Nawaza kijinga jinga tuu

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
Nimekuwa kimya kwa siku kadhaa nikiutazama muelekeo wa siasa zetu za upinzani haswa sasa tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa October 2020. Naona mapicha picha tuu.

Dhana ya kuona wengine CCM B inazidi kusambaa na wasambazaji wakubwa wakiwa ni Chadema na viongozi wao, yaani hadi kiongozi mkubwa tu kama Mdee naye anashiriki kuita wenzake CCM B.

CUF waliitwa Ccm B na Chadema kisha wakaungana Kuunga UKAWA, walipoulizwa uCcm B wa CUF wakatafuna maneno baada ya CUF msalaba wa Ccm B ukawaangukia ACT na Zitto akapewa cheo cha Yuda escsriot wa siasa za mageuzi.

Mwaka huu mwanachama mwenza wa UKAWA ambae ni NCCR anageuka kuwa Ccm B, kisa anakijenga chama chake. Jamani vyama viache kujijenga kisa vitaonekana Ccm B? Vyama vikatae wanachama wapya kisa vitaonekana Ccm B? Huu ni ujinga ujinga unaoanza kuonekana tabia ya Chadema.

Eti kwenda Ikulu, kwenye awamu ya Kikwete Chadema walienda Ikulu mara nyingi zaidi kuliko wapinzani wowote waliowahi kutokea nchi hii na hakuna yeyote aliyewaita Ccm B, Chadema wameenda Mwanza kuomba ushirikiano na serikali hakuna yeyote aliyewaona wanatumika.

Leo Mbatia kuonana na Rais kwa malengo yaleyale ya kuimarisha umoja na mshikamano wa nchi hii anaonekana mamluki, mole na kibaraka wa Ccm. Mbona Maalim alienda na tangu atoke huko hakuna anayemuita Ccm B.

Hofu yao ni Nccr kusema wanataka kuwa chama kikuu cha upinzani? Kama wamejipima na kuona hio ni hatua namba moja kuelekea hatua ya pili kuing'oa Ccm. Chadema wameongoza kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa miaka kumi mfululizo awamu mbili ni lazima wawe na nguvu zote za kuing'oa Ccm Nccr lazima ipambane kupata wabunge ili nafasi ya Ccm ichukuliwe na Chadema na nafasi ya Chadema uchukuliwe na Nccr Ccm ifutike kabisa.

Tafakuri yangu ya kijinga jinga inaniambia Chadema wanahofu ya kupokonywa dhamana ya kuwa vibaraka wa Ccm na Nccr, Chadema ni mamluki na ndio maana kila uchaguzi unapokaribia wataleta migogoro ya ndani ili watu wapoteze mori ya mabadiliko.

Ndatama Hassan
255684711398_status_5f3cfd0aa4024f0988d1fbaef47de402.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli unawaza kijinga jinga sana tu, ila kuna mahala umewaza vizuri ujinga ulikuwa kidoooogo sana. Chadema hawana Jipya, sera zao ni Matusi kwa Rais na Viongozi wengine wa serikali. Halima mdee na Lema akili zao zinapaswa kupimwa kama ziko sawa sawa...!
Huenda namimi nawaza kijinga jinga, ila sio hivyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom