Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Umeweka maelezo mazuri sana
yana uzuri gani mkuu ,hayo maelezo ya jamaa
kama Yesu alikufa Alhamis na kuzikwa jioni yake, kwahiyo siku ya kwanza inaisha ijumaa jioni, ya pili inaisha jumamosi jioni na ya tatu inaisha jumaipili jioni
Kumbuka watu walienda kaburini jumapili asubuhi wakakuta ameishafufuka.
ambapo sasa three nights and three days hazijatimia
 
Mkuu kukusaidia tu jaribu kuangalia aina mbalimbali za sabato ambazo zilishikwa na wayahudi.

Kuna sabato za namna nyingi hapa katika tukio hili yohana anaitaja kabisa ilikuwa "High Sabbath" maana yake the first day of the feast of unleavened bread yani siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu.

Pili Yesu anaitwa mwanakondoo aondoe dhambi za ulimwengu sehemu kadhaa ilikuwa lazima auwawe siku maalum sio siku yoyote tu hii ni kwa sababu lazima ishara zote na unabii ukamilike.

Mkilazimisha Friday crucifixion mnaongeza maswali mengi kuliko majibu na mnawapa haki wayahudi kumkataa kwasababu anakuwa hakutimiza unabii wowote sasa wao wata muamini vipi MTU ambae muongo??? Kwa kigezo hicho wayahudivwanakuwa sahihi kumkataa lakini hali haikuwa hivo ni hizi doctrine za kulazimisha ambazo makanisa zimeokota kutoka kwa mama yao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Anayetoa hizo habari za kusulubishwa Yesu ni nani ikiwa Mark 14:50 ina sema Wanafunzi wake alipokamatwa wote walikimbia ??

Huoni hizi habari ni za mitaani tu hazina ukweli wowote
 
Je Yesu alikufa siku tatu kama alivyojitabiria au siku tatu (masaa 72) hazikufika au hakumaanisha siku tatu kamili? ( siku tatu za Yesu zilikuwa za masaa 72?)
Mathayo 12: 40 '' Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku'' (Mathew 12:40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.)
Kumbuka hili ni jibu la Yesu wakati akitaka kuwathibitishia mafarisayo na walimu waliotaka ishara kutoka kwake Mathayo12.38 Ndipo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema: “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” . Hivyo akatumia mfano wa Yohana kwa kuwaambia atakaa chini ya moyo wa ardhi kama alivyokaa Yona kwa siku tatu. Kwa hiyo hii ilibaki mioyoni mwao kama kipimo cha ukweli wake. Angefufuka kabla siku hizo tatu hazijafika mafarisayo wasingemuelewa. Wangemuita muongo na hakutoka kwa Mungu.

Kuna waalimu hufundisha kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa na wanaiita Ijumaa kuu ( Good Friday) na akafufuka Jumapili asubuhi na mapema.Je kuna ukweli hapo? Tukiamini kwamba Yesu alikufa Ijumaa mchana na akazikwa jioni kabla ya Sabato na kufufuka Jumapili asubuhi sana, Je siku Tatu zilitimia?

Kwa hesabu hizi alilala ijumaa usiku, akashinda jumamosi mchana na jumamosi usiku.
Je hizo ni siku tatu mchana na usiku kwa maana ya three days and three nights.

Wajuzi wa mambo tuelimishane hii ipoje
Zama zaidi mtafute mtu anayeitwa lsukiri.. uje na mlejesho.
 
Ukiesabu masaa, ata masaa 48 hayafiki, mfano kutoka ijumaa saa sita mpaka jmos saa sita ni 24hrs, kutoka jmos saa sita iyi mpaka jpl asubui ni karibu 18hrs, sasa apo nin haswa unataka, japo nnavyo ona ni kama walihesabu siku bila kuzingatia masaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ocran, umeanza comment yako vibaya, japo umefanya conclusion nzuri. Wayahudi walihesabu siku bila kuzingatia sana masaa. Kwa mujibu wa system yao ya kuhesabu time, Good Friday haikuanza usiku saa 6:00 sharp, ilianza jana yake baada ya jua kuzama. Siku ilihesabiwa hata kama tukio limetokea saa machache kabla ya siku kukoma (kukamilika). Mara chache, Wayahudi walipotaka kuwa a bit specific with time, waligawanya siku ktk makundi manne - Zamu ya I, Zamu ya II, Zamu ya III na Zamu ya IV.
Nikipata muda, nitarudi kufafanua kuhusu Zamu.
 
Siku zinazozungumzwa ni za matukio, na co cku kamili za kibinadamu yaani masaa 72,,
-siku ya kwanza kafara ya ukombozi ilitolewa kwa kifo cha Yesu Kristo (Ijumaa)
-siku ya pili, Yesu alipumzika kaburini(Jumamosi )
-siku ya tatu alifufukA(Jumapili )

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani alikwambia Yesu alipumzika kaburini siku ya Jumamosi? Jitahidi kusoma maandiko matakatifu ukiongozwa na Roho.
 
Ocran, umeanza comment yako vibaya, japo umefanya conclusion nzuri. Wayahudi walihesabu siku bila kuzingatia sana masaa. Kwa mujibu wa system yao ya kuhesabu time, Good Friday haikuanza usiku saa 6:00 sharp, ilianza jana yake baada ya jua kuzama. Siku ilihesabiwa hata kama tukio limetokea saa machache kabla ya siku kukoma (kukamilika). Mara chache, Wayahudi walipotaka kuwa a bit specific with time, waligawanya siku ktk makundi manne - Zamu ya I, Zamu ya II, Zamu ya III na Zamu ya IV.
Nikipata muda, nitarudi kufafanua kuhusu Zamu.
Mkuu hapa tunaangalia andiko Yesu mwenyewe alisema siku tatu, usiku na mchana. Na Yesu alikuwa myahudi pia muumbaji, hivyo anaposema siku tatu anajua anachomaanisha, akafafanua zaidi akasema usiku na mchana

Mathayo 12:40 NEN​

Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa siku tatu, usiku na mchana, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika moyo wa nchi siku tatu, usiku na mchana.
 
Wayahudi hawatumii hesabu ya saa 72, siku zao hupimwa jioni na asubuhi (Mwanzo 1:5, ... ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku moja) na haijalishi ikiwa ni sehemu ya siku - Jewish Nucyhmeron. Otherwise utapoteza muda mwingi kulazimisha hizo saa zako 72 ambazo hazitakufisha kunako pepo.
 
Je Yesu alikufa siku tatu kama alivyojitabiria au siku tatu (masaa 72) hazikufika au hakumaanisha siku tatu kamili? ( siku tatu za Yesu zilikuwa za masaa 72?)
Mathayo 12: 40 '' Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku'' (Mathew 12:40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.)
Kumbuka hili ni jibu la Yesu wakati akitaka kuwathibitishia mafarisayo na walimu waliotaka ishara kutoka kwake Mathayo12.38 Ndipo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema: “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” . Hivyo akatumia mfano wa Yohana kwa kuwaambia atakaa chini ya moyo wa ardhi kama alivyokaa Yona kwa siku tatu. Kwa hiyo hii ilibaki mioyoni mwao kama kipimo cha ukweli wake. Angefufuka kabla siku hizo tatu hazijafika mafarisayo wasingemuelewa. Wangemuita muongo na hakutoka kwa Mungu.

Kuna waalimu hufundisha kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa na wanaiita Ijumaa kuu ( Good Friday)
(i) Luka 23:54 - Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.
Swali: Siku ya Maandalizi ya Sabato huanza siku gani?
Day # 1
(ii) Mt. 27:62-64 - Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalizi ya Sabato, viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakamwendea Pilato 63 na kusema, “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mdanganyifu wakati alikuwa bado hai alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Kwa hiyo uamuru kaburi lilindwe kwa uthabiti mpaka baada ya siku tatu. La sivyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kuuiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuliwa kutoka kwa wafu. Udanganyifu huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”
Swali: Siku iliyofuata baada ya Maandalizi ya Sabato - ni siku gani?
Day #2 (Kesho yake)
Kwanini Makuhani na Mafarisayo walimwendea Pilato siku hii na kwanini isiwe kesho yake?
Wayahudi walijua fika kwamba siku ya tatu itakuwa wakati wowote ifikapo siku ya kwanza ya Juma ndiyo maana walimfuata Pilato mapema ili waweke walinzi pale kaburini.

na akafufuka Jumapili asubuhi na mapema.
Luka 24:1 - Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini.
Swali: Siku ya kwanza ya Juma ni siku gani?
Luka 24:21 - Lakini tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angelikomboa Israeli. Zaidi ya hayo, leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee.
Je kuna ukweli hapo? Tukiamini kwamba Yesu alikufa Ijumaa mchana na akazikwa jioni kabla ya Sabato na kufufuka Jumapili asubuhi sana, Je siku Tatu zilitimia?
Kwa hesabu hizi alilala ijumaa usiku, akashinda jumamosi mchana na jumamosi usiku.
Je hizo ni siku tatu mchana na usiku kwa maana ya three days and three nights.
Jaribu kutafuta na kusoma hii kitu: Jewish Nucyhmeron
Wajuzi wa mambo tuelimishane hii ipoje
Kwani Lesson zenu za Kisabato zinafundisha nini kuhusu hili?
 
(i) Luka 23:54 - Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.
Swali: Siku ya Maandalizi ya Sabato huanza siku gani?
Day # 1
(ii) Mt. 27:62-64 - Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalizi ya Sabato, viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakamwendea Pilato 63 na kusema, “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mdanganyifu wakati alikuwa bado hai alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Kwa hiyo uamuru kaburi lilindwe kwa uthabiti mpaka baada ya siku tatu. La sivyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kuuiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuliwa kutoka kwa wafu. Udanganyifu huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”
Swali: Siku iliyofuata baada ya Maandalizi ya Sabato - ni siku gani?
Day #2 (Kesho yake)
Kwanini Makuhani na Mafarisayo walimwendea Pilato siku hii na kwanini isiwe kesho yake?
Wayahudi walijua fika kwamba siku ya tatu itakuwa wakati wowote ifikapo siku ya kwanza ya Juma ndiyo maana walimfuata Pilato mapema ili waweke walinzi pale kaburini.

Luka 24:1 - Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini.
Swali: Siku ya kwanza ya Juma ni siku gani?
Luka 24:21 - Lakini tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angelikomboa Israeli. Zaidi ya hayo, leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee.

Jaribu kutafuta na kusoma hii kitu: Jewish Nucyhmeron

Kwani Lesson zenu za Kisabato zinafundisha nini kuhusu hili?
kwani kulikuwa na sabato ya aina moja tu?
 
Ukitaka kutambua kwa usahihi siku ambazo mwili wa Yesu Kristo ulikaa kaburini ni vyema uchunguze kwanza maandiko yanasemaje kuhusu msingi uliowekwa wa maadhimisho ya sikukuu za,
a) Sabato ya kila mwisho wa juma,
b) Pasaka,
c) Pamoja na siku 7 zinazoambatana na Sabato ndogo mbili za maadhimisho ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu.

Wayahudi walikuwa na sikukuu ya Sabato kubwa ambayo iliadhimishwa kila siku ya 7 ya juma. Katika sikukuu hii iliwalazimu kustarehe kabisa bila ya kufanya kazi yoyote ile, na pia kushiriki katika kusanyiko takatifu. Katika Sabato hii hawakutakiwa kufanya kazi yoyote ile, iwe ya utumishi ama kazi nyingine ya nyumbani isiyokuwa ya utumishi.

Aidha kulikuwa na sikukuu za sabato ndogo ambazo ziliadhimishwa mara moja kwa mwaka kama vile zilivyoainishwa ndani ya vitabu vya Torati, hazikupaswa kuadhimishwa kila juma kama ilivyo Sabato kubwa, masharti pekee ilikuwa wafanye kusanyiko takatifu na kutokufanya kazi za utumishi tu. Hivyo Torati haikuwalazimisha kustarehe kabisa na kuacha kufanya kazi zingine zisizokuwa za utumishi. Ebu kwanza tuirejee nukuu ifuatayo kutoka katika maandiko matakatifu,

MAMBO YA WALAWI 23

1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za BWANA, ambazo mtazitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu.
3 Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yoyote; ni Sabato kwa BWANA katika makao yenu yote.
4 Sikukuu za BWANA ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo
5 Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni Pasaka ya BWANA.
6 Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa BWANA ya mkate usiotiwa chachu; mtaila mikate isiyochachwa muda wa siku saba.
7 Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yoyote ya utumishi.
8 Lakini mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi
.

Yesu Kristo alikula sikukuu ya Pasaka na wanafunzi wake jioni ya siku ya 14 ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa Kiyahudi (Walawi 23:5). Ambapo baada ya hapo alikwenda nao bustani ya Gethsemane. Kutokana na juma letu hii ilikuwa ni siku ya Jumanne. Nukuu kutoka katika kipande cha Neno la Injili kinasema,

LUKA 22

7 Basi, siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwanakondoo wa Pasaka huchinjwa.
8 Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, “Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka.”

Siku ya 15, yaani siku ya Jumatano ilikuwa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu (Walawi 23:6), siku ambayo aliteswa na kufa msalabani muda wa saa 9 alasiri. Nukuu ya kipande cha Neno la Injili kinasema,

MATHAYO 27

45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza.
46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, “Anamwita Eliya!”
48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdomoni.
49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.”
50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho.

Siku ya 16, yaani Alhamisi, ilikuwa ni sikukuu ya sabato ndogo (Walawi 23:7), kwa kuwa ilikuwa ni siku ya kusanyiko takatifu ambapo Wayahudi hawakupaswa kufanya kazi za utumishi. Hii ilikuwa siku ya kwanza kwa mwili wake kukaa kaburini chini ya moyo wa nchi. Nukuu kutoka katika kipande cha Neno la Injili kinasema,

LUKA 23

50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya, ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye alikuwa mjumbe wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshimika.
51 Lakini yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo cha kumsulubisha Yesu.
52 Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu.
53 Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi hilo lilikuwa halijatumika bado.
54 Siku hiyo ilikuwa ni siku ya Maandalio, na sabato ilikuwa karibu ianze.
55 Wale wanawake waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo.
56 Kisha wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili. Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.

Siku ya 17 ya mwezi huu wa Kiyahudi, yaani siku ya Ijumaa, ilikuwa ni siku ya maandalizi ya sikukuu ya Sabato kubwa ya kila juma. Hii ilikuwa ni siku ya pili kwa mwili wake kukaa kaburini. Nukuu kutoka katika kipande cha Neno la Injili kinasema,

MATHAYO 27

62 Hata siku ya pili, yaani ndiyo iliyo baada ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato
63 wakamwambia, “Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’
64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.”
65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.”
66 Wakaenda wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na
kuwaweka askari walinzi.

Na hatimaye Bwana Yesu Kristo alifufuka kutoka katika wafu siku ya 18 ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa Kiyahudi, yaani siku ya Jumamosi, saa 9 alasiri, baada ya kutimia kwa siku tatu kamili za mwili wake wa awali wa kibinadamu kukakaa kaburini kama vile yeye mwenyewe alivyonena kuhusu jambo hilo.

Tukio hili lilitokea siku ya Sabato kubwa ambayo Wayahudi walipaswa kustarehe kabisa na hawakutakiwa kufanya kazi za namna yoyote ile. Ndiyo maana wakuu wa makuhani walikwenda kumuomba Pilato ulinzi wa kaburi ufanywe na askari wa Kirumi.

Ikawa jioni, ikawa asubuhi siku ya 19 ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa Kiyahudi, yaani siku ya Jumapili alfajiri na mapema, ndipo taarifa za kufufuka kwake zilipoanza kusambaa. Lakini tukio la kufufuka kwake na kuondoka kwake kaburini lilidhihirika na kuwa bayana kabisa kwa wale askari wa Kirumi waliokuwa na jukumu ya kulilinda kaburi lake, nao walikwenda kutoa ushuhuda wao kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao waliwahonga kwa fedha kuuficha ukweli huo. Nukuu ya kipande cha Neno la injili kinasema,

MATHAYO 28

11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu yote yaliyotokea.
12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana, waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na
13 kuwaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’
14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata shida yo yote.”
15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha wakafanya kama walivyoagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi mpaka leo.

Hakuna utata wowote ule katika hesabu za siku 3 za mwili wa Yesu Kristo kukaa kaburini. Maandiko matakatifu yanahitaji hekima kubwa sana kupitia karama za Roho wa Kristo, ili kuweza kuyapatanisha vyema na kuleta maana sahihi iliyokusudiwa kwa kuzingatia misingi iliyojengeka kupiria katika Neno hilo hilo.

Ukiyasoma pasipo kuwa na hekima hii utaishia kujichanganya wewe mwenyewe na kisha kuishia kuleta tafsiri potofu sana. Neno la Mungu hujisimamia na kujitetea lenyewe, halihitaji falsafa, dhana, elimu wala simulizi za mapokeo ya kibinadamu ili kujenga mantiki. Jambo la msingi ni kuzipatanisha aya sahihi ili zitupe kwa usahihi ujumbe uliokusudiwa.

Mbarikiwe sana kupitia Jina lipitalo majina yote duniani na mbinguni, Jina la BWANA YESU KRISTO.
 
Hamuwezi kupata jibu sahihi kwasababu yesu mwenyewe hajawahi kufa na akafufuka bali ni stori za kale zilizojaa uongo na utapeli wa mawazo.
 
Back
Top Bottom