Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,854
- 12,090
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kihutubia Taifa kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Pamoja na mambo mengine, Rais Samia amesema mojawapo ya sababu zinazofanya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar udumu ni uwepo wa tume ya pamoja chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais inayosikiliza na kutatua kero za Muungano kila zinazojitokeza.
Aidha, katika diplomasia, Muungano umeiongezea Tanzania sifa ya ushawishi mkubwa kikanda na kimataifa. Wakati nchi hizi zinaungana zilikuwa kwenye kiwango duni cha maendeleo na wananchi wengi walikuwa katika hali ya kimaskini pamoja na kukuza pato la taifa kufikia trilioni 170 kwa takwimu za mwaka 2022 na pato la mtu mmoja mmoja kufikia wastani wa Milioni 2.8 na sasa Tanzania imefikia uchumi wa kati ngazi ya Chini.
Wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania umeongezeka kutoka miaka 45 mwaka 1964 hadi wastani wa miaka 67 mwaka 2024, sensa ya kwanza ilionesha uwepo wa watu Milioni 9 na sensa ya mwisho ya mwaka 2022 ilionesha uwepo wa watanzania 61 karibu 62.
Katika mwaka 2021 hadi sasa, hoja 15 kati ya 18 zimeshapatiwa ufumbuzi.Aidha, katika diplomasia, Muungano umeiongezea Tanzania sifa ya ushawishi mkubwa kikanda na kimataifa. Wakati nchi hizi zinaungana zilikuwa kwenye kiwango duni cha maendeleo na wananchi wengi walikuwa katika hali ya kimaskini pamoja na kukuza pato la taifa kufikia trilioni 170 kwa takwimu za mwaka 2022 na pato la mtu mmoja mmoja kufikia wastani wa Milioni 2.8 na sasa Tanzania imefikia uchumi wa kati ngazi ya Chini.
Wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania umeongezeka kutoka miaka 45 mwaka 1964 hadi wastani wa miaka 67 mwaka 2024, sensa ya kwanza ilionesha uwepo wa watu Milioni 9 na sensa ya mwisho ya mwaka 2022 ilionesha uwepo wa watanzania 61 karibu 62.
Kabla ya muungano kulikuwa na chuo kikuu kimoja, kwa sasa kuna vyuo vikuu 49 ambapo 30 kati yake ni binafsi, 46 vipo Tanzania bara na 3 Zanzibar.