BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,441
- 8,261
Kufuatia video inayosambaa mtandaoni ikionesha Mtu akipatiwa adhabu ya kugalagala chini pamoja na kuruka kichura baada ya kukaidi kulipa ushuru wa halmashauri kwa watumishi wanaohusika na ukusanyaji wa ushuru katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Mkuu wa wilaya ya Kahama @mboni_mhita ametoa ufafanuzi wa tukio hilo
Tukio hilo lilitokea Mei 2, 2024 likiwahusisha watumishi watano wa halmashauri hiyo kutoa adhabu kwa mwananchi aliyekaidi kulipa ushuru.
Wasafi Media imemtafuta Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kupata ufafanuzi wa suala hilo ambapo amekiri uwepo wa tukio hilo pamoja hatua walizochukuwa kwa watumishi hao waliojihusisha na kutoa adhabu hiyo na kusema kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.