Naomba ushauri kuhusu matumizi ya samadi kilimo cha mahindi

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
Habari za humu ndani wadau, nimesoma maandiko mengi na kusikiliza wataalamu wengi juu ya kilimo cha mahindi.

Wapo wanaosema unaweza tumia viua magugu km round up kuandaa shamba badala ya kulima. Hili wadau mnasemaje

Na pili ni kwenye matumizi ya mbolea. Nataka kupanda kwa kutumiwa mbolea ya samadi, swali naweza pia tumia sanadi haswa ya Ng'ombe kukuzia?

Asanteni
 
Nimelima mahindi miaka zaidi ya miwili maeneo tofauti.

Nachoweza kusema kwa hapa Tanzania Lima mahindi kama
Unalima for funny ila usitegemee faida
 
Nimelima mahindi miaka zaidi ya miwili maeneo tofauti.

Nachoweza kusema kwa hapa Tanzania Lima mahindi kama
Unalima for funny ila usitegemee faida
Mkuu nimewahi kulima ya kuchoma nilipata mkuu. tena mwishowe nilipata zaidi maana mengine nilichoma mwenyewe. nililima kwa mfereji na ilikuwa ni off season. Hekari moja tu mkuu. changamoto ilikiwa ni ngedere lakini tuliwadhibiti.
 
mkuu kuhusu hizo dawa za magugu sina uzoefu nazo lakini ili kuokoa gharama kwenye mbolea. ni vyema kabla ya kuweka mbolea ni vyema upime udongo ili kujua ni nini kimepungua. vile vile utaweza kukua aina gani ya mbegu itafanya vizuri kwenye udongo huo.
na inawezekana ndani ya shamba moja kukawa na udongo tofauti tofauti au hali tofauti napo pia unaweza kushauriwa kitaalamu. kwa mfano kuna eneo lenye mwinuko, unyevu zaidi, hali ya mawemawe utashauriwa uweke mbegu gani na uongoze madini gani kwenye udongo. au uweke mbolea kiasi gani. hii itasaidia sana kuokoa gharama. maana unapoweka tuu mbolea bila kupima unaweza kukuta kuna madini ya aina fulani zaidi nawe ukayaongezea na ukaharibu udongo na kupata matokeo usiyotarajia.

Ni vyema mtaalamu afike eneo husika. au kama ataagiza sample zichukuliwe na mtu mwenye utaalamu huo.
 
Samadi is the best kwenye kilimo cha mahindi. Ntakushauri jinsi ya kuitumia
1.Kwanza weka alama kwenye shamba lako sehemu ambazo mazao huwa hayafanyi vizuri.
2. Rundika Samadi( ya ngo'mbe au mashudu ya nyanya)maeneo hayo kipindi cha kiangazi km sasa.
Mwezi wa 11 sambaza hiyo samada tayari kwa kulima shamba lako.
3.Ukishapanda wakati mahindi yana wiki 2 weka mbolea ya kuku kwenye shina la muhindi. Hapo utakuwa umeroga shamb lako.

Faida za kutumia samadi.
1.Kuboresha afya ya udongo( Soil health)
2. Huboresha au kurudisha Bionuai kwenye udongo( Biodiversity). Yaani uwepo wa wadudu mbalimbali kwenye udongo.
3. Hupunguza/ hurekebisha kuchachuka kwa udongo( Soil PH)
4. Husaidia udongo kutunza unyevunyevu
5.Huboresha soil structure and texture( Sijui kwa Kiswahili) n.k

NB mbolea ya ng'ombe inatumika kipindi cha kupanda na si kipindi cha kukuzia kwasababu inafanya kazi polepole kwa mda mrefu. Mbolea ya kuku ina nguvu ila inafanya kazi kwa msimu tu.

Pamoja na kutumia samadi ni muhimu kuweka mbolea ya kukuzia ya viwandani kwani samadi haina virutubisho vyote hasa Micronutrients km Zink,Sulfur n.k
 
Mashudu ya nyanya ni moja kati ya samadi bora sanaa
20220616_142602.jpg
20220616_142744.jpg
20220616_142624.jpg
 
Nimelima mahindi miaka zaidi ya miwili maeneo tofauti.

Nachoweza kusema kwa hapa Tanzania Lima mahindi kama
Unalima for funny ila usitegemee faida
Panda mbegu Hybrid zinazohimili ukame , kabla uandae shamba vizuri na palizi na mbolea za dukani ...Mimi nalima mahindi ni sehemu napata faraja kwakweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom