SoC03 Nitunze zaidi, niishi zaidi na upate zaidi

Stories of Change - 2023 Competition

Tonytz

Senior Member
Jul 18, 2022
159
1,142
Kwanza nianze kwa kuipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa inayoendelea kuzichukua katika kutunza na kulinda mazingira yetu na vyanzo mbalimbali vya asili ambapo kama nchi tumebarikiwa kuwa navyo.

Ni wazi kuwa mazingira yanayozunguka nchi yetu yamejaliwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya asili ikiwemo mito, misitu, Wanyama pori, madini, na ardhi yenye rutuba tele. Vyanzo hivi vyote vya asili ni muhimu sana kutunzwa na kulindwa kwa mustakabali wa Maisha yetu hasa kimaendeleo.

Katika andiko hili nitajikita kuelezea mambo makuu matatu;

Kwanza shughuli zinazoathiri mazingira yetu na vyanzo mbalimbali vya asili,

Pili sababu za kwanini Watanzania wanashindwa kutekeleza sera za utunzaji wa mazingira (sera ya mazingira ya Taifa yam waka 1997 na sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004), na mwisho nini kifanyike ili kuongeza uwajibikaji katika kutunza na kulinda mazingira yetu.

SHUGHULI ZINAZOATHIRI MAZINGIRA YETU NA VYANZO VYA ASILI VILIVYOMO

Baadhi ya shughuli hizo za kibinadamu zinazoharibu mazingira na vyanzo vyetu vya asili ni pamoja na;

Kwanza, ukataji wa miti holela pasipo kufata taratibu na sharia elekezi katika uvunaji wa miti wenye tija. Watu wengi hujikita katika ukataji miti kinyume na sheria ili kuchoma mkaa, kujipatia maeneo ya makazi au kusafisha mashamba. Halii huathiri mazingira yetu kwani hupelekea mabadiliko ya Tabianchi.

Pili, ufugaji holela, ufugaji ni sehemu ya Maisha yetu Watanzania wengi. Kuna baadhi ya jamii za kitanzania zimejikita katika ufugaji hasa za kanda ya ziwa na mikoa ya kati ya Tanzania (Singida, Dodoma n.k). shughuli hizi zimekuwa zikifanywa kiholela sana kiasi cha kuharibu mazingira yetu na vyanzo mbalimbali vya asili vinavyopatikana maeneo yetu.

Tatu, ujengwaji holela wa viwanda bubu na nyumba za makazi. Viwanda bubu hapa namaanisha viwanda visivyorasimishwa au kukosa kibali. Hii haimaanishi kuwa viwanda vyenye kibali haiviathiri, la hasha. Viwanda hivi huathiri mazingira kutokana na kuzalisha moshi wenye sumu, kutiririsha maji yenye sumu kwenye udongo na vyanzo vya maji ambapo huathiri watumiaje wa vyanzo hivyo.

Nne, shughuli nyinginezo ni uwindaji haramu, uvuvi haramu,mbinu mbaya za kilimo kama vile matumizi makubwa ya mbolea za kemikali, mifumo ya elimu, umasikini na uchomaji moto misitu.

KWANINI WATANZANIA WANASHINDWA KUTEKELEZA SERA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA?

Katika sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021 kumeainishwa kazi na majukumu ya kiutekelezwaji kwa wizara husika ya mazingira(BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA).

Baraza hili liliundwa kwa sheria ya Taifa ya usimamizi wa mazingira yam waka 1983 na 2004 ikiwa na dhumuni kuwa kiwe chombo cha kuishauri serikali juu ya masuala ya utunzaji endelevu wa mazingira nchini kwetu.

Pamoja na uwepo wa sera hizo na Baraza hilo,lakini kumekuwa na kutotekelezeka kwa sera hizo kwa kiwango kile kilichotarajiwa kama ilivyoorodheshwa kwenye sera ya mwaka 1997. Kuna mambo mengi yanayopelekea kutotekelezwa kwa sera hizi. Hapa nitaeleza machache tu.

Kwanza, kukosekana kwa uwajibikaji kwa waliopewa dhamana ya kusimamia mazingira. kwani baadhi ya viongozi wetu wamekosa uzalendo na uadirifu katika utendaji kwani sasa kuna wimbi la kufanya kazi kimaandishi Zaidi na siyo kufika maeneo ya tukio na kutenda.

Pili
, jamii kubwa ya Watanzania hawana uelewa mkubwa juu ya sera ya usimamizi na utunzaji wa mazingira.

Tatu, kukosekana kwa mipango endelevu ya utumizi sahihi wa vyanzo vya asili, hivyo vyanzo hivi hutumika kimazoea na kupelekea kuharibika au kupungua.

Nne, kukosekana au ushirikishwaji hafifu kwa taasisi na mashirika binafsi zinazojihusisha na utunzaji wa mazingira pamoja na wadau wengine wa mazingira ikiwemo watu binafsi wa mazingira katika kutekeleza sera, mikakati, mipango na miradi ambayo malengo ya sera yangetekelezwa.

Tano, kukithiri kwa vitendo vya rushwa ambapo kwa namna moja au nyingine huathiri uwajibikaji na utekelezaji wa sera hizo.

Sita, umasikini kwa kundi Fulani la watanzania. Hayo na mengine mengi kama vile ukuaji wa sayansi na teknolojia unaothiri utekelezaji hukwamisha utekelezwaji wa sera.

MAMBO YATAKAYOONGEZA UWAJIBIKAJI KATIKA UTUNZAJI NA KULINDA MAZINGIRA PAMOJA NA UTEKELEZAJI WA SERA YA TAIFA YA KULINDA NA KUSIMAMIA MAZINGIRA.

Kila mtanzania anapaswa kuwajibika katika kutekeleza sera, mipango, mikakati na miradi inayohusu kutunza na kulinda mazingira. Baadhi ya mambo yatakayoweza kuchochea uwajibikaji,

Kwanza kubuni na kupanua wigo wa namna ya kutoa elimu kwa watanzania wote, hii inaenda sambamba na kufanya somo la mazingira na vyanzo vya asili ndani ya Taifa letu kuwa somo linalojitegemea kuanzia shule za msingi. Pia kuwa na mikutano maalumu katika vijiji na vitongoji vinavyoelezea juu ya sera ya Taifa ya mazingira kuwa ni nini na inataka nini na utekelezwaji wake. Hii itasaidia kuongeza idadi kubwa ya watanzania katika kujua na kutambua njia sahihi za utunzaji mazingira.

Pili, serikali kuwa na ushirikishi endelevu kwa raia wake juu ya mipango, mikakati na miradi ya utunzaji wa mazingira. Hii itasaidia kuepukana na migogoro katika utelezwaji wa sera na mikakati yake.

Tatu,
kuwepo na mabalozi wa mazingira wenye kuzingatiwa na kuwezeshwa katika ngazi za vijiji, kata na shule. Hapa naomba ifahamike kuwa pengine watu hawa wapo lakini hawawajibiki kwa kuwa hakuna uzingativu juu yao. Kuwepo na maslahi kidogo kwao yatakayowaongezea hari ya utendaji.

Nne, natambua sehemu nyingi za vijijini kuna kamati za mazingira, lakini kamati hizi zimejaa ubinafsi, rushwa na kutishia amani kwa watu, hivyo wizara husika iwe na desturi ya kufatilia na kuwauliza wanakijiji katika mwenendo wa utekelezaji wao.

Tano, serikali iongeze ushirikishwaji Zaidi kwa taasisi, mashirika binafsi na wadau mbalimbali wa mazingira katika utekelezaji wa sera, mikakati, mipango na miradi yenye kutekelezeka ya kimazingira.

Sita, serikali kuongeza juhudi za kutafuta mipango mikakati endelevu ya kusaidia kuondoa umasikini kwa watu wake ili kuwafanya wapunguze utegemezi kwenye vyanzo vya asili kama vile ukataji miti na uvuvi haramu. Hapa naishauri serikali kutafuta nyanzo mbalimbali vya ajira kwa watu wake.

Saba, serikali kutoa uhuru chanya kwa vyombo vya habari na wanahabari katika jitihada zao katika utekelezwaji wa sera, mipango, mikakati na miradi ya kimazingira kwani wao ni kioo cha jamii na huwafikia wengi.

Mwisho, serikali kusimamia misingi ya utawala bora katika utekelezaji na usimamizi wa sera Taifa ya kusimamia na kutunza mazingira
. Mambo haya yasifanyike kwa kukurupuka au kwa mihemko ya kiongozi mmoja mmoja na badala yake iwe ni sauti ya umma yenye tija na manufaa kwa Taifa letu.
 
Kwanza nianze kwa kuipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa inayoendelea kuzichukua katika kutunza na kulinda mazingira yetu na vyanzo mbalimbali vya asili ambapo kama nchi tumebarikiwa kuwa navyo.

Ni wazi kuwa mazingira yanayozunguka nchi yetu yamejaliwa kuwa na vyanzo mbalimbali vya asili ikiwemo mito, misitu, Wanyama pori, madini, na ardhi yenye rutuba tele. Vyanzo hivi vyote vya asili ni muhimu sana kutunzwa na kulindwa kwa mustakabali wa Maisha yetu hasa kimaendeleo.

Katika andiko hili nitajikita kuelezea mambo makuu matatu;

Kwanza shughuli zinazoathiri mazingira yetu na vyanzo mbalimbali vya asili,

Pili sababu za kwanini Watanzania wanashindwa kutekeleza sera za utunzaji wa mazingira (sera ya mazingira ya Taifa yam waka 1997 na sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004), na mwisho nini kifanyike ili kuongeza uwajibikaji katika kutunza na kulinda mazingira yetu.

SHUGHULI ZINAZOATHIRI MAZINGIRA YETU NA VYANZO VYA ASILI VILIVYOMO

Baadhi ya shughuli hizo za kibinadamu zinazoharibu mazingira na vyanzo vyetu vya asili ni pamoja na;

Kwanza, ukataji wa miti holela pasipo kufata taratibu na sharia elekezi katika uvunaji wa miti wenye tija. Watu wengi hujikita katika ukataji miti kinyume na sheria ili kuchoma mkaa, kujipatia maeneo ya makazi au kusafisha mashamba. Halii huathiri mazingira yetu kwani hupelekea mabadiliko ya Tabianchi.

Pili, ufugaji holela, ufugaji ni sehemu ya Maisha yetu Watanzania wengi. Kuna baadhi ya jamii za kitanzania zimejikita katika ufugaji hasa za kanda ya ziwa na mikoa ya kati ya Tanzania (Singida, Dodoma n.k). shughuli hizi zimekuwa zikifanywa kiholela sana kiasi cha kuharibu mazingira yetu na vyanzo mbalimbali vya asili vinavyopatikana maeneo yetu.

Tatu, ujengwaji holela wa viwanda bubu na nyumba za makazi. Viwanda bubu hapa namaanisha viwanda visivyorasimishwa au kukosa kibali. Hii haimaanishi kuwa viwanda vyenye kibali haiviathiri, la hasha. Viwanda hivi huathiri mazingira kutokana na kuzalisha moshi wenye sumu, kutiririsha maji yenye sumu kwenye udongo na vyanzo vya maji ambapo huathiri watumiaje wa vyanzo hivyo.

Nne, shughuli nyinginezo ni uwindaji haramu, uvuvi haramu,mbinu mbaya za kilimo kama vile matumizi makubwa ya mbolea za kemikali, mifumo ya elimu, umasikini na uchomaji moto misitu.

KWANINI WATANZANIA WANASHINDWA KUTEKELEZA SERA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA?

Katika sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021 kumeainishwa kazi na majukumu ya kiutekelezwaji kwa wizara husika ya mazingira(BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA).

Baraza hili liliundwa kwa sheria ya Taifa ya usimamizi wa mazingira yam waka 1983 na 2004 ikiwa na dhumuni kuwa kiwe chombo cha kuishauri serikali juu ya masuala ya utunzaji endelevu wa mazingira nchini kwetu.

Pamoja na uwepo wa sera hizo na Baraza hilo,lakini kumekuwa na kutotekelezeka kwa sera hizo kwa kiwango kile kilichotarajiwa kama ilivyoorodheshwa kwenye sera ya mwaka 1997. Kuna mambo mengi yanayopelekea kutotekelezwa kwa sera hizi. Hapa nitaeleza machache tu.

Kwanza, kukosekana kwa uwajibikaji kwa waliopewa dhamana ya kusimamia mazingira. Hii inaweza kukionesha wazi kuwa baadhi ya viongozi wetu wamekosa uzalendo na uadirifu katika utendaji kwani sasa kuna wimbi la kufanya kazi kimaandishi Zaidi na siyo kufika maeneo ya tukio na kutenda.

Pili
, jamii kubwa ya Watanzania hawana uelewa mkubwa juu ya sera ya usimamizi na utunzaji wa mazingira.

Tatu, kukosekana kwa mipango endelevu ya utumizi sahihi wa vyanzo vya asili, hivyo vyanzo hivi hutumika kimazoea na kupelekea kuharibika au kupungua.

Nne, kukosekana au ushirikishwaji hafifu kwa taasisi na mashirika binafsi zinazojihusisha na utunzaji wa mazingira pamoja na wadau wengine wa mazingira ikiwemo watu binafsi wa mazingira katika kutekeleza sera, mikakati, mipango na miradi ambayo malengo ya sera yangetekelezwa.

Tano, kukithiri kwa vitendo vya rushwa ambapo kwa namna moja au nyingine huathiri uwajibikaji na utekelezaji wa sera hizo.

Sita, umasikini kwa kundi Fulani la watanzania. Hayo na mengine mengi kama vile ukuaji wa sayansi na teknolojia unaothiri utekelezaji hukwamisha utekelezwaji wa sera.

MAMBO YATAKAYOONGEZA UWAJIBIKAJI KATIKA UTUNZAJI NA KULINDA MAZINGIRA PAMOJA NA UTEKELEZAJI WA SERA YA TAIFA YA KULINDA NA KUSIMAMIA MAZINGIRA.

Kila mtanzania anapaswa kuwajibika katika kutekeleza sera, mipango, mikakati na miradi inayohusu kutunza na kulinda mazingira. Baadhi ya mambo yatakayoweza kuchochea uwajibikaji,

Kwanza kubuni na kupanua wigo wa namna ya kutoa elimu kwa watanzania wote, hii inaenda sambamba na kufanya somo la mazingira na vyanzo vya asili ndani ya Taifa letu kuwa somo linalojitegemea kuanzia shule za msingi. Pia kuwa na mikutano maalumu katika vijiji na vitongoji vinavyoelezea juu ya sera ya Taifa ya mazingira kuwa ni nini na inataka nini na utekelezwaji wake. Hii itasaidia kuongeza idadi kubwa ya watanzania katika kujua na kutambua njia sahihi za utunzaji mazingira.

Pili, serikali kuwa na ushirikishi endelevu kwa raia wake juu ya mipango, mikakati na miradi ya utunzaji wa mazingira. Hii itasaidia kuepukana na migogoro katika utelezwaji wa sera na mikakati yake.

Tatu,
kuwepo na mabalozi wa mazingira wenye kuzingatiwa na kuwezeshwa katika ngazi za vijiji, kata na shule. Hapa naomba ifahamike kuwa pengine watu hawa wapo lakini hawawajibiki kwa kuwa hakuna uzingativu juu yao. Kuwepo na maslahi kidogo kwao yatakayowaongezea hari ya utendaji.

Nne, natambua sehemu nyingi za vijijini hasa huku kijijini kwetu kuna kamati za mazingira, lakini kamati hizi zimejaa ubinafsi, rushwa na kutishia amani kwa watu, hivyo wizara husika iwe na desturi ya kufatilia na kuwauliza wanakijiji katika mwenendo wa utekelezaji wao.

Tano, serikali iongeze ushirikishwaji Zaidi kwa taasisi, mashirika binafsi na wadau mbalimbali wa mazingira katika utekelezaji wa sera, mikakati, mipango na miradi yenye kutekelezeka ya kimazingira.

Sita, serikali kuongeza juhudi za kutafuta mipango mikakati endelevu ya kusaidia kuondoa umasikini kwa watu wake ili kuwafanya wapunguze utegemezi kwenye vyanzo vya asili kama vile ukataji miti na uvuvi haramu. Hapa naishauri serikali kutafuta nyanzo mbalimbali vya ajira kwa watu wake.

Saba, serikali kutoa uhuru chanya kwa vyombo vya habari na wanahabari katika jitihada zao katika utekelezwaji wa sera, mipango, mikakati na miradi ya kimazingira kwani wao ni kioo cha jamii na huwafikia wengi.

Mwisho serikali kusimamia misingi ya utawala bora katika utekelezaji na usimamizi wa sera Taifa ya kusimamia na kutunza mazingira
.

Mambo haya yasifanyike kwa kukurupuka ua kwa mihemko ya kiongozi mmoja mmoja na badala yake iwe ni sauti ya umma yenye tija na manufaa kwa Taifa letu.
Bandiko qonki sana .....liwekewe lamination
 
Back
Top Bottom