SoC03 Utawala wa Sheria unachochea Utawala Bora

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Mahitaji ya utawala-wa-sheria hayana maandishi kama vile meupe/meusi lakini ni suala-la-kiasi. Hakuna viwango visivyobadilika vinvyoashiria ikiwa mahitaji hayo yamefikiwa/hayakufikiwa. Kwamfano, ni rahisi kusema kuwa sheria lazima ziwe wazi kwa wale wanaokusudiwa sheria hizo. Hata hivyo, kuwa wazi kabisa ni kitu kisichoweza kufikiwa. Kuna kitu kimoja.

Busara huwa maneno yote yanaweza kuwa na maana-tofauti katika baadhi ya mambo,mfano, ikiwa sheria-ya-mtaani inasema kuwa vyombo-vya-usafiri haviruhusiwi katika bustani, ni wazi kuwa bajaji au pikipiki haviruhusiwi.

Lakini vipi kuhusu toroli Maneno yote yana maana moja ya msingi ambayo haipingiki, lakini siku zote kuna mwanya wa kutokuwa na uhakika wa maana ya neno.

Ingawa maneno-ya-sheria lazima yakaribiane na maneno-ya-lugha ya kawaida kwa kadri inavyowezekana, kiasi fulani cha utaalamu lazima kiwemo kwa ajili ya uwazi-wa-sheria. Pia, mifumo-mingi-ya-sheria ina-maana nyingi kwa sababu za msingi-yanaingizwa kwa makusudi maneno katika sheria ambayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna mbalimbali; vipengele vya haki-za-binadamu kikatiba na mikataba-ya-kimataifa ni mifano iliyo wazi. Kadhalika na vipengele kuhusiana na usawa/kiasi katika makosa/kanuni-za-sheria-za-mkataba.

Uwazi kuwa athari-za-mambo haya na mambo-mengine kuhusu uwazi-wa-sheria zisiongezwe kupita kiasi. Maranyingi, inawezekana kuhakikisha kuwa raia na watumishi-wa-serikali wanaelewa kuhusu wajibu-wao muhimu na haki-zao.

Muhimu ni kwa kiwango gani mifumo-ya-sheria inaendana na utawala-wa-sheria hilo ni sual- la-kiasi – hivyo linajadilika. Mfumo-Muhimu, tahadhari nyingine ni mahitaji yaliyotajwa hapo-juu yana hulka ya misingi-ya-jumla. Ili iweze kufanyakazi lazima ichambuliwe na kanuni-zilizo-wazi na taratibu-za-kisheria.

Katika mchakato-huu, lazima yafanywe machaguo mengi. Kwamfano, katika baadhi ya mifumo-ya-sheria watu-wasiokuwa-na-utaalamu hawashiriki katika kutoa hukumu-za-kesi-za-jinai na madai, wakati mifumo mingine ya sheria hutumiwa watu wasiokuwa na utaalamu kwa madhumuni hayo.

Hatahivyo, kwa namna mbili zote hizo utoaji-wa-hukumu unachukuliwa kuridhisha mahitaji-ya-usuluhishi-wa-migogoro ulio-huru na usiopendelea upande-wowote na mahitaji-ya-usikilizwaji-wa-kesi ulio-wa-haki. Mifumo mingi ya sheria imeipa mahakama madaraka ya kuangalia kama sheria zilizotungwa na Bunge zinalingana na katiba, wakati mifumo-mingine-ya-sheria haina utaratibu kama huo wa kuhuisha katiba.

Hatahivyo, chini ya mifumo hiyo yote miwili unaweza kuwepo udhibiti wa kutosha ili kuhakikisha kuwa sheria zinazotungwa na Bunge zinalingana na katiba. Katika baadhi ya mifumo-ya-sheria, waendesha-mashtaka wana wajibu wa kuendesha mashtaka ya uhalifu au kosa lolote linaloletwa mbele yao, wakati katika mifumo mingine ya sheria waendesha-mashtaka wana kiasi fulani cha kutumia hiari yao kuhusiana na hilo. Hatahivyo, kwa mifumo hiyo yote miwili utekelezaji wa sheria-ya-jinai unaweza kuwa ni wa kutosha na wenye kutabirika. Hakuna Suluhisho la Namna Moja Tu Kwa ufupi, hakuna jibu moja tu lililo sahihi kwa swali, ni kwa namna gani mahitaji ya utawala-wa-sheria yanaweza kutekelezwa. Kinyume chake, kwa kawaida kuna njia nyingi za kulifanya hilo.

Mifumo-ya-sheria inayotofautiana sana juu ya yale halisi yaliyomo katika kanuni na asasi inaweza kutosheleza mahitaji ya utawala-wa-sheria kwa kiasi kilicho sawa. Kwahiyo, hakuna mfumo wa sheria unaoweza kuwa ndiyo mfumo-wa-dunia unaokubalika wa utawala-wa-sheria.

Hakuna suluhisho la namna moja kwa tatizo la tafsiri ya mahitaji ya jumla ya utawala-wa-sheria katika kanuni-mahasusi-za-kisheria. Hii ina maana pia kuwa hakuna mwanasiasa anayeruhusiwa kudhani kuwa mtindo wake wa kitaifa ndio mtindo pekee ulio sawa kwa utawala-wa-sheria. Hili ni muhimu katika uwanja wa ushirikiano wa kisheria na nchi nyingine, hasa kama madhumuni ya ushirikiano huo ni kujenga au kuimarisha utawala-wa-sheria katika nchi hizo.

Uelewa juu ya Mambo kuhusiana na Hali Ilivyo, Vilevile mtu hatakiwi awe na imani kuwa mambo hutegemea hali ilivyo. Baadhi ya kanuni na taratibu za sheria hukiuka mahitaji-ya msingi ya utawala-wa-sheria. Ikiwa majaji wanateuliwa moja-kwa-moja na serikali bila ya kinga yoyote na kama serikali inaweza kuwafukuza majaji kama inavyopenda, hapo utawala-wa-sheria hauheshimiwi .

Ikiwa watu wanaweza kukamatwa na kuwekwa magerezani kwa masiku mengi bila ya kufikishwa mbele ya jaji, hapo utawala-wa-sheria unakiukwa. Ikiwa vitendo vya serikali vinavyohusiana na matumizi ya madaraka kuhusiana na raia havimo katika yale yanayochambuliwa na kupitiwa kisheria, hapo utawala-wa-sheria unakiukwa.

NINI KIFANYIKE?
Kujizuia katika Matumizi ya Madaraka , serikali ina madaraka makubwa kwa raia wake katika:-. kuwaadhibu au kuwachukulia hatua hasi, kutoza ushuru, kutoa msaada-wa-kifedha, kadhalika. Madaraka-ya-serikali yana athari kubwa kwa Maisha-ya-raia. Ikiwa watumishi-wa-serikali wanawajibika kutenda mambo kwa kufuata na kwa mujibu wa sheria, matumizi-ya-madaraka yanakuwa ndani ya mipaka-ya-sheria.

Utawala-wa-sheria unakataza matumizi-ya-hiari ya mtu na kuzuia matumizi-mabaya-ya-madaraka, kwa maneno mengine matumizi ya madaraka kwa misingi ya mtu kufanya atakavyo, kufanya mambo kiholela, chuki, kufanya mambo kwa kukurupuka na upendeleo.

Hii ndiyo sababu kubwa kwa nini utawala-wa-sheria ni lazima. Ni wazi kuwa raia hunufaika pale madaraka yanapokuwa hayatumiwi kiholela. Lakini hili ni muhimu kwa sababu nyingine vilevile. Kwamfano, wawekezaji kutoka nje hawavutiwi katika nchi ikiwa kila muamala wa kiserikali lazima uambatane na hongo au ikiwa ulinzi wa rasilimali hutegemea matakwa ya watumishi wa serikali.

Nchi inayotaka kuvutia rasilimali hufanikiwa zaidi ikiwa inaweza kutoa uhakika kuwa miamala-ya-kiuchumi hufanyika katika mfumo-wa-chombo kinachoendeshwa kwa sheria zilizowazi na za kuaminika, njia za kusawazisha mambo kisheria zipo, maamuzi ni ya kuaminika na kuwa wenye mamlaka wanatenda kwa mujibu-wa-sheria. Kuyaweka matumizi ya madaraka chini ya sheria ni jambo zuri kwa vyote, biashara na kwa haki za wafanyakazi.

MAZINGATIO
• MISINGI YA KATIBA INAPASWA IFUATWE
• UTANGAZAJI, UWAZI, KUTOTAZAMA NYUMA NA UTULIVU NI VYA MSINGI KATIKA UTAWALA WA SHERIA
• KUWEKWA MIPAKA YA MATUMIZI YA HIARI
• MAZINGATIO YA MGAWANYO WA MADARAKA KATIKA MIHIMILI MITATU YA NCHI
• WALE WALIO KATIKA MAHAKAMA LAZIMA WAWE HURU KUTOKANA NA SHINIKIZO KUTOKA NJE

Nguzo-Tatu za Utawala-wa-Sheria: Uhalali, Demokrasia na Haki-za-Binadamu, utawala-wa-sheria unahusiana na mahusiano kati ya wale-wanaotawaliwa na wale-wanaotawala na mahusiano kati ya vyombo-binafsi, ikiwa ni binadamu au chombo-chenye-uhai-wa-kisheria kama vile vyama na makampuni.

Utawala-wa-sheria mara zote huwa ndiyo kipimo pale madaraka-ya-kiserikali yanapotumika.
Wakati wowote ambao mtumishi-wa-serikali atatumia madaraka, lazima awe na mamlaka-ya-kisheria ya kufanya hivyo. Kwamfano, ikiwa mtumishi-wa-serikali anataka kuipekua nyumba, mtumishi-huyo-wa-serikali lazima awe na mamlaka-ya-kisheria yanayotakiwa. wakati wa kutumia madaraka yao, watumishi wa serikali lazima watii sheria.

Kwamfano, wakati wa kumkamata mtu, mtumishi-wa -erikali ana wajibu wa kisheria wa kuonyesha hati-ya-kukamata na kumwarifu mtu anayemkamata sababu za kumkamata. Mwenye kuhoji lazima amwarifu mtuhumiwa kuwa kila atakachokisema kinaweza na kitatumiwa dhidi yake mahakamani. Sheria inaamua madaraka yatumiwe namna gani.

Hii inaweza pia kuitwa “namna ya kulinda haki-ya-mtu” ambayo inakusudia, mfano, kulinda haki-za-watu na kuwalinda wasitiwe gerezani bila ya kuwepo mashtaka, na kuhakikisha kuwa watu wanaweza kuwafikia mawakili pindi wanapofunguliwa mashtaka au wanapokamatwa.

UTAWALA-WA-SHERIA UNAYAWEKA MATUMIZI YA MADARAKA CHINI YA SHERIA NA UNAHUSIANA NA MAHUSIANO KATI YA WATU-BINAFSI NA VYOMBO-VYA-BINAFSI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom