Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,310
35,745
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
 
Ukweli usemwe tu huu muungano hauna maslahi kwa bara ni mzigo tu.
 
Wanasem Wazenji kwamba wakipewa uhuru wao, watawaita Waarabu wa Dubai na Oman wapabadirishe hapo pawe kama Dubai...

Sasa akili zao zilivyo fupi, chakula kinatoka Bara.. na Wazenji wengi hawana kazi za maana nikimaanisha hakuna mzunguko wa hela unaoeleweka ukiweka pembeni shughuli za Utalii na Uvuvi.

Mazao yao hayo ya karafuu, mwani etc havitoshi kuingiza kipato kwa mtu mmoja mmoja.

Ikumbukwe karibu nusu yao wapo huku Bara.. wakipewa uhuru wao na sisi tunawatimua huku warudi kwao hivyo overpopulation itakuwepo na ufinyu wa resources lazima uzidi kuwadidimiza.

I wish siku ifike kila mtu abebe chake.
 
Siyo kwa huo ukanda wetu comrade. Karibu visiwa vyote vinategemea Tanganyika. Kuna wengine walimpindua Rais, wakaja kuomba TZ imfurushe aliyempindua Rais, na TZ wakaenda kumfurusha.

Ova
Hii ya kumpindua rais hata Tanganyika ilitaka tokea wakati wa Nyerere na MI6 ilisaidia(UK). Sio visiwa tu ndio vyenye mambo ya kusaidiwa ikitokea mapinduzi nchi za Afrika magharibi ishatokea sana tu.

Mfano mdogo Burundi imehitaji msaada nao pia miaka michache tu iliopita kwa Tanzania. Tusitumie nguvu na ujanja kuwa tawala wa zanzibar kwa njia ya muungano.
 
Unaitaja Tanganyika bila kufikiri kuwa ilikuwa na umri gani tangu ipate uhuru wakati huo wa kuomba msaada baada ya mapinduzi.

Burundi nayo ni ya kutolea mfano kama nchi iliyofanikiwa? Ungetaja Rwanda labda.

Comrade, umeshaenda kwenye hivi visiwa tunavyovizungumzia? Hata kile kilichojipendekeza kwa Ufaransa, kikoje hali yake?

Ova
 
Ni sawa na kusema Tanzania bila ya misaada ya ulaya isinge toboa.

Hivi kuna kisiwa duniani hakiwezi jiendesha wenyewe?.
Nakwambia hivi, Tanganyika kwa sasa ndio inatusitiri sisi wazanzibar. Bila Tanganyika hatuna ulinzi, usalama wala umeme.

Karafuu iliyokuwa inatupa jeuri ilishakufa kitambo sana, na kwa uvivu wetu tumeshindwa kuifufua, na sasa tunasikia huko Tanganyika mlishaanza kuotesha na kuvuna karafuu yenu kwa fujo.....

Bandari ya Zanzibar iko mahututi maana kila jirani yetu (Beira, Mombasa, Comoro, Eritrea, Djibout, Dar, Mtwara, Tanga) alisha imarisha bandari yake, Zanzibar hatuna tena upekee wa kibandari....

Zanzibar tumebakia na Utalii pekee yake (ambao ni wa msimu, na watalii wenyewe wengi huanzia bara au kumalizia bara maana huko wako huru kuvaa chochote, kula mwaka mzima (huku kula hadharani kipindi cha Ramandan ni mwiko!), kula chochote (hata kitimoto), kunywa chochote(pombe), hapa Zanzibar watalii wanapita kwa siku zisizozidi tatu (kushangaa mchanga mweupe wa beach ambao umegundulika umejaa vilivyo kule Tanganyika (Kigamboni), kutafuna machoko wakizenji na kubwia unga kwa uhuru kisha kusepa zao). Bahati mbaya sana na huo utalii pekee hautoshi kuendesha maisha ya wazanzibar zaidi ya 1.5milioni kwa siku zaidi ya 90.

Yote kwa yote, mmasai ameshaingia Zanzibar na sasa anataka kutawala utaliii wote.

Nasema hivi, Zanzibar bila Tanganyika twafaa!
Mtanganyika anatujali mnooo.
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
Hakuna kitu kizuri kama kuwa na shukrani!. It's about time Zanzibar iwe na shukrani na kuonyesha shukrani kwa yote mazuri Bara inayowatendea.
P
 
Ila Zanzibar ina potential kubwa sana. Kuishi chini ya kivuli cha Tanganyika ni kujichelewesha.
Potential ipi hiyo tena ipo Zanzibar kwa sasa?
Karafuuu?
Nazi???
Tende??
Bandari?
Utalii???

Labda kama tutaanza kuchimba mafuta, lakini tukianza tu basi mfaransa, muingereza, mmarekani, mchina au mrusi ataweka kambi na huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa sisi waswahili pale Zenji.
 
Ukweli usemwe tu huu muungano hauna maslahi kwa bara ni mzigo tu.
Mimi mpaka kesho najiuliza, nyinyi watanganyika mnafaidika nini na huu muungano?
Nani aliwaloga?
Hampati chochote na bado mnabebeshwa mzigo mzito wa kuihudumia Zanzibar lakini hamchoki tu.

Yaani Mzanzibar ataendelea kumdharau kila mtanganyika milele.
 
Nakwambia hivi, Tanganyika kwa sasa ndio inatusitiri sisi wazanzibar. Bila Tanganyika hatuna ulinzi, usalama wala umeme.

Karafuu iliyokuwa inatupa jeuri ilishakufa kitambo sana, na kwa uvivu wetu tumeshindwa kuifufua, na sasa tunasikia huko Tanganyika mlishaanza kuotesha na kuvuna karafuu yenu kwa fujo.....

Bandari ya Zanzibar iko mahututi maana kila jirani yetu (Beira, Mombasa, Comoro, Eritrea, Djibout, Dar, Mtwara, Tanga) alisha imarisha bandari yake, Zanzibar hatuna tena upekee wa kibandari....

Zanzibar tumebakia na Utalii pekee yake (ambao ni wa msimu, na watalii wenyewe wengi huanzia bara au kumalizia bara maana huko wako huru kuvaa chochote, kula mwaka mzima (huku kula hadharani kipindi cha Ramandan ni mwiko!), kula chochote (hata kitimoto), kunywa chochote(pombe), hapa Zanzibar watalii wanapita kwa siku zisizozidi tatu (kushangaa mchanga mweupe wa beach ambao umegundulika umejaa vilivyo kule Tanganyika (Kigamboni), kutafuna machoko wakizenji na kubwia unga kwa uhuru kisha kusepa zao). Bahati mbaya sana na huo utalii pekee hautoshi kuendesha maisha ya wazanzibar zaidi ya 1.5milioni kwa siku zaidi ya 90.

Yote kwa yote, mmasai ameshaingia Zanzibar na sasa anataka kutawala utaliii wote.

Nasema hivi, Zanzibar bila Tanganyika twafaa!
Mtanganyika anatujali mnooo.
Hata mchanga tu wa kujengea majumba ya Zanzibar unatoka Tanganyika.

Ova
 
Wanasem Wazenji kwamba wakipewa uhuru wao, watawaita Waarabu wa Dubai na Oman wapabadirishe hapo pawe kama Dubai...

Sasa akili zao zilivyo fupi, chakula kinatoka Bara.. na Wazenji wengi hawana kazi za maana nikimaanisha hakuna mzunguko wa hela unaoeleweka ukiweka pembeni shughuli za Utalii na Uvuvi.

Mazao yao hayo ya karafuu, mwani etc havitoshi kuingiza kipato kwa mtu mmoja mmoja.

Ikumbukwe karibu nusu yao wapo huku Bara.. wakipewa uhuru wao na sisi tunawatimua huku warudi kwao hivyo overpopulation itakuwepo na ufinyu wa resources lazima uzidi kuwadidimiza.

I wish siku ifike kila mtu abebe chake.
Muarabu wa nini tena Zenji wakati tulishamtimua kwa mapinduzi mwaka 1964?
Aje kufanya nini tena Zanzibar?
Aje kututawala?
Hatumtaki na hatumhitaji, na hilo analijua na analizingatia.

Labda aje kukodisha (kununua?!) visiwa vidogo vidogo, maana viko vingi tu, na mswahili hana akili za kichaga au kikinga kuweza kuvitumia kibiashara hivyo muwekezaji yoyote wa kigeni (hata mzungu au mchina) aje tu kuwekeza, milango iko wazi hata sasa.
 
Japokuwa huu muungano ni kichefu chefu tu kwa wazanzibar lakini ukweli mchungu ni kuwa, bila huruma na upendo wa Tanganyika basi huenda Zanzibar tusiweze kutoboa hata miezi mitatu.

Kuanzia Ulinzi, Usalama mpaka umeme tunapewa bureee na watanganyika. Kodi na rasimali za watanganyika ndio zinatupa maisha wazanzibar.

Rasimali na mapato yetu ya ndani ya Zanzibar hayawezi kutosha kugharamia ulinzi, usalama, umeme na huduma zingine muhimu za kijamii kwa zaidi ya miezi mitatu, tutaangamia!
Kabla ya kuitwa nchi, kabla ya ukoloni, walikufa? Chkua time.
 
Unataka kutupiwa majini ?
Majini yalikuwa yanatumika kutisha watu Zanzibar enzi za zamani huko, kwa sasa huwezi kumtisha mtu na majini Zanzibar. Maana dawa ya majini (Kitimoto!) inapatikana vizuri tu visiwani. Zenji tunaita ni antidot, maana inazuia majini mpaka popobawa.

Aliyeanza kuleta kitimoto Zanzibar ana siti yake peponi, maana ametupa uhuru kweli kweli.
 
Back
Top Bottom