Tahadhari ili kuepuka gharama uji wa ulezi huchanganywa na unga wa mchele

Yeh, unga wa ulezi wanaweka maziwa mgando baada ya uji kuiva. Huu ni upikaji wa asili unavyokuwa huko uchagani. Pia huwa wanaongeza siagi kama uchumi unaruhusu. Huu upikaji wa uji wa ulezi kwa watoto ambao huchanganya vitu kama karanga, ngano nk. ni version ya ambayo imeanzia mjini.
Hii nimeisikia kwako kwa mara ya kwanza yan uji wa ulezi pekee!?
 
Unga wa uji Mimi mamaangu alikuwa anaweka mahind,ulezi,ngano,mchele karanga na soya
Sijui labda Kuna kingine kinafanya ukose ladha lkn sio mchele

Nyie wa wapi hamjui hata Jinsi unga wa uji unakuwaje Kuna aina nyingi sana
Dr Lizzy
Missy Gf hebu njoeni kwanza
Aaliyyah mi kwenywe swala uji sio mtaalam kabisa!🙈

Sio mpenzi, kina Jr nao walikataa kabla hata hawajajua what it was, kwahiyo nipogi nipogi tu.
 
Mkuu kwani TFNC -
"Tanzania Food and Nutrition Centre" ina kazi gani?

TFDA unayosema haikufutwa bali ilitengenishwa Vyakula kivyake na Madawa kivyake ili kuleta ufanisi kwa hiyo vyakula vinasimamiwa haswaa.
Asante kwa ufafanuzi. Hebu eleza ile taasisi iliyofutwa ilikuwa ikishughulikia maswala gani. Hapo ndipo sikuwa na ufahamu napo.
 
Hii nimeisikia kwako kwa mara ya kwanza yan uji wa ulezi pekee!?
Yap. Wachaga mbona ni chakula chao cha asili kwa wanawake waliojifungua? Kama ni kuchanganya mambo mengine haya mambo yameanza miaka ya karibuni. Zamani ilikuwa uji wa ulezi+maziwa mgando+siagi(option)
 
Hahahah Tanzania bhana Kwan mchele n sumu inamana hujawah sikia unga wa lishe
 
Tatizo la mchele ukiwa unga ukizidisha kipimo uji wake unakuwa mzito kwa haraka sana (kumbuka vitumbua) ukitaka kuhakiki hilo ukoroge uji wa mchele peke yake haunogi kabisa
 
Unajua balaa la uji wa ulezi ambao haukuchanganywa na nafaka nyingine yoyote?
Unga wa ulezi ni lazima uchanganywe na mafaka zingine kama mchele, mihogo, karanga, ili kuzuia mnywaji kupata ugumu wa choo. Unajua balaa la ulezi tupu wewe, ukienda chooni ni balaa.
 
Unakumbuka ile taasisi ya Lishe serikali iliifuta?
Inawezekana serikali ilifanya hivyo kwa ujinga ilionao, kutojua umuhimu wa taasisi kama hiyo.
Hata hivyo nachelea kusema serikali itakuwa imechukuwa uamzi kama huo kwa vile taasisi ilikuwa ikifanya kazi zake kwa ueledi.

Mambo kama haya uliyo yaelezea hapa hutokea kwenye nchi hovyo hovyo kama hii yetu sasa hivi. Serikali hakuna inalosimamia kwa ufanisi, kila jambo ni hovyo hovyo tu.
Kwani Kuna tatizo Gani kuchanganya mchele na ulezi?
 
Kwani Kuna tatizo Gani kuchanganya mchele na ulezi?
Sioni tatizo linaloweza kutokea kuchanganya mchele na ulezi. Binafsi, nijuavyo hakuna tatizo. Lakini hilo siyo swala hapa.
Anayeuza huo uji anatangaza ni uji wa ULEZI, na mnunuzi, ananunua kwa kuamini hivyo alivyo ambiwa, kuwa ni uji wa ulezi; kumbe ukweli ni kwamba ni uji wa mchanganyiko, ulezi na unga wa mchele.
Sasa niambie, hakuna udanganyifu hapo?
 
Kwani ulezi una extra Gani kiubora zaidi ya mchele?zote si ni wanga tu?au Mimi ndio sielewi
 
Kwani ulezi una extra Gani kiubora zaidi ya mchele?zote si ni wanga tu?au Mimi ndio sielewi
LOooh! Joannah.
Ni hivi: kabla hata ya kwenda huko kwenye ubora n.k., ni udanganyifu, kudai kwamba mtu anauza uji wa ulezi, wakati ni mchanganyiko wa ulezi na unga wa mchele. Aseme tu wazi kwamba anauza uji uliochanganywa ulezi na mchele, na watu wanaotaka uji wa namna hiyo watanunua kwa hiari yao wenyewe, kwa bei iliyopangwa na muuzaji.

Kuna watu unapowaambia ni uji wa ulezi, wanajuwa ni ulezi ambao haukuchanganywa na mchele, na wao watanunua kwa bei husika. Hapo hakuna udanganyifu wowote.

Kuhusu utofauti uliopo kati ya ulezi na mchele, kuna vitu vingi; inaweza hata kuwa ni muonjo wake tu; kiasi cha wanga, 'fiber', na kadhalika. Bado hatujazungumzia madini, na hata kiasi cha protein, hata kama ni kidogo sana kwa kila moja wapo.

Lakini ninachokusisitizia ni hilo la kutokuwa mdanganyifu unapofanya biashara ya aina hiyo. Bila shaka unajua kwamba bei ya ulezi ipo juu kulko bei ya unga wa mchele. Sasa nikuulize hapa, wewe unadhani ni kwa sababu gani?
 
😁😁 Nimependa ulivyoanza maelezo,yaani ni kama nakuchosha....Ukisema ulezi upo juu kuliko mchele unakosea,bei ya soko inayotambulika na wizara ya viwanda na biashara mchele ndio uko juu,mchele min ni sh 2000-max3000,na wakati ulezi ni min1800-max1900..Sasa Ukiona mama kakuchanganyia na mchele ujue wewe ndio mnyonyaji........ila inaonekana wewe ni mpenzi wa uji wa ulezi.
 
Back
Top Bottom