KWELI Posho za wasimamizi wa mtihani wa Kidato cha nne hutofautiana kulingana na idadi ya siku walizosimamia

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Baadhi ya Halmashauri zimedaiwa 'kuwapiga' cha juu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.

Kwa utafiti wangu usio rasmi wa kuwapigia watumishi wa Halmashauri tofauti tofauti, nimegundua kwamba kuna Halmashauri zingine zimewalipa wasimamizi siku 19, zingine zikalipa siku 14 na zingine zikalipa kwa siku msimamizi atakazoingia darasani kusimamia. Kwa mfano, kama shule ina mchepuo wa sanaa pekee na ratiba ni siku tano au saba basi wamelipwa kwa siku hizo.

Kwanini siku za malipo zitofautiane? Malipo hayo yamegharamiwa na NECTA au kila halmashauri inalipa kulingana na uwezo wake?

1657973158063.png
 
Tunachokijua
JamiiForums imefuatilia madai haya na kubaini kuwa wasimamizi wa mitihani wanalipwa na TAMISEMI, hao wasimamizi huchaguliwa na TAMISEMI. Malipo yote huwa kiwango sawa kwa kuwa yanafanyika kwa kipindi kimoja.

Wasimamizi hulipwa kulingana na siku wanazosimamia mitihani. Mfano anayesimamia kwa siki 5 atalipwa malipo ya siku 5, anayesimamia kwa siku 10 atalipwa malipo ya siku 10.

Aidha, TAMISEMI ina jukumu la kuchagua wasimamizi wa mitihani ya kidato cha nne na huwalipa kiwango sawa ila kulingana na idadi ya siku walizosimamia.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom