SoC04 Tanzania ifanye haya kupunguza mfumuko wa bei nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

jastin22

New Member
May 2, 2024
3
0
Mambo matano ya kuyafanya

1. Kuweka mkazo katika sera zake za uendeshaji wa mashirika binafsi kuzalisha malighafi za viwandani kama alizeti, miwa pamoja na mazao ya chakula.

2. Kupunguza ushuru katika vifaa vya kilimo kama uagizaji wa trekta za kulimia ili kuweka usawa na watu binafsi waweze kuagiza vifaa hivyo.

3. Kuwapa mkopo kwa kutumia halimashauri wale wenye ndoto ya kwenda katika sekta ya kilimo.

4. Kupokea hoja na kuzitatua kwa wale wanaohitaji kujikita katika sekta zinazozalisha.

5. Kuongeza watalaam katika sekta kuhudumia wahitaji katika sekta zinazozalisha kama Kilimo.
Hayo ni mambo muhimu matano ya kufanya ili kupunguza mfumuko wa bei nchini
 
Okay tumesikia na pointi zako zimejikita katika kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya UZALISHAJI katika kilimo.

Sasa hayo yote yakishafanyika linatakiwa SOKO la kilimo la uhakika. Tena hii ya soko na uwekezaji ni kama kuku na yai 'paradox'. Japo mimi kama ambavyo ninachagua alianza kuku, basi pia ninachagua lianze soko.

Manaake kama uliyoanzisha yakifanyika peke yake, tutakuwa na uzalishaji mwingi msimu fulani na mdogo msimu mwingine. Kwa hiyo mkulima atalia wakati wa kushuka bei. Na mnunuzi atalia wakati wa mfumuko wa bei(kama andiko linavyogusia)

Na ndugu yangu hatutaki mmoja alie mwingine acheke kwa wakati wake. La. Tunataka wote tucheke wakati wote WIN WIN
 
Back
Top Bottom