu wote hawa wamefariki kwa hizi mvua?
1714224678165-png.2975351

Je, Taarifa ya kuwa watu 155 wamefariki kwa Mafuriko na mvua zinazoendelea imetoka wapi?
JamiiCheck imefuatilia chanzo cha taarifa hii na kuthibitisha kuwa taarifa hii ni ya kweli na ilitolewa na serikali 25/04/2024 kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa Bungeni. Waziri Mkuu Majaliwa alitoa taarifa ya kuhusu mwendendo wa Matuko ya hali ya hewa, athari zake na hatua zilizochukuliwa na Serikali Soma hapa.

Kuhusu kuwepo vifo 155 kutokana na mafuriko Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema:

Mvua kubwa za El nino zinazoendelea zikiambatana na upepo mkali, mafuriko na maporomoko ya udongo maeneo mbalimbali nchini zimesababisha athari kubwa ikiwemo vifo, uharinifu wa makazi na mazao mali za wananchi, miundombinu na kutokana na athari hizo zaidi ya kaya 51,000 za watu 200,000 waliathirika ambapo Watu 155 walipoteza maisha, 236 walijeruhiwa na nyumba zaidi ya 10,000 ziliathiriwa kwa kiwango tofauti.

Hivyo, kutokana na pitio hilo JamiiCheck inawatoa mashaka Wadau wote waliodhani Vyombo vya Habari vya Kimataifa vimepika data na kutunga taarifa hiyo kuwa, taarifa hii haijatungwa na imetolewa na Serikali kama ilivyoonekana hapo juu.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom