Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,865
- 4,693
Zaidi ya wananchi 1,000 wa Kijiji cha Namwangwa, Kata ya Hezya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, wamekosa huduma za afya kwa miezi mitatu sasa, baada ya tabibu anayehudumu kwenye zahanati ya kijiji hicho kustaafu.
Wananchi hao wamekumbwa na changamoto hiyo baada ya mhudumu wa awali kustaafu tangu Novemba, 2023 na Serikali ilipeleka tabibu mwingine Februari, 2024 lakini mwezi uliopita amehamishwa na kusababisha zahanati hiyo ifungwe.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Digital leo Jumanne Aprili 16, 2024 kijijini hapo, baadhi ya wananchi wamesema zahanati hiyo ambayo ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 50 kwa siku, ilikuwa msaada mkubwa kwao, lakini sasa wanalazimika kufuata huduma maeneo mengine.
Mwananchi Digital imemtafuta Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Alex Mugeta ambaye amekiri zahanati hiyo kufungwa kwa kukosa mhudumu.
Hata hivyo, amesema tayari wameanza utaratibu wa kumpata tabibu mwingine na watakamilisha muda si mrefu, japo hakutaja ni lini hasa atapatikana.