Ni kwa namna gani teknolojia imeathiri biashara ya maduka ya viandikia (Stationery)

Apr 24, 2024
9
7
Muda mrefu duniani imekuwa ikipita mabadiliko makubwa ya teknolojia kutoka mapinduzi ya mwanzo ya viwanda mpaka sasa kuelekea mapinduzi mapya ya viwanda ambayo yanaelekea kuja na taswira mpya na aina mpya ya uwekezaji hususani kwa sasa teknolojia inayozungumzwa ni teknolojia ya akili bandia ( artificial intelligence), mabadiliko hayo yamekuwa yakija na athari mbalimbali katika maisha ya kila siku huku yakiwa yamegawanyika katika sehemu mbili (2) ambazo ni athari chanya(positive impact) na athari hasi (negative impact).

Kwa upande wa athari chanya mabadiliko ya teknolojia yamekuwa ya kurahisisha uchakataji wa taarifa na mambo mengine mbalimbali huku kwa upande wa athari hasi mabadiliko haya ya teknolojia yamekuwa na athari mbalimbali kwa baadhi ya watu na baadhi ya biashara zimeanza kuwa na uzorotaji wa baadhi ya biashara, leo nimeleta makala kuhusiana na kuanza kufifia kwa biashara ya maduka ya viandikia au kama ilivyozoeleka stationary .

Kwa kipindi cha miaka ya nyuma biashara ya maduka ya viandikia yalikuwa ni maduka muhimu sana kwa pande hususani katika eneo la utoaji wa nakala, huduma ya kuscan vitu, huduma ya internet na mambo mbalimbali , katika ukuaji huu mpya wa teknolojia biashara hii imeanza kukosa soko hususani kwa upande wa wawekezaji wa maduka hayo.

Kipindi cha nyuma maduka hayo yalikuwa muhimu kwani watu walilazimika kutumia maeneo hayo kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali mfano wa shughuli hizo ni hizi zifuatazo, TYPING, miaka ya nyuma watu walilazimika kwenda kwa wingi katika maduka hayo ya viandikia kwa ajili ya kufanya taratibu za uandikaji uliokuwa na uhitaji wa kitarakilishi (kompyuta) katika uandishi wa vitu mbalimbali kwa hiyo ili kuwa ni biashara kwa watu hawa waliowekeza katika biashara hiyo ili kuwa inaingiza faida kwao kwani walilazimika kuwatoza wa fedha ili waweze kupewa huduma hiyo kwa urahisi hivyo ili ni chanzo cha kuendeleza biashara yao na kuingiza faida.

ila hali imeanza kubadilika kwa sasa teknolojia imekuwa tunaona kupitia simu za mkononi hususani simu janja zimekuwa na application mbalimbali kwa ajili ya kuandika vitu ambavyo unavihitaji kuviandika hivyo kupunguza gharama za fedha , ambayo pia inapelekea kupungua kwa kipato cha wawekezaji wa maduka ya viandikia.

Utoaji wa Nakala (copy), ukuaji wa teknolojia umeenda kupunguza matumizi ya makaratasi kwa office nyingi za umma kuanzia serikalini mbaka sekta binafsi kwani tunaona katika mapinduzi haya ya teknolojia watu wamelazimika kuhama kutoka kwenye mfumo wa matumizi ya documents kwa njia ya karatasi na kuelekea katika njia mpya ya uandaaji wa documents na uwasilishaji kwa njia inayojulikana kama Paper less njia inahusisha zaidi barua pepe katika uwasilishaji wa taarifa mbalimbali ambayo ni salama kwa ajili ya siri za ofisi na kampuni kwani zamani kama ulikuwa unalazimika kutoa nakala kulikuwa na uwezekano mkubwa wa baadhi ya siri za ofisi na kampuni kuvuja kwa watu ambao si sahihi ,hii pia inapelekea kupungua kwa nguvu ya maduka ya viandikia.

Kufanya udahili wa vitu mbalimbali, kwa miaka ya nyuma maduka ya viandikia yalikuwa yakitoa huduma ya kufanya udahili wa vitu mbalimbali kwa waliokuwa na uhitaji wa mambo hayo mfano watu waliokuwa wanahitaji udahili wa vyuo vikuu kwa ndani au nje ya nchi, watu waliokuwa wanahitaji kuomba ajira ndani na nje ya nchi kwa kampuni zilizokuwa zinatumia mfumo wa barua pepe au pia kwa baadhi ya sekta binafsi hii ilikuwa inaingiza kipato kikubwa sekta hiyo kwani walikuwa wakiwatoza kiwango fulani cha fedha ili waweze kupewa huduma hiyo mfano kwa miaka ya nyuma ilikuwa inatozwa shilingi elfu 3 mbaka elfu 10 shilingi za Tanzania kwa ajili ya kufanya udahili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati

Mabadiliko ya teknolojia yamerahisisha gharama hizo kwani mtu anaweza kuanda kazi yake kupitia simu janja yake akaituma kwa njia ya baruapepe kupitia simu yake hiyo huku usiri wa taarifa zake kuwa mkubwa au kutumia application mbalimbali zinawezoweza kurusha jumbe hizo, vilevile kwa watu wanaofanya udahili wa vyuo vikuu na vyuo vya kati wanaweza kutumia njia ya simu zao za mkononi hususani simu janja kwa ajili ya udahili wa vyuo.

Scan, kwa miaka ya nyuma maduka ya viandikia ndio yaliyokuwa yakitoa huduma za kuscan hususani vitu kama vyeti vya kuzaliwa , elimu ili kuleta uthibitisho kwamba vina uhalali kisheria kwa muhusika huyo ambaye alikuwa anavitumia hii pia imeathirika na ukuaji wa teknolojia kwani kupitia pia simu janja mtu anaweza kuscan vyeti vyake kwa matumizi anayoyahitajia pale anapokuwa amehitaji pia imepunguza gharama za fedha kwa watu ila imeendelea kuathiri kwa watu wa biashara ya maduka ya viandikia.

Biashara ya viandikia,kukua kwa teknolojia kumeanza kupunguza pia matumizi na manunuzi ya viandikia kama kalamu na vitu mbalimbali kama chaki kwani watumiaji wa kubwa wa vifaa hivyo zilikuwa ni taasisi za elimu mfano kwa taasisi za elimu ya juu yani (vyuo vikuu na vyuo vya kati) wamehamia katika utaratibu wa kutumia teknolojia ya progector katika uwasilishaji wa ufundishaji na uwasilishaji wa kazi za wanafunzi wao kwa njia hii ambayo pia imepunguza matumizi ya chaki ambayo yalikuwa yanaleta magonjwa katika njia ya hewa kutokana na athari ya vumbi litokanalo na chaki, hii pia imeanza kutumika na baadhi ya shule za sekondari za binafsi, pia ufanyaji wa kazi za kila siku wa vyuo vingi umeamia katika uwasilishaji wa kazi kwa njia ya baruapepe kwahiyo uuzaji wa karatasi umeeanza kupungua kwa matumizi hayo.

Uuzaji wa vitabu na mitihani, kwa miaka mingi watu walilazimika kununua mitihani ya nyuma ya kitaifa katika maduka ya viandikia kwa ajili ya maendeleo lakini tunaona kwa sasa baraza la mitihani kwa nchi yetu limekuwa likiiachia mitihani hiyo kwa njia ya mtandao nakila mtu mwenye uhitaji kuweza kufanya, vitabu vya kiada mara nyingi vilikuwa vikipatikana katika maduka makubwa ya viandikia ila kwa sasa teknolojia imekuwa na vitabu vingi vimeanza kupatikana kwa njia ya mtandao kwa upande wa mtandao vinaweza kupatikana pia kwa baadhi ya shule wameanza kutumia simu janja ambazo hazina mfumo wa upigaji wa simu wala ujumbe mfupi ila zina uwezo wa kuingizwa notes mbalimbali na kutumika kwa ajili ya kujisomea hii pia imepunguza mzigo mkubwa wa kubeba vitabu kwa wanafunzi wao.

Hayo ni mambo machache ambayo yalikuwa yakisababisha biashara ya maduka ya viandikia kuwa kubwa ila kwa miaka ya karibuni tumeona kwamba biashara hizo zimeanza kushuka biashara imeanza kuwa kwa watu wachache hambao bado hawana elimu ya matumizi ya njia hizi , pia imekuwa ikitumika na watu wachache hususani waliopo nje ya mji ambapo maendeleo ya teknolojia na elimu bado sio kubwa hivyo ila imesaidia kupunguza gharama kwani asilimia kubwa ya maduka ya viandikia yalikuwa yakitoa huduma hiyo kwa gharama kubwa kwa watu ambapo kwa sasa watu wameanza kuhama kwa kiasi kikubwa mfano kwa vyuo vikuu tuuh vya habari watu walilazimika kutoa magazeti ya chuo kwa njia ya nakala za karatasi kwa gharama kubwa ambapo kwasasa inakuwa ni tofauti , teknolojia imerahisisha wanatumia gharama ndogo sana ya internet kufikisha kazi zao kwa njia ya baruapepe au mitandao ya kijamii.

Muandaaji n : RASHID ATHUMAN MSIRI. rashidmsiri@gmail.com,Thanks.
 
Yani mm nimetoka kuscan makolokolo yangu Kwa nguvu ya bando no stress 😀
 
Back
Top Bottom