Ni miaka mingi sasa imepita tokea nimalize elimu yangu ya shahada(degree) kwenye moja ya top three ya kozi ngumu sana hapa Tanzania.
Lakini leo nitapenda kutoa ushuhuda wangu namna elimu yangu ya chuo ilivyokua , kupata mafanikio makubwa ya kibiashara na kupelekea watu wengi kunishangaa
Kiufupi kwenye elimu ya sekondari na kidato cha tano mimi nilikua msongo, nikisema msongo namaanisha msongo haswa to the extent kwamba, Olevel nilibeba vyeti 8 kati ya tisa, na Advance nikiwa nasoma sayansi nilibeba vitatu kati ya vitano na kwenye matokeo ya mwisho ya olevel na alevel nilifanikiwa kuibuka kinara,
hii si mada ya leo, ni chombeza tu, sasa twende kwenye mada ya leo
baada ya kuchaguliwa elimu ya chuo kikuu, Semester ya Kwanza nilikua napenda shule sana na hata wale wasongo ilifikia sehemu tukipewa pepa zetu(maana kuna baadhi ya masomo walikua hawabandiki matokeo), lazima waje kuconfirm nimepata ngapi, maana wasongo hua wanajuana, haikua case.
Kufika mwaka wa pili akili ikawa haitaki kukomaa na shule muda wote nawaza biashara tu, nikaanza biashara mdogo mdogo ilivyokolea nikawa ni mzee wa kudoji mapindi, nachukua slides kwa wana napiga msuli, napiga pepa biashara imeisha.
Mwaka wa tatu biashara zikawa zimeninyookea wakuu, yaani nilikua na biashara kama tatu halafu zote zinalaza pesa nzuri sana(kwa kifupi nilipatia biashara na locations) nikaamua kununua gari ndogo ya kutembelea kama 10M kipindi hicho, lakini ninachomshukuru Mungu sikuwa mtu wa Mademu kabisa, nilikua na demu mmoja tu halafu 1st yr kwa wakati huo, kwa kua nilikua na uchumi halafu niko busy mara nyingi nilikua nikitaka mzigo alikua akinipatia maana pia alikua akiniogopa(pesa huleta msimamo na heshima) japo nae alikua hapati shida ndogo ndogo, Pombe nilikua nagusa occasionally (kwa matukio) mfano kwenye birthday za chuo, outing na washikaji mara moja moja,
Mwaka wa nne nikanunua kiwanja changu cha kwanza kikiwa na boma milion 12(jamaa alikua na shida sana), yaani hapo mambo yamejipa si kitoto, ila sikua na wazo la kusema sijui niache chuo, yaani nilikua matured mpaka wakati huu hua nashangaa nilikuaje
baadae niliongeza biashara zikawa nne na zote zimepamba moto, halafu nilikua yanki tu, ilipelekea chuo kizima kujulikana. lakin wengi walikua hawanijui kwa sura kwamba ni mimi, wanajua baadhi ya biashara zangu na jina kwa kuambiwa.
Pia watu wengine walikua wakisikia story zangu na biashara zangu na wakija kuoneshwa kua ni mimi wakawa hawaamini, kwasababu pia sikua mtu wa matukio wala magroup, nilikua na circle ndogo tu ya washikaji wa damu ikikaribia mitihani labda UE, wiki nzima nakesha library na madarasani (nilikua sifanyi discussion kwa kua sikuzoea kabisa toka kusoma kwangu kote), biashara nafanya kwa kuwapigia simu wafanyakazi na kutembelea kidogo, kiufupi nili delegate usimamizi ila nilikua mkali sana kwenye biashara, ukizingua huna kazi,
Namshukuru Mungu sikuwahi kupata Supp ya somo lolote mpaka namaliza chuo.
Mpaka namaliza chuo nilikua na mtaji kama 97M ukiongeza na hiyo asset ya kiwanja nilipomaliza tu baada kama ya miezi mitatu nikapata ajira gvt, kiukweli biashara ilikua hot sana, niliomba ajira kama kujaribu kwakua home walikua wakinisihi sana na hawakujua kama mtoto wao huku mambo yalishajipa,(sikuwah kuwaambia chochote), na home ilikua mkoa wa mbali sana nilienda kuanza kazi nikiwa na mtaji wa zaidi ya milioni 100 (biashara, assets na Cash).
Inshort niliajiriwa nikiwa tayar nimetoboa, japo kazi za serikali zimerudisha nyuma biashara zangu, ila si sana (nitakuja kusimulia siku nyingine).
Lakini mpaka leo hua siamini ninachokiona, maana nilikula U-turn ambayo ilibadilisha maisha yangu, sijui ningekomaa na shule tu leo ningekua wapi lakini naishikuru biashara imenipa kila kitu nilichotaka tena katika umri mdogo ambao nilichanganya na masomo pia.
Tuliochanganya elimu na biashara na tukatoboa kotekote tukutane hapa.