SoC03 Serikali ifanye haya kuimarisha Utawala bora na Uwajibikaji katika Sekta ya Afya

Stories of Change - 2023 Competition

siscam

New Member
Jun 23, 2023
1
0
Afya ya msingi(PHC)
Upatikanaji wa huduma ya afya na mipango ya afya ya msingi katika ngazi ya jamii, Zahanati,na vituo vya afya ni changamoto ngumu sana katika nchi zinazoendelea. Utawala Bora katika afya ya msingi ni jambo muhimu sana ambalo serikali imesahau kuwekea kipaumbele.

Hii inahusisha Upatikanaji wa maafisa afya ya jamii pamoja na mazingira, wanasaikolojia,na watoa ushauri katika ngazi ya kijiji. Magonjwa mengi yanaweza kuzuiwa kirahisi kwa kutoa elimu bila kutibu mfano, Elimu kuhusu afya ya akili, Elimu ya afya ya ngono na uzazi, uchimbaji wa vyoo na mashimo ya takataka, umuhimu wa lishe na vyakula Bora, Upatikanaji wa chanjo, usambazaji wa kondomu, hii inasaidia sana afya ya jamii nakurefusha maisha ya uma.

Utafiti na uchunguzi
Wizara ya afya ijikite zaidi katika utafiti wa magonjwa mbalimbali sambamba na kuweka bajeti nzuri katika utafiti.Kukusanya na kuchambua data kwa jamiiili kutathmini Hali ya afya ya jamii.Tathmini ya Hali ya afya kwa idadi ya watu na uchumi wa jamii, mazingira, Hali ya afya ya watu, Upatikanaji wa raslimali na wataalam ili kutafiti Upatikanaji wa afya Bora kwa jamii.

Rushwa
Rushwa ni adui wa haki.Uwazi katika kutoa Huduma ya afya sambamba na kuwepo kwa tekinologia nzuri inayoweka mifumo yote ya utoaji Huduma kwa njia ya kisasa zaidi itapunguza mianya ya rushwa na Huduma za afya zitakua Bora zaidi.Elimu itolewe ya uzalendo wa nchi kuanzia ngazi ya shule ya msingi ili kila mtu ajifunze kumthamini binadamu mwenzie na kumtunza Mali za uma.

Elimu
Serikali ihakikishe Huduma ya elimu ya msingi inatolewa kwa jamii kama kufanya mazoezi,namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo.Hii itatusaidia kupunguza wimbi kubwa la ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza kama Kansa,kisukari,magonjwa ya moyo,magonjwa ya akili,magonjwa ya mifumo ya fahamu,magonjwa ya figo na

Shinikizo la damu
Ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza yanaathiri sana ukuaji wa uchumi kwa kua yanatumia gharama kubwa.

Wizara na wadau wa afya waweke wazi malengo na namna ya uboreshaji wa Huduma za afya.Runinga na redio zitumike kufikisha ujumbe kwa jamii sambamba na kutoa tamthilia na nyimbo (muziki)zinazotoa elimu ya afya na uwajibikaji kama tamthilia ya ZAHANATI YA KIJIJI.
 
Back
Top Bottom