Watakatishaji fedha wanaotoa mikopo mitandaoni wanalindwa na nani? Wanapata wapi pesa za kukopesha watu wasiowafahamu?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
943
4,458
Tanzania kuna mtandao mkubwa umeibuka wa utakatishaji fedha unaoongozwa na wanasiasa na viongozi wa umma wanaokwapua fedha za walipa kodi zisizo haki yao.

Kutokana na watu hawa kupata fedha wasizo na uchungu nazo wametengeneza application zakutoa fedha online kama mikopo. Masharti yao hayaendani kabisa na masharti ya mikopo Duniani.

Lakini pia mikopo hii haina kulipa kodi wala hakuna ufuatiliaji unaoendelea nchni. Katika hali isiyo ya kawaida wameweza kushirikiana na watendaji wasio na maadili kwenye mitandao ya simu na kufanikiwa kupata mawasiliano ya watu mbalimbali ambapo kupitia mawasiliano hayo wanatumia namba za watu kufanya maombi ya mikopo na kisha meseji za madai kutumwa kwa wenye namba.

Moja ya kijana mmoja anayefanya kazi na mwanasiasa mmoja katika biashara hii amefanikiwa akiwa mwajiriwa wa watoa mikopo hii kukopa zaidi ya milioni tano kwa line za simu mbali mbali na baada ya kupata fedha hizo ameendelea kushawishi watu waruhusu line zao zitumike kukopa na wanapata mgawo .

Nilipofiatilia nimebaini wamiliki wa application hizi wanafahamika na vyombo vyetu na waajiriwa wanafahamika ila wanapofuatiliwa maelekezo utoka kwamba waachwe waendelee na utakatishaji fedha huu.

Nchi yetu Tanzania naomba kufahamu
1. Chanzo cha hizi fedha ni nini?
2. Wamiliki wa application hizi ni wakina nani?
3. Usajili wa hizi application unafanywa na nani?
4. Makampuni ya simu yana haki yakutoa taarifa za wateja wao kwa wahalifu hawa?
5. Je fedha hizi zinazosafishwa zinawezaje kuathiri walipa kodi kama mabenki na taasisi nyingine za mikopo zilizosajiliwa?
6. Fedha hizi haziwezi zikatumika kufadhili uhalifu kama CDF alivyosema wakimbizi wamejaa nchini?
7. Gavana wa BOT, mdodoro wa uchumi na kukosekana kwa dola hakuwezi kuwa sehemu ya wenye dola kununua madafu na kusafisha kupitia mikopo umiza?
 
Pesa zinazotangazwa na mkaguzi wa mahesabu kila Mwaka, zabuni hewa na manunuzi bila ya usimamizi ni baadhi ya vyanzo vyao
 
Back
Top Bottom