SoC04 Vitu hivi vitasaidia kuifikia Tanzania Tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

MsigwaRolenzo1

New Member
Apr 19, 2024
1
0
TANZANIA TUITAKAYO

Tanzania ni nchi inayopatikana barani afrika katika ukanda wa afrika mashariki, ni nchi iliyojariwa vyanzo mbalimbali vya kuvutia kama madini , mbuga za wanyama mbalimbali, milima, mito na reli za kisasa
Vitu ambavyo watanzania wengi wanapenda kuiona Tanzania ikipiga hatua kubwa sana kimaendeleo vitu hivi vitasaidia kuifikisha TANZANIA TUITAKAYO endapo serikali ikatilia mkazo tutaiona Tanzania ni nchi ya kipekee sana na itakayopiga hatua kwa wakati mfupi.

UTALII hii ni njia ya kipekee tunayoweza kuitumia kuitangaza nchi kiutalii na kutuletea maendeleo na ushindani katika nyanja ya utalii hapa duniani endapo tukaongeza njia zitakazo wavutia watalii waweze kutembelea vivutio vyetu njia hizo ni kama ifuatavyo kubrand mbuga zetu katika masharika ya ndege na mabango haya yaliyokuwepo barabarani asa Yale maeneo ya airport na madaraja ya kuvutia kama daraja la tanzanite, daraja la kijazi na madaraja mengine mengi endapo tukaweka picha za kuvutia za vitu adimu vinavyopatikana hapa Tanzania pekee basi tutaliweza kuliteka soko na mapato yakaongezekana.

Kwasasa naona serikali unafeli kuwaleta wasanii kutoka India hii njia wanayotumia si sahihi na ni ya mda mfupi na ukiangalia pesa zinapotea nashauri serikali ibadilike tuwe na mfumo wa kisasa zaidi kubrand mbuga zetu kwenye haya mabango ya barabarani na hata kwenye matangazo ya YouTube tuwe tunatangazo huko ili tuwavutie watalii waweze kuongezeka zaidi.

MADINI katika nchi yetu tanzania tumejaliwa kuwa na madini ya aina mbalimbali kama dhahabu, almasi, makaa ya mawe na tanzanite. Ni fahari sana Tanzania kubarikiwa madini ya kipekee yaitwayo tanzanite sababu haya ni madini yanayooatikana Tanzania tu na hakuna popote duniani yanapochimbwa zaidi ya Tanzania pekee , hivyo basi serikali inatakiwa kusimamia haya madini kuanzia yanapochimbwa na kuyauza na yasiishie kuuzwa tu Bali ibuni kwa kuyachonga yawe kama makombe yanashondiniwa kwenye michezo kwa kufanya hivi basi tutaweza itangaza Tanzania na kuyapandisha thamani.

ELIMU katika elimu naona Tanzania tupo nyuma sana ni vyema tukawa tunaanda watoto wakiwa bado shule za awali tuwatengeneze na kuwasomesha shule maalumu kuna haja kubadili mtaala na sio kutumia huu mtaala kulilishana madarasani , sasa mfano mzuri mtoto mwenye ndoto ya kuja kuwa mwanasayansi itakua vyema tu kaweka mitaala ya sayansi iwe maalumu kusoma na kuwakuza kimalezi kuliko kumjaza kichwani masomo yasiyo na umuhimu kwake tukifanya hivi tutapunguza mzigo . mfano wa pili mtoto mwenye ndoto kuwa mchezaji mpira aandaliwe tangu udogoni kwake na kupewa masomo maalumu hii itasaidia sana kukuza vipaji mfano mzuri angalia nchi zilizoebdelea kama China, ulaya, ufaransa, Korea nk

KUKOMESHA RUSHWA hii ni njia itakayotufikisha mbali endapo tukalitilia mkazo itakua vyema tukawachukulia hatua wale viongozi wanaotajwa na CAG kuchukuliwa hatua Kali kama tunavyo chukuliwa sisi wananchi wa kawaida bila kusahau adhabu ya viboko iwepo tuige mfano China wakati inaanza kujijenga kiuchumi, tunatambua hakuna alie juu ya sheria sasa kwanini viongozi wazembe wanaopoteza zaidi ya mabilioni na kuitia hasara serikali hawachukuliwi hatua Bali yule mwananchi anaekwepa kodi ya elfu moja basi anachukuliwa hatua kali sana utadhani kasababisha hasara ya mabilioni , haki tunaomba iwepo iwe sawa kwa wote , rushwa ni adui wa maendeleo tupambane kwa pamoja kutokomeza rushwa tuwe na maendeleo.
 
serikali inatakiwa kusimamia haya madini kuanzia yanapochimbwa na kuyauza na yasiishie kuuzwa tu Bali ibuni kwa kuyachonga yawe kama makombe yanashondiniwa
Nzuri: kwamba tusiishie tu kuwa wachimbaji wa malighafi. Bora tuyachakate pia na bidhaa zake tuzipate.

Inashangaza leo nikihitaji pete ya plastiki na steel niitafute nje hadi ya dhahabu nayo nzuri zitoke nje tu🤗
Tufike hatua wamasai, wasukuma na makabila mengine yale mapambo wanayovaa yawe ni madini mtupu. Tumejitahidi shaba, bado fedha na dhahabu na matanzanite kila kitu.

kuja kuwa mwanasayansi itakua vyema tu kaweka mitaala ya sayansi iwe maalumu kusoma na kuwakuza kimalezi kuliko kumjaza kichwani masomo yasiyo na umuhimu kwake tukifanya hivi tutapunguza mzigo
Hili wazo linajitokeza sqna panapoongelewa elimu lakini nnaomba kukuuliza chief: Je tukisema kuwa kuwepo kwa masomo mengi kunampa mwanafunzi uwanda mpana zaidi wa kuielewa dunia na kuitawala utatoa maoni yepi?
haki tunaomba iwepo iwe sawa kwa wote , rushwa ni adui wa maendeleo tupambane kwa pamoja kutokomeza rushwa tuwe na maendeleo.
Hakika, HAKI huinua taifa.
 
Back
Top Bottom