Ndata
JF-Expert Member
- Mar 2, 2017
- 226
- 321
MBWEMBWE ZA MAALIM MWISHO OCTOBER
Wanasiasa wote wenye historia Safi ya kushindwa huwa na ushamba Fulani hivi wa kushabikia nyomi la watu.
Kuthibitisha hili taenda na mifano hai kabisa tena nitacheza na mifano ya juzi juzi sio ya mbali Sana.
Uchaguzi wa mwaka 2015 Mh Lowasa alikusanya nyomi, watu walideki lami ila alipigika kirahisi tuu na mwisho wa siku alikubali matokeo.
Mwaka 2016 Kiza Besigye Uganda alikusanya nyomi Kila mtu akajua mwisho wa M7 umefika. Baada ya matokeo kutangazwa akajipatia asilimia zake 30+ akatulia.
Mwaka 2017 Raila Odinga alidanganywa na nyomi akapinga matokeo uchaguzi ukarudiwa ila aliweka mpira kwapani akakimbia uwanja.
Hii ndio nyomi anayojisia Maalim ambapo baada ya Kuzoom vizuri nimewaona watoto wa Kigoma wengi ambao sio wapiga kura Zanzibar. Halafu anajisifia nyomi.
Mwenzake Membe anaogopa hata kuandaa mapokezi huku bara, maana Kuna uwezekano akapokewa na mkewe au hata mkewe akaikwepa aibu.
Mwisho wa yote ujumbe huu umfikie Maalim, Kama hadi anazeeka haelewi tofauti ya wapiga kura na nyomi la wahuni basi astaafu siasa tuu akalee wajukuu.
Pichani Kaliyango diwani Kigoma mjini na Monalisa mtoto wa Shirika Kigoma.