Suluhisho la mikopo umiza:Raisi Samia, unda Chombo au Taasisi maalumu itayohusika kusimamia na kudhibiti biashara ya kukopesha fedha

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,129
144,626
Tatizo la.mikopo umiza maarifu kama "kausha damu", linazidi kushika kasi hapa nchini huku Benki Kuu yenye dhamana ya kusimamia na kuendesha hii biashara, ilionekana kushindwa kabisa kudhibiti uholela wa hii biashara japo teyar kuna sheria na Kanuni za kusimamia uendeshaji wa hii biashara..

Binafsi, naona Benki Kuu hawako serious kabisa kusimamia sheria husika na hii inawzekana ni kwasbabu kwao hii si shughuli muhimu kama zilivyo shughuli nyingine na ndio maana hii biashara inaendelea kufanywa kiholela kama hakuna kabisa sheria.

Benki Kuu imekosa ubunifu katika kusimamia hii sheria ndio maana hata taasisi zinazofanya hii biashara kihallali (zenye leseni) zinakiuka sheria na hata mashariti ya leseni wanazopewa na Benki Kuu.

Mfano wa wazi ni taasisi hizi kukaa na kad za benki za wateja wao bila hofu kabisa jambo ambalo n8 kinyume na sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 na Kanuni zake za mwaka 2019.

Ukiacha hilo, watu binafs wasiokuwa na leseni kufanya hii biashara na hata kupeleka wateja wao polisi huku wao wenyewe wakiwa ni wahalifu wanaofanya hio biashara pasipokuwa na leseni.

Kasoro zingine ni kama uholela wa kutoza riba, unyanyasaji, udhalilishaji, na mambo mengine yaliyo kinyume kabisa na sheria

Suluhisho:
Nafikiri wakati umefika serikali kuunda chomno au taasisi maalumu itayo-deal na hii biashara kwa maana ya Benki Kuu kunyang'anywa hilo jukumu na kukabidhiwa kwa taasisi au chombo kingine.

Tukiwa na chombo au taasisi maalumu kusimamia na kudhibiti hii biashara, umaskini, usimamizi na ufuatliaji ws hii sheria utaonekana kwani hilo ndio litakuwa jukumu la kubwa tofauti na ilivyo sasa chini ya Benki Kuu ambayo teyari ina majukumu mengine mengi.

Mikopo kausha damu inarudisha nyuma maendeleo ya watu, inatia umaskini, inavunja kama sio kuvuruga ndoa za watu, kusababisha vifa(watu kujiua) n.k

Kwa kifupi, madhara ni mengi na bila shaka ndio maana hata serikali ilikuja na hiyo sheria mwaka 2018. Hivyo, ni wakati sahihi wa kupata chombo au taasisi maalumu ya kusimamia hiyo sheria kwa vitendo. Benki Kuu huenda majukumu yamewazidi au tu hawako serious.
 
Lipa mara moja, mara unapokopa, kitolipa kunaathiri wakopaji wengine wenye mahitaji ya kifedha.
 
Back
Top Bottom