Mbunge Kimei atembelea miradi ya maendeleo, amshukuru Rais Samia

MTANZANIA620

Member
Jun 20, 2023
37
38
Na Mwandishi Wetu
Vunjo - Moshi

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ametembelea Kata ya Kirua Vunjo Kusini na Kirua Vunjo Mashariki zilizopo tarafa ya Vunjo Magharibi kwa madhumuni ya kukagua mradi wa kuboresha huduma ya maji katika kijiji cha Yamu Makaa unaogharimu shilingi milioni 576, shule ya sekondari Pumuani iliyogharimu shilingi milioni 584, zahanati mpya ya Kileuo iliyogharimu shilingi milioni 125 itakayohudumia watu 13,245 toka vijiji vitatu vya Kileuo, Mero na Mrumeni pamoja na kukagua ujenzi wa madarasa matano kwa shilingi milioni 100 shule ya msingi Mrumeni.

Aidha, Mhe Dkt ameishukuru serikali ya CCM Awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika kata ya hizi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.385 ambayo imejikita katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

Mbunge Kimei amewapongeza madiwani wa Kata hizo Mhe Peter Meela na Mhe Alex Umbella pamoja na Kamati zao za ujenzi kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo na kuwasisitiza kazi zilizosalia kwa baadhi ya miradi hiyo wahakikishe zinakamilika kwa wakati ili ianze kutumika na wananchi waanze kupata huduma.

"Kwa dhati ya Moyo wangu napenda kumshukuru Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake kwetu wanavunjo kwani katika miaka yake mitatu madarakani tumepokea takribani shilingi bilioni 39 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo hii tuliyoikagua. Nawapongeza wote waliohusika katika usimamizi na utekelezaji wake kwa kazi nzuri. Tujitahidi tukamilishe kazi zilizosalia kwa baadhi ya miradi ili sasa tuanze kunufaika nayo." Amesema Dkt Kimei

Akijibu kero za wananchi, Mbunge Kimei amewahakikishia wananchi kwamba ahadi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Uchira, Kisomachi mpaka Kolarie ipo palepale na kwamba wataendelea kuifuatilia kwa ajili ya utekelezaji wake kwa kuwa hatua muhimu za awali zimeshakamilika ikiwemo kuanza kwa kazi hiyo kwa kipande cha kilomita moja kati ya nne zinazotakiwa kujengwa.

Katika hatua nyingine wananchi wa kata ya Kirua Vunjo Mashariki kupitia taasisi ya maendeleo ya jamii hiyo waishio Dar es Salaam iitwayo Lekidea walinunua eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari tano kwa shilingi milioni 30 ambapo leo diwani wa kata hiyo Mhe Alex Umbella amekabidhi hati hiyo ya manunuzi kwa Mbunge Kimei ili sasa anze juhudi za kupata fedha za kuanza ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Diwani wa kata ya Kirua Vunjo Mashariki Mhe Alex Umbella amemshukuru Rais Samia kwa miradi mikubwa ndani ya kata hiyo na pia amemshukuru Mbunge Kimei kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kuwaletea wananchi maendeleo na hasa ujenzi wa zahanati ya kwanza kujengwa na serikali - zahanati ya Kileuo ambayo imeanza kutoa huduma hali iliyowapunguzia wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma pamoja na unafuu wa gharama kwa huduma zinazotolewa.
 
Kimei muda umekwenda kasi sana na bado yale ma-skills yako ya crdb watu wamegoma kukuona ukapaisha bado wamemng'ang'ania jamaa mmoja kaamua kuingia kwenye biashara ya soka japo haimpendi lakini kila kukicha ananunua timu!
 
Back
Top Bottom