Ripoti ya LHRC na ZAFAYCO: Ukatili dhidi ya Wenza umeongeza sababu ikiripotiwa kuwa "Wivu wa Mapenzi"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,851
12,088
Snapinsta.app_437516516_18321069856133657_7891081056491284815_n_1080.jpg
LHRC wakishirikiana na Zanzibar Fighting Against Youth Challenges Organization (ZAFAYCO) wanazindua ripoti ya Haki za binadamu 2023.

Ripoti inatazamia kuonesha hali ya Haki za Binadamu Zanzibar na Tanzania Bara kwa mwaka 2023.

Ripoti hii ni ya 22 kutolewa na LHRC tangu 2002.



Ripoti ya Haki za Binadamu ya Tanzania ya Mwaka wa 2023 ni ripoti ya 22 ya LHRC, ikionyesha hali ya haki za binadamu nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara na Zanzibar.

Ripoti hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano na Shirika la Kupambana na Changamoto za Vijana Zanzibar (ZAFAYCO).

Inagusa baadhi ya masuala muhimu kuhusu vizazi vitatu vya haki za binadamu, yaani: haki za kiraia na kisiasa; haki za kiuchumi, kijamii, na kitamaduni; na haki za kikundi.

Baadhi ya vipengele vipya katika ripoti ni pamoja na matokeo na mapendekezo ya ripoti ya Tume ya Rais kuhusu Mageuzi ya Sheria ya Jinai, masuala yanayohusiana na faragha, masuala ya uwajibikaji, na haki za watoto.

Kaulimbiu ya toleo la mwaka wa 2023 la ripoti ni "KATIBA, UWAJIBIKAJI, NA ULINZI WA HAKI," ikizingatia wasiwasi juu ya ukosefu wa uwajibikaji uliotolewa na wadau mbalimbali mwaka wa 2023.

Ripoti hiyo inaonyesha pande zote chanya na hasi zilizotokea katika mwaka wa 2023 na ni matokeo ya tathmini za LHRC na ZAFAYCO za masuala muhimu na utekelezaji wa Tanzania wa majukumu yake ya haki za binadamu, uliofanywa kwa kutumia viwango vya kimataifa, kikanda, na kitaifa vya haki za binadamu kama kigezo.

Ripoti imegawanyika katika sura 7

---
Muhtasari wa Ripoti

Haki ambazo zilioneshwa kukiukwa zaidi mwaka 2023
  • haki ya kuwa huru na salama
  • Haki ya Kuishi
  • Haki ya uhuru dhidi ya ukatili
  • Haki ya usawa mbele ya sheria
  • uhuru dhidi ya utesaji

Haki zote hizi zinaangukia katika kizazi cha haki za kiraia na haki za kisiasa na ukikwaji wake ulichangiwa na mambo mbalimbali ikiwemo mauaji na wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Mauaji yanayotokana na imani za kishirikina, mauaji ya wenza, vikwazo vya upatikanaji wa haki na changamoto mbalimbali zinazotokana na mfumo wa haki jinai ikiwemo uwekaji wa watuhumiwa kizuizini na kwa muda mrefu, pia ukamataji na uwekwaji kizuizini kinyume na sheria, uchunguzi wa kesi kuchukua muda mrefu na ubambikwaji wa kesi.

Ripoti hii imeonesha kuwa

  • Watoto wameendelea kuwa manusura wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu 45%, asilimia imepungua kulinganisha na mwaka jana 47%.
  • Kwa wanawake ni 30% kutoka 33%
  • Wazee 12% kutoka 10%
  • Wanaume 10% kutoka 6%
  • Wenye ulemau 3% kutoka 4%

Matukio ya wananchi kujichukuliwa sheria mkononi yameendelea kuwa mwiba kwa haki ya kuishi ambapo mwaka huu LHRC imekusanya matukio 42 mawili zaidi kulinganisha 2022. Matukio ya aina hii yanayokusanywa na jeshi la polisi ni zaidi ya 400 kila mwaka tokea 2022

Matukio yanayotokana na imani ya kishirikina yameendelea kuwa changamoto katika jamii japo yamekuwa yakiendeleka kupungua hivi miaka ya karibuni. Hali kadhalika hakukuwa na mashambulizi yoyote ya watu wenye ualbino 2023.

Aina nyingine iliyoathiri haki ya kuishi na ukatili dhidi ya wenza. 2023 LHRC ilikusanya matukio 50 ambayo ni ongezeko la matukio 17 kulinganisha na mwaka 2022. Wanawake wameendelea kuwa wengi kwenye ukatili huu dhidi ya wenza ikiwa ni asilimia 90 wakiwa wamefanyiwa ukatili na kuuawa. Matukio mengi yakiripotiwa kutokana na wivu wa mapenzi.

Kuhusu uhuru wa Kujieleza
Mwaka 2023 tulikuwa na marekebisho ya sheria ya huduma za habari ya 2016 ambayo wadau walikuwa wakiihitaji. Pamoja na sheria hiyo kuleta vifungu chanya, sheria hiyo pia imeleta vifungu ambavyo vinaminya uhuru wa kujieleza. Hali kadhalika bado kuna sheria nyingine kama kanuni za maudhui ya mtandao bado ina vifungu vyenye utata.

Uhuru wa kujumuika na kukusanyika
Tunaishukuru Serikali kwa kuondoa katazo la mikutano ya siasa ya hadhara mwanzoni 2023, lakini pia kuna haja ya kufanyia marekebisho ya sheria zinzohusu haki hizi ikiwemo sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi ili kuziimarisha zaidi haki hizi.

Zaidi soma ripoti hapa....
 

Attachments

  • Tanzania Human Rights Report 2023.pdf
    13.4 MB · Views: 2
Back
Top Bottom