Mwalimu ajinyonga huko Moshi kisa riba kubwa ya mkopo

Jun 20, 2023
66
74
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Ebenezer iliyopo Sango mkoani Kilimanjaro, Anthony Sulle amefariki dunia kwa kujinyonga.

Habari kutoka Moshi zinadai kuwa kabla ya kujinyonga marehemu aliandika ujumbe unaoelezea kisa cha yeye kuchukua maamuzi hayo magumu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ujumbe huo unadai kisa cha marehemu kuchukua maamuzi hayo ni kitendo cha Mwajiri wao kuwapa mikopo walimu yenye riba kubwa (kaushadamu)

Ujumbe huo unadai kuwa riba hiyo kubwa imemfanya kuishi kwa shida kwani kila mwisho wa mwezi amekuwa akijikuta hana chochote.

Hata hivyo mmoja wa wakurugenzi wa shule hiyo, Doreen Makundi hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo kwa kile alichodai hahusiki kwa namna yoyote.

Kazi kwenu waalimu na mikopo kausha damu.
 
Pole sana,nadhani marehemu kuna sehemu kaficha,salary slip yangu haipumui ila sina mpango wa kujinyonga na wala sijawahi hlkuwaza huu upuuzi,yeye kakwama wapi?

Mimi nikisikia habari za taasisi kukopesha fedha lazima nitie mguu,poor and coward teacher kafa na kuacha huzuni kwa ndugu
 

Attachments

  • Screenshot_20240510-162451~2.png
    Screenshot_20240510-162451~2.png
    377 KB · Views: 3
Back
Top Bottom