Mungu aweza kukutoa kwenye hiyo shida!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
10,021
20,256
AMINI AHADI ZA MUNGU ZITATOKEA KWAKO

HESABU 23:19
, Mungu si mtu, aseme uongo, wala si mwanadamu, ajute, iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza? (Ref: 1Samwel 15:29, Malaki 3:6, Tito 1:2)

1FALME 8:56, Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israel kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lolote katika ahadi yake njema aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake. (Ref; Kumb 12:10, Yoshua 21:45, Yoshua 23:14).

YEREMIA 1:12, Ndipo Bwana akaniambia, umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize. (hii maana yake nini?, anatafuta wapi alisema kitu ili akitimize vilevile kama alivyosema, anaangalia alichokisema ili akitimize, analinda kile alichokisema hadi kitimizwe, yupo nyuma ya chochote alichokisema hadi kitimie).

Labda kama Mungu hakutamka, ila maadamu alikisema, lazima kitatimia chote.

Hebu jiulize, una sababu gani ya kutoamini kile Mungu alichokisema? Ni kwamba unaona Mungu hawezi kufanya au vipi? Hauoni kuwa unaposhindwa kuamini kuwa Mungu atafanya jambo alilolisema unakuwa unamdharau kwamba hana uwezo? Hizo ni dharau, kwanini usiamini kuwa anaweza kufanya? Kwanini unamtilia mashaka?

Basi, kama kuna kitu cha kukitilia mashaka maishani mwako, sio Mungu, unapaswa kutilia mashaka hayo mashaka yako wewe mwenyewe kwasababu huna uhakika kama mashaka yako yana mashiko yeyote, huna uhakika kama Mungu hatafanya hivyo yatilie mashaka mashaka yako mwenyewe. Usiyaamini mashaka yako, lakini usije kuwa na Mashaka na Mungu, yeye sio mtu hata aseme uongo, wala sio mwanadamu hadi ajutie kile alichokisema kwamba kwanini alikisema labda kwasababu hakitatokea.

Jifunze leo, wanadamu huwa wanaahidi vitu vingi ila baadaye wanaanza kujuta kwanini waliahidi kwasababu wanajikuta hawawezi kutimiza, kwa Mungu ni tofauti, yeye sio mwanadamu hadi ajutie kile alichokisema labda kwasababu ameona hataweza kukifanya, HAKUNA alichowahi kukitamka akashindwa kukitimiza. Pia yeye huliangalia Neno lake ili lisikae bure bila kulitimiza. ukiamini kile alichokitamka kuhusiana na hali uliyo nayo, kitatokea hata bila kuwekewa mikono, kwasababu namna pekee ya uhusiano wetu na Mungu ni kwa njia ya IMANI. pasipo imani hakuna aliyewahi kumpendeza Mungu, pasipo imani manake unamtilia mashaka Mungu unaona hana nguvu au kama hataweza au kama aliahidi uongo, na hiyo ni dharau kwake. Mwamini Mungu, soma Neno lake na uliamini.

ISAYA 55: 11 INASEMA
, ndivyo litakavyokua Neno langu litokalo katika kinywa changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yote niliyolituma.
 
Mungu amenifunua mambo mengi sana baada ya kupata tafakari hii. Kwanza jua Mungu anakupenda sana na anataka utoke kwenye hilo tatizo, anataka umuamini na umuombe, atakutoa, hilo ni sharti kuu, mwamini, usipoamini umeshindwa masharti. Kwenye Biblia kuna mistari mingi mno inayoonesha Mungu hajawahi kusema uongo, na huwa anaangalia wapi aliahidi ili apatimize, kama alisema anao uwezo kuponya wagonjwa, ukimkumbusha ahadi hiyo kwa imani, anakuponya, vivyo hivyo na kwenye mahitaji mengine, na hata kama hauna shida wewe kama mwanadamu unahitaji kuwa karibu naye ili ufurahie uwepowa wake, na yeye pia ameahidi kwamba "nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa mioyo yenu yote. Na kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. kwahiyo ni kazi kwako, yeye anapatikana. Mtafuteni BWana maadamu anapatikana, mwiteni maadamu yu karibu.
 
Mtu anajiamkia zake tu kashiba kiporo za makande anadai Mungu amesema ,mara mungu kamwonyesha.
Wala sijala kiporo cha makande wala chochote. Nimeweka vifungu vya Neno, Mungu amesema hivyo, na atatenda. Mwaminini Mungu, When we do our part, God is always faithful to do His part. nafasi yetu sisi ni kumwamini yeye na Neno alilolisema, na upande wake yeye ni kulitimiza, na hakika huwa analitimiza. Mungu sio mwanadamu hadi awe mwongo kama sisi wanadamu, wala huwa hajuti, amesema hivyo kwenye Neno lake na anatimiza hata leo hivi. uamini usiamini hivyo ndivyo.
 
Wala sijala kiporo cha makande wala chochote. Nimeweka vifungu vya Neno, Mungu amesema hivyo, na atatenda. Mwaminini Mungu, When we do our part, God is always faithful to do His part. nafasi yetu sisi ni kumwamini yeye na Neno alilolisema, na upande wake yeye ni kulitimiza, na hakika huwa analitimiza.
Allah au Yehova?
 
Asiponiokoa nikafa ni mpango wake

Nikipona jina lake lihimidiwe

Upuuzi mtupu.
huo mdomo unaotukana kuwa ni upuuzi ni Mungu mwenyewe ameushikilia uwe mzima ili uendelee kuongea. wapo watu vitandani sasaivi hata kunyanyua tu mdomo waongee neno moja hawawezi, ila wewe Mungu bado anakujaalia, na bado unatukana kuwa ni upuuzi. jitafakari na Mungu akufungue ufahamu umjue na uwe mtu mwema.
 
Kwanini asiwe Allah mmoja tu asie na mshirika , au kwanini asiwe Mungu wa babu zako awe wa isaka na yakobo?
kwasababu allah sio Mungu wa kweli, ni shetani mwenyewe yaani Ibilisi aliyekuja kupotosha Neno la Mungu wa kweli. pia hapa sipo kwa ajili ya malumbano ya dini, wewe kama allah wako alishawahi kukusaidia chochote utajua mwenyewe ila kwa upande wangu nimethibitisha kuwa Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo aliyefanyika mwili kwa njia ya Yesu Kristo awe kafara la kutukomboa, huyo pekee ndiye Mungu. mababu zako pia walikuwa na miungu mashetani. mwamini Mungu wa kweli.
 
huo mdomo unaotukana kuwa ni upuuzi ni Mungu mwenyewe ameushikilia uwe mzima ili uendelee kuongea. wapo watu vitandani sasaivi hata kunyanyua tu mdomo waongee neno moja hawawezi, ila wewe Mungu bado anakujaalia, na bado unatukana kuwa ni upuuzi. jitafakari na Mungu akufungue ufahamu umjue na uwe mtu mwema.
Kwanini wewe UPO?

Alishasema "Niko ambae Niko"

Jibu kwanza hilo swali
 
huo mdomo unaotukana kuwa ni upuuzi ni Mungu mwenyewe ameushikilia uwe mzima ili uendelee kuongea. wapo watu vitandani sasaivi hata kunyanyua tu mdomo waongee neno moja hawawezi, ila wewe Mungu bado anakujaalia, na bado unatukana kuwa ni upuuzi. jitafakari na Mungu akufungue ufahamu umjue na uwe mtu mwema.
Nani kawafanya waumwe kama sio huyo mungu

Imani potofu hizi mimi nakuambia
 
shetani ndio kawafanya waumwe, hata wewe shetani anaweza kukufanya uumwe, wala sio Mungu. Mwivi (yaani shetani) haji ila kuua kuchinja na kuharibu. unapoamua kutokukaa mikononi mwa Mungu, unakuwa exposed kwa shetani anaweza kukufanya chochote atakacho, akiamua kukuua anakuua, akiamua uwe mgonjwa anakufanya hivyo, akitumia wachawi wakuloge anafanye, akiamua upate ajali unapata, akiamua uwe vyovote anakuchezea apendavyo.

ukiwa mikononi mwa Mungu, yeye ni ngao yako, hata ukipatwa na mabaya jua labda umefungua mlango kwa kutenda dhambi ukampa shetani nafasi akaingia na kukudhuru, au Mungu ameruhusu kwa kupunguza ulinzi kwa ajili ya mapenzi yake labda anakufundisha kitu au vyovyote vile, lakini bado yupo pamoja nawe.

Biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele. ni ajabu kwamba, tunaposema Mungu anaweza kukuponya na tumeweka mistari, wewe unakuja kusema hizi ni imani potofu, hauoni kama umefungwa ufahamu na shetani? imani potofu ipi sasa kati ya hiyo mistari niliyoiweka?
 
AMINI AHADI ZA MUNGU ZITATOKEA KWAKO

HESABU 23:19
, Mungu si mtu, aseme uongo, wala si mwanadamu, ajute, iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza? (Ref: 1Samwel 15:29, Malaki 3:6, Tito 1:2)

1FALME 8:56, Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israel kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lolote katika ahadi yake njema aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake. (Ref; Kumb 12:10, Yoshua 21:45, Yoshua 23:14).

YEREMIA 1:12, Ndipo Bwana akaniambia, umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize. (hii maana yake nini?, anatafuta wapi alisema kitu ili akitimize vilevile kama alivyosema, anaangalia alichokisema ili akitimize, analinda kile alichokisema hadi kitimizwe, yupo nyuma ya chochote alichokisema hadi kitimie).

Labda kama Mungu hakutamka, ila maadamu alikisema, lazima kitatimia chote.

Hebu jiulize, una sababu gani ya kutoamini kile Mungu alichokisema? Ni kwamba unaona Mungu hawezi kufanya au vipi? Hauoni kuwa unaposhindwa kuamini kuwa Mungu atafanya jambo alilolisema unakuwa unamdharau kwamba hana uwezo? Hizo ni dharau, kwanini usiamini kuwa anaweza kufanya? Kwanini unamtilia mashaka?

Basi, kama kuna kitu cha kukitilia mashaka maishani mwako, sio Mungu, unapaswa kutilia mashaka hayo mashaka yako wewe mwenyewe kwasababu huna uhakika kama mashaka yako yana mashiko yeyote, huna uhakika kama Mungu hatafanya hivyo yatilie mashaka mashaka yako mwenyewe. Usiyaamini mashaka yako, lakini usije kuwa na Mashaka na Mungu, yeye sio mtu hata aseme uongo, wala sio mwanadamu hadi ajutie kile alichokisema kwamba kwanini alikisema labda kwasababu hakitatokea.

Jifunze leo, wanadamu huwa wanaahidi vitu vingi ila baadaye wanaanza kujuta kwanini waliahidi kwasababu wanajikuta hawawezi kutimiza, kwa Mungu ni tofauti, yeye sio mwanadamu hadi ajutie kile alichokisema labda kwasababu ameona hataweza kukifanya, HAKUNA alichowahi kukitamka akashindwa kukitimiza. Pia yeye huliangalia Neno lake ili lisikae bure bila kulitimiza. ukiamini kile alichokitamka kuhusiana na hali uliyo nayo, kitatokea hata bila kuwekewa mikono, kwasababu namna pekee ya uhusiano wetu na Mungu ni kwa njia ya IMANI. pasipo imani hakuna aliyewahi kumpendeza Mungu, pasipo imani manake unamtilia mashaka Mungu unaona hana nguvu au kama hataweza au kama aliahidi uongo, na hiyo ni dharau kwake. Mwamini Mungu, soma Neno lake na uliamini.

ISAYA 55: 11 INASEMA
, ndivyo litakavyokua Neno langu litokalo katika kinywa changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yote niliyolituma.
Ameen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom