Ukitaka kukosa furaha jaribu kufuatilia mambo ya watu

Accumen Mo

JF-Expert Member
May 15, 2022
15,442
33,336
Habari wanajf!

Basi kama kawaida yetu kujadili na kupeana mawili matatu, basi leo nakuletea mambo yaliyopo duniani ambao kwa 99% ndio uhalisia.

Hii ni tafiti yenye ushahidi wa kutosha, mambo hayo ni;

1. Ukitaka kukosa furaha jaribu kufuatilia mambo ya watu, kama kufuatilia imani za watu, tamaduni na mila zao kwa sababu duniani nzima kuna jamii zeny mitazamo tofauti.

2. Mitandao ya kijamii imechangia pakubwa kuleta msongo wa mawazo, watu kuona wengine wakiwa na kipato kupitia mitandao ya kijamii hata kuishi maisha mazuri ilhali wao hawana kitu, watu kuona wapenzi wao wa zamani maarufu kam ''EX'' wakiwa furaha mitandaoni nayo imeongeza stress.

3. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba kufanikiwa kunatokana na juhudi. Sababu kubwa watu wengi waliofanikiwa wanatokana na sababu nyingine tofauti na juhudi ambazo ni zaidi ya 80%.

4. Hakuna sababu ya muhimu inayowafanya binadamu kuzaliana zaidi ya kuendelea kusalia duniani, kuzaliana ndio kumefanya mpaka leo kiumbe binadamu kuwepo duniani na wala watu hawana sababu za msingi za kuzaliana zaidi ya kufuata mfumo yaani kama utaratibu tu hakuna sababu ya msingi.

5. Hakuna ushahidi wa kutosha kwamba dini zililetwa na wakoloni Africa kwa sababu nchi kama Ethiopia na liberia hazijawahi kutawaliwa, zina mfumo wa dini tena ule mkongwe kabla hata ya ukoloni tena wanafuata asilimia kubwa ya watu wake.

6. Wajinga pekee ndio wanaamini dini zimerudisha nyuma maendeleo ya Africa, ndio wajinga kwa vile hakuna uhusiano wa dini na maendeleo ya nchi za Kiafrica, kuna sababu nyingi kama ukoloni ndio kubwa.

7. Waafrika walikuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa ambazo sasa zinazalishwa
India kwa kutumia chuma, watu waliacha kuzalisha bidhaa hizo baada ya kuja elimu ya mkoloni hapo watu wakaanza kuamini kweny kuajiriwa na kukaa kweny viti wakiwa wamevaa suti (Boss).

8.Watu weny akili sana (genius) wana tabia za ubishi, ubinafsi, dharau hata ugomvi. Takwimu zinaonyesha watu hao kama walisoma basi walishawahi kugombana au kubishana na walimu wao katika kujenga hoja na kuuliza maswali yao.

9. Africa ingeweza kufanya vizuri zaidi kidunia kama ingefanya mapinduzi ya kilimo tu.

10. Mtu anayekufa hana wasiwasi wala uoga wowote kuhusu kifo, sababu ubongo wake ulishakubaliana na hali ya kifo.

11. DUniani wapo watu wenye pesa kuliko wale wanaotajwa na forbes, ile list ni ambao wanafanya kazi tu ila wapo ambao hawafanyi kazi na wana pesa. Utajiri wao wa pesa wanaprint tu na kuamua kutumia popote dunia ila sheria za pesa zinawabana wengi wapo uingereza.

12. Nchi yenye nguvu zaidi duniani ni uingereza, ikiwa na mamlaka ya kiroho sio nguvu ya kawaida katika kutawala ulimwengu, watu wengi wanaamini ni nguvu za kishetani.

13. Wazungu wanafundishwa kwamba Africa ina watu wajinga hawana uwezo wala elimu, wakati huo wafrica wanafundsihwa kwamba wazungu ni watu weny akili, wana mioyo safi wanaleta misaada africa. Hii ndio sababu kubwa ya mtu mweusi kuwa chini duniani.

14. Umaskini duniani ni wa kutengenezwa na wanadamu wenyewe kwa sababu walichagua kuipa thamani pesa na kuandaa mfumo mmoja centralized, mfumo huo ndio unaratibu uchumi wa watu wote duniani. Ukitaka kuamini Marekani kuna homeless kibao ila nchi inatoa mpaka trillion kufanya vita nch nyingine wakati vita ya umaskini kwao bado ipo kwa uchache.

15. Serikali ya TZ na zote duniani zinao uwezo wa kuwahudumia wastaafu wote bila ya kukusanya michango yao katika mifuko ya hidhafi kama NSSSF.

16. Watu wengi waliosoma mpaka kufika kiwango cha juu cha elimu kama masters na Phd, halafu wakafanikiwa kweny biashara basi sio elimu ndio imewafanya kufanikiwa bali ni connection za watu wengi wailokutana nao ndio ziliwafanya kufanikiwa kweny biashara kama kupata wazo la biashara, masoko ya bidhaa zao.

17.Hakuna uhusiano wa elimu na kufanikiwa kwenye biashara, ukileta elimu ya darasani basi jiandae kuangukia mbavu, elimu inafanya kazi pekee kweny kuendeleza biashara sio kuanza.

18. Inawezekana mitazamo yako kuhusu maisha na dunia ikabadilika pale utakapotembelea sehemu tofauti dunia, ushauri jaribu kutembea sehemu tofauti unaweza kupata mawazo mapya kuhusu maisha na dunia kwa ujumla.

19. Watu waliofanikiwa kweny biashara baada ya kuoa au kuolewa, asilimia 90% waliwasharikisha wenza wao kweny biashara zao bila ya kuwaficha chochote.

20. Wanawake wana uwezo mkubwa kiakili na kiuendaji ila mwanaume ndio mtalawa wa dunia ndio maana sio rahisi wanawake kuitawala dunia katika nyaja tofauti kama kiuchumi, sababu kubwa kuna wanaume.


21. Ukifikisha miaka 80 ndio unakuwa mtu halisi mwenye uwezo wa kufikria bila ya kuingiliwa kifikra na mambo ya kidunia, umri huo mtu anaweza kufanya jambo bila ya kujali uwezo wako wa kipesa wala elimu. Usishangae mzee wa miaka 80 akawa anakula vyakula vya kawaida kama ugali na kuishi kawaida japo ana pesa nyingi bank.

22. Dini ni mpango wa ulimwengu kama ilivyo kuwa na mitazamo tofauti kwa sababu miaka 2000 nyuma walikuwepo atheists ila hawakufua dafu, asili ya dunia kila mtu ana mtazamo wako hivyo huwezi kulazimisha watu wasiamini wanachoamini.

24. Duniani kila sehemu iwe nchi au jamii kuna tamaduni zao, so jaribu kuendana na sheria za kila sehemu unapofika hii itakufanya uwe mwerevu zaidi.

25. RIba kwenye mikopo ndio inawafunga watumishi kufikia malengo yao, akichukua mkopo miaka 5 ina maana hapo hawezi kuacha kazi ndani ya miaka mitano ili aendelee kulipa mkopo na ikiisha atakuwa kapata hasara zaidi maana kalipa riba. Basi atakopa na kuendelea kusalia kazini kwa vile mkopo unamfunga, takwimu 20% ya watumishi wa serikali walitaka kuacha kazi ila waliogopa mkopo watalipaje ikiwa tayari washachukua mkopo.

26. Hakuna binadamu anajua kesho yake, haya ya kuandaa kesho yetu ni sehemu ya maisha yanachangia 60% pekee nyingine ni mfumo wa maisha ya dunia, hata Rais wetu hakuwa na ndoto ya kuwa Rais.

27. Matajiri wanapata furaha zaidi wanaposaidia watu, sawa furaha wapatayo kupitia kufanikiwa kweny biashara zao.
 
Mitandao ya kijamii imechangia pakubwa kuleta msongo wa mawazo, watu kuona wengine wakiwa na kipato kupitia mitandao ya kijamii hata kuishi maisha mazuri ilhali wao hawana kitu, watu kuona wapenzi wao wa zamani maarufu kam ''EX'' wakiwa furaha mitandaoni nayo imeongeza stress.
sidhani… mimi naona mitandao inaleta amsha amsha full burudani yan. Muda wa kustresika unautoa wapi
 
Ile namba 5. nakujibu sawa ethiompia haikukoloniwa lakn ilitembeleewa na wamisionali kutoka huko ulaya kabla ya bara la africa kugawiwa kwenye mkutano wa berlin, waafrica wakoloni kutoka ulaya waliwakuta na tamaduni zao. Waliwakuta hawajuw kama kunayesu alitokea duniani. Wakawafuza wao kuhusu biblia na yesu, alafu haohao waafrica wakawafanya kuwa watumwa, manyanyaso na kuwapeleka america utumwa??
 
sidhani… mimi naona mitandao inaleta amsha amsha full burudani yan. Muda wa kustresika unautoa wapi
Inachangia sana kuleta unyonge ndio maana watu wa magharib wanatumia vyombo vya habari kutawala wengine kifikra.
 
Ile namba 5. nakujibu sawa ethiompia haikukoloniwa lakn ilitembeleewa na wamisionali kutoka huko ulaya kabla ya bara la africa kugawiwa kwenye mkutano wa berlin, waafrica wakoloni kutoka ulaya waliwakuta na tamaduni zao. Waliwakuta hawajuw kama kunayesu alitokea duniani. Wakawafuza wao kuhusu biblia na yesu, alafu haohao waafrica wakawafanya kuwa watumwa, manyanyaso na kuwapeleka america utumwa??
Usiwe mbishi dini ya wamisionaries na waethipia ni tofouti kumbuka hao ni orthodox wale ni catholic
 
Ile namba 5. nakujibu sawa ethiompia haikukoloniwa lakn ilitembeleewa na wamisionali kutoka huko ulaya kabla ya bara la africa kugawiwa kwenye mkutano wa berlin, waafrica wakoloni kutoka ulaya waliwakuta na tamaduni zao. Waliwakuta hawajuw kama kunayesu alitokea duniani. Wakawafuza wao kuhusu biblia na yesu, alafu haohao waafrica wakawafanya kuwa watumwa, manyanyaso na kuwapeleka america utumwa??
Angalia ethipia
 

Attachments

  • VID_80570101_195229_621.mp4
    29.8 MB
Dini ni utapeli tu kutoka kwa wazungu, ili kuwatapeli waafrika, kudumaza hakili zao, kifikira ili waendelee kuwa watumwa mambo leo??
 
Back
Top Bottom